Athari za Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi Katika Fonolojia Arudhi

  • Cheruiyot Evans Kiplimo Chuo Kikuu Cha Kenyatta
  • Leonard Chacha Mwita, PhD Chuo Kikuu Cha Kenyatta
Keywords: Fonolojia Arudhi, Kusambaa Kwa Shadda, Likwidi, Shadda, Silabi Na Udondoshaji Wa Kihistoria
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kiswahili ni lugha mojawapo ya Kiafrika inayochangia ujifunzaji wa fonolojia. Wanaisimu wamejadili mifanyiko ya kifonolojia katika Kiswahili bila kugusia swala la athari zake katika vipashio vikubwa kuliko fonimu. Hata hivyo, siyo mifanyiko yote ya kifonolojia ndio huathiri fonolojia arudhi ya lugha husika. Fonimu zinapoungana ili kuunda vipashio vikubwa vya lugha kama vile silabi na neno, zinaathiriana katika viwango mbalimbali. Athari zingine huwa ndogo kiasi kwamba hazionekani bayana ilhali athari zingine huwa kubwa kiasi cha kuonekana bayana. Mfanyiko wa kifonolojia unaohusishwa na utowekaji wa fonimu ni udondoshaji. Fonimu inapotoweka katika neno, vipashio vikubwa kuliko fonimu yenyewe hupokea athari katika mfumo wa lugha. Makala hii inaonyesha jinsi mabadiliko ya udondoshaji wa kihistoria wa fonimu za likwidi huathiri fonolojia arudhi ya Kiswahili. Hili liliwezekana kwa kujenga umbo la awali la neno kisha kuonyesha jinsi kudondoshwa kwa fonimu kuliathiri fonolojia arudhi. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya fonolojia zalishi iliyoasisiwa na Chomsky na Halle (1968). Makala hii, imetegemea data ya maktabani iliyokusanywa kwa kusoma, kudondoa na kunakili.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Carr, P. (2013). English Phonetics and Phonology: An Introduction (2nd ed.). Malden: Wiley-Blackwell.

Chomsky, N & Halle, M. (1968) Sound Pattern of English. New York: Harper & Row.

Clements, G.N. & Keyser, S.J. (1983). CV Phonology: A Generative Theory of the Syllable. Cambridge Mass: The MIT Press

Crystal, D. (2008). A Dictionary of Linguistics and Phonetics. (6th ed). London: Blackwell Publishing.

Fromkin, V., Rodman, R. & Hyams, N. (2003). An Introduction to Language (7th ed.). Washington D.C: Thomson Wadsworth

Fudge, E. (1987). Branching Structure within the Syllable: Journal of Linguistics, Vol. 23, No. 2, pp. 359-377.

Hayes, B. (2009). Introductory Phonology. Malden: Blackwell Publishing.

Katamba, F. (1989). An Introduction to Phonology. London: Longman Publishers.

Kiplimo, C. E. &. Mwita L. C. (2021). Thibitisho la Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi. East African Journal of Swahili Studies, 4(1), 43- 57. https://doi.org/10.37284/eajss.4.1.474.

Massamba, D. P. B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa. Dar es Salaam: TUKI.

Massamba, D. P. B. (2011). Maendeleo katika Nadharia ya Fonolojia. Dar es Salaam: TATAKI.

McMahon, A. (2002). An Introduction to English Phonology. Edinburgh: Edinburgh University Press.

Mwaliwa, H. C. (2014). An analysis of the syllable structure of standard Kiswahili loan words from modern standard Arabic. [Unpublished Ph.D thesis, Univesity of Nairobi].

Mwangi, I. (2008). A synchronic segmental morphophonology of standard Kiswahili. [Unpublished Ph.D thesis, University of Nairobi].

Njogu, N., Mwihaki, A. & Buliba, A. (2006). Sarufi ya Kiswahili: Uchanganuzi na Matumizi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Obuchi, S. M. & Mukhwana, A. (2010). Muundo wa Kiswahili: Ngazi na vipengele. Nairobi: A- Frame Publishers.

Okal, B.O. (2015). Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili. Kioo cha Lugha Juz. 13, pp. 103-124.

Pike, K. & Pike, E.V. (1947). Immediate Constituents of Mazateco Syllables. International Journal of American Linguistics, 13, pp. 78–91.

Roach, P. (2009). A little Encyclopaedia of Phonetics. Cambridge: Cambridge University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
13 Januari, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Kiplimo, C., & Mwita, L. (2022). Athari za Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi Katika Fonolojia Arudhi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 12-24. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.527