Mabadiliko katika Maudhui, Mtindo na Muundo Katika Fasihi

  • Simon Kiarie Mwangi Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Naomi Ndumba Kimonye Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Jamii, Uvumbuzi, Msambao, Fasihi, Muundo, Mtindo, Maudhui
Sambaza Makala:

Ikisiri

Fasihi na jamii ni vitu viwili ambavyo haviwezi kutenganishwa. Kwamba fasihi humulika yaliyo katika jamii na kwa upande mwingine jamii hutumia fasihi kuendeleza amali zao. Hivyo basi fasihi huwa kama kioo cha jamii kwa kuangazia tamaduni za jamii husika. Tamaduni za jamii husika hubadilika zinapoathiriwa kidaikronia. Kwa msingi huu fasihi hubadilika kulingana na mabadiliko yatokeao katika jamii hiyo. Makala haya yanadhamiria kuchunguza mabadiliko hayo ya kimaudhui, kimutindo na kimuundo katika fasihi ya kisasa kwa kuilinganishwa na fashi ya kale. Mabadiliko ni hali ambayo jamii fulani huchukua mambo mapya yanayotokea na kuyakubali kama sehemu ya utamamdi wayo. Kuna mabadiliko anuwai ambayo yameshuhudiwa katika uandishi wa kazi za fasihi za Kiswahili katika maudhui, wahusika, muundo na mtindo. Kazi za fasisi zitakazochunguzwa ni fasihi andishi hasa mashairi, riwaya, hadithi fupi na tamthilia. Lengo kuu la makala haya ni kutathimini mabadiliko hayo kwa kuchunguza asili yake na athari zake katika fasihi ya kisasa. Fasihi huwakilisha yanayotokea katika jamii na waandishi hutumia ubunifu wao kuyaangazia. Maudhui, wahusika, ploti na mtindo katika fasihi andishi hutokana na mambo yaliyo katika jamii. Kimsingi, utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Msambao wa Uvumbuzi. Nadharia hii inatambua hatua tatu kuu zinazohusishwa na usambazaji wa maudhui. Hatua hizi ni uvumbuzi, usambaaji na ukubalifu. Hatua hizi tatu za nadharia hii zilitumiwa kuendeleza utafiti huu. Data ya utafiti huu ilitoka maktabani na iliteuliwa kwa njia ya kimakusudi kutoka vitabu teule vya Kiswahili. Data ilikusanywa kwa kusoma vitabu, majarida na kusakura mtandaoni kupata data inayohusiana na kazi hii. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kimaelezo kwa kulinganisha kazi za fasihi za kale na kisasa. Matokea ya utafiti huu yalionyesha kuwa kuna mabadiliko yanayoshuhudiwa katika fasihi ya sasa hasa katika maudhui, mtindo na wahusika. Kwa mfano, imebainika kuwa mashairi ya kisasa yanalenga zaidi kupitisha ujumbe kuliko kubanwa na muundo wa mashairi arudhi. Matokea ya utafiti huu yatakuwa ya manufaa kwa waandishi wa kazi za fasihi, wanafunzi katika viwango tofauti vya elimu na wasomi katika nyanja tofauti kama anthropojia

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Arege, T.M. (2009). Mstahiki Meya. Nairobi: Vide-Muwa Publishers.

Arege, T. (2020). Bembea ya Maisha. Nairobi: Access Publishers.

Bukenya A, na Nandwa, J (1983). African Oral Literature for Schools. Nairobi. Longman Kenya.

Davies, S. (1976). The Diffusion of Process Innovations. Cambridge: Cambridge University Press.

Everett, R. M. (1962). Diffusion of Innovations. New York: The Free Press.

Griffin, E. (2000). A First Look at Communication Theory (8th Ed.). Boston: McGraw-Hill.

Hussein, E. N. (1970). Kinjeketile. Dar es Salaam: Oxford University Press.

Kea, P. (2016). Kigogo. Nairobi: Storymoja.

Hussein, E. (1971). Mashetani. Nairobi: Oxford University Press.

Kimonye, N. (2021). Mzigo. Nairobi: Rinny Educational and Technical Publishing.

Kimonye, N. (2022). Mwongozo wa Tamthilia ya Bembea ya Maisha: Maswali na Majibu.Nairobi: Rinny Educational and Technical Publishing.

Lutomia, D. & Muthama, P. (2019). Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine. Nairobi: Mountain Top Educational Publishers.

Matei, A. (2017). Chozi la Heri. Nairobi: One Planet Publishing Company.

Masebo, J.A & Nyangwine, N. (2007). Nadharia ya Fasihi. Dar es Salaam: Nyambari Nyangwine Publishers.

Mohamed, A. (1980). Utengano. Nairobi: Sasa Sema Publications.

Mumanyi, C. (2021). Nguu za Jadi. Nairobi: Queenex Publishers.

Robert, S. (1951). Kusadikika. Nchi iliyo Angani. London: Nelson.

Rogers, E.M. (1995). Diffusion of Innovation. New York. The Free Press.

Senkoro, F.E.M.K. (1987). Fasihi na Jamii. Dar es Salaam: Press and Publicity Centre.

Simiyu, W. F. (2011). Kitovu cha Fasihi Simulizi. Mwanza: Serengeti Bookshop

Thompson, S. (1946). The Folktale. London: University of California Press.

Walibora, K. & Mohamed, A. (2007). Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine. Nairobi: Moran (E.A.) Publishers Limited.

Wamitila, K. (2010). Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi. Nairobi: Focus Publication.

Wellek, R na Warren, A. (1949). Theory of Literature. New York: Harcourt, Brace.

Tarehe ya Uchapishaji
22 October, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Mwangi, S., & Kimonye, N. (2023). Mabadiliko katika Maudhui, Mtindo na Muundo Katika Fasihi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 403-411. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1531