Uchanganuzi wa Kimofosintaksia wa Viangami katika Lugha ya Kiswahili.
Ikisiri
Dhamira ya makala haya ni kuonyesha sheria zinazozingatiwa wakati wa kuambisha viangami katika lugha ya Kiswahili. Viangami ni mofimu zinazojisimamia kisintaksia lakini kifonolojia ni tegemezi. Uchunguzi huu umeongozwa na nadharia Boreshaji. Kwa mujibu wa Nadharia Boreshaji, lugha yoyote ile ulimwenguni ina maumbo ya ndani na maumbo ya nje (Prince na Smolensky,1993). Maumbo haya hutumika kuzalisha maumbo tokeo tofauti. Umbo la nje hutokea baada ya umbo la ndani kubadilishwa. Data iliyotumika katika utafiti huu ilipatikana maktabani. Vitabu mbalimbali vya kisarufi na isimu vilitumika. Usampulishaji wa kimakusudi ulitumika. Vitabu vilivyochapishwa kwa lugha ya Kiswahili viliteuliwa kimakusudi. Vitabu hivi ni pamoja na riwaya, tamthilia, mashairi na vitabu vya kiada. Data ilikusanywa kwa mbinu ya kusoma na kunukuu. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Baada ya utafiti, imebainika kuwa shughuli ya kuambisha vipashio vya kisarufi hufanywa kwa uangalifu mkubwa sana. Data iliyopatikana inaweka wazi uambishaji wa viangami katika lugha ya Kiswahili. Utafiti huu utawafaa walimu, wanafunzi na wataalamu wa isimu. Pia waandishi wa kazi za isimu na fasihi watafaidika.
Upakuaji
Marejeleo
Alotaiby, F., Foda, S. and Alkharashi, I. (2010). Clitics in Arabic Language: A Statistical Study. Saudi Arabia: King Saud University.
Anderson, S.T. (2010) Clitics. Cambridge: Cambridge University Press.
Kager, R. (1999). Optimality Theory. Cambridge. Cambridge University Press.
Mgullu, R. (2001). Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn.
Polyglossia (2013). Multilingualism: Language Policy. Georgetown University Press.
Prince, A. and Smolensky, P. (1993). Optimality Theory: Constraints Interaction in GenerativeGrammar. Rutgers Center for Cognitive Science: Rutgers University.
Spencer, A. and Luis, A. (2012). Clitics: An Introduction. Cambridge: Cambridge University Press
Copyright (c) 2022 Naomi Ndumba Kimonye, Leonard Chacha Mwita, PhD

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.