Jinsi Leksimu za Mitishamba Zinavyoakisi Uhifadhi wa Mazingira ya Waswahili Nchini Kenya

  • Nelly Bonareri Karoli Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Leonard Chacha Mwita, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Waswahili, Mitishamba, Leksimu, Uhifadhi, Mazingira
Sambaza Makala:

Ikisiri

Lugha na utamaduni wa watu ni vitu visivyoweza kutenganishwa. Mifumo ya lugha huathiri namna binadamu anavyofikiri kuhusu ulimwengu wake na husababisha matendo ambayo ni kiini cha changamoto za kiikolojia wanazokabiliana nazo. Katika makala hii, tulichambua namna leksimu za mitishamba zinachukuliwa kama ishara za uhifadhi wa mazingira katika mifumo ya ikolojia katika jamii ya Waswahili. Data ilikusanywa kwa mbinu ya mahojiano kutoka kwa Waswahili wa Mvita. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya semiotiki ikolojia iliyotusaidia kuelewa kuwa kile kilichotambuliwa kama athari kwa ikolojia mara nyingi huwa na sababu za kisemiotiki na tofauti katika kufasiri ishara au misamiati. Tulibainisha kuwa kuna leksimu za mitishamba kama ‘mpambamwitu’ ambayo Waswahili walitumia kuonyesha ile hali ya kurembesha misitu yao kwa kuleta taswira ya kiasili na mwonekano mzuri wa kipekee, ‘linda ziwa’ iliakisi uhifadhi wa vyanzo vya maji. Mahali ambapo ulimea, maji yalikuwa safi na tayari kutumika katika shughuli za pale nyumbani. Mti huu ulifananishwa na jokofu kwani hata nyakati za joto ulipoenda mtoni ungepata maji hayo ni baridi na safi. Waswahili ambao walikuwa ni watumiaji wa leksimu hizi walionyesha kuwa ilipofikia suala la uhifadhi wa mazingira, wanajamii walijitahidi kutunza mazingira yao. Jinsi tunavyochagua misamiati yetu katika mawasiliano kuhusu mazingira kunaweza kubadilisha jinsi wanajamii wanavyoyaona mazingira hayo. Ikolojia inategemea mawazo yaliyopo, kanuni, na sheria za jamii. Makala hii imapendekeza kuwa kwa kubadilisha jinsi tulivyoyatazama mazingira yetu ya asili tunaweza kutambua thamani yake halisi. Kwa kuiweka thamani hiyo katika sera zetu mipango na mifumo ya uchumi, tunaweza kuelekeza uwekezaji katika shughuli ambazo zinarejesha uasili wa mazingira yetu na tukapata faida. Kwa kutambua kuwa mazingira yetu ni mshirika wetu mkubwa basi tutayafanya kuwa endelevu.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Kokwaro, O. J (2009) Medicinal Plants of East Africa (3rd ed). Nairobi. University of Nairobi Press.

Kull, K. (2001). Semiotic ecology: Different natures in the semiosphere. Sign System Studies. 26(1), 344- 371. Retrieved from https://www.academia.edu/3882436/semiotic-ecology.

Lincoln, Y.S., & Guba, E.G. (1985). Naturalistic Inquiry. Newbury Park, CA: Sage.

Maran, T. (2007). Towards an integrated methodology of ecosemiotics: The concept of nature-text. Sign Systems Studies, 35(1/2), 269–294. Retrieved from https://doi.org/10.12697/10.12697/SSS.2007.35.1-2.10.

Maran, T. & Kull, K. (2014). Ecosemiotics: Main Principles and Current Developments. Geografiska Annaler. Series B, Human Geography, 96(1), 41-50. Retrieved from https://doi.org/10.1111/geob.12035.

Noth, W. (2001). Ecosemiotics and the semiotics of nature. Sign Systems Studies, 29 (1), 71–81. Retrieved from https://doi.org/10.12697/SSS.2001.29.1.06.

Nöth, W. and Kull, K. (2001). Introduction: Special Issue on Semiotics of Nature. Signs Systems Studies, 29(1), 9-11. Retrieved from https://doi.org/10.12697/SSS.2001.29.1.01.

Posner, R. (2000). Semiotic Pollution: Deliberations towards an ecology of signs. Sign Systems Studies, 28, 290–307. Retrieved from https://doi.org/10.12697/SSS.2000.28.16.

Tarehe ya Uchapishaji
27 September, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Karoli, N., & Mwita, L. (2023). Jinsi Leksimu za Mitishamba Zinavyoakisi Uhifadhi wa Mazingira ya Waswahili Nchini Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 374-381. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1469

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.