Thibitisho la Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi

  • Cheruiyot Evans Kiplimo Chuo Kikuu Cha Kenyatta
  • Leonard Chacha Mwita Chuo Kikuu Cha Kenyatta
Keywords: Fonolojia Zalishi, Likwidi, Mbinu Linganishi, Udondoshaji, Uundaji Ndani
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kiswahili ni lugha ya Kibantu iliyofanyiwa uchanganuzi wa kisasa. Mabadiliko ya lugha yamechunguzwa katika matawi ya isimu yakiwemo isimu historia na isimujamii. Hata hivyo, tawi la isimu historia halijafanyiwa utafiti wa kuridhisha katika Kiswahili. Makala hii inatoa ithibati ya udondoshaji wa kihistoria wa fonimu za likwidi katika maneno teule ya Kiswahili. Nadharia ya fonolojia zalishi (FZ) ya Chomsky na Halle (1968) iliteuliwa kuongoza utafiti huu. Mbinu ya uundaji ndani (UN) na mbinu linganishi (ML) zilitumiwa kama malighafi ya kutoa ithibati ya udondoshaji huu. Kwa kutumia mbinu ya uundaji ndani, tofauti za kisinkroniki na ujumbe uliopo kuhusu etimolojia ya neno ulimsaidia mtafiti kuelewa leksika ya sasa. Mbinu linganishi ilitumika kulinganisha maneno ya Kiswahili na mengine ya lugha mnasaba (Ekegusii, Kikuyu, Kiluhya, Kimeru, Kitaita na Kikamba). Mbinu hizi zilijengana na kukamilishana kila moja ikifidia upungufu wa nyingine. Iwapo ushahidi upo kutoka kwa uundaji ndani kama mbinu ya uundaji upya wa leksika, mbinu linganishi ilitumika kuhakikisha usahihi wa ushahidi uliotolewa na mbinu ya uundaji ndani. Isitoshe, pale ambapo mbinu ya uundaji ndani ilikosa kutoa ithibati au kuwa na upungufu, mtafiti alirejelea mbinu linganishi ili kubaini umbo asilia la neno teule la Kiswahili. Data ya maktabani iliwekea msingi upataji wa data ya nyanjani ambayo ilikusanywa kupitia kwa maswali ya hojaji. Data imechanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo, majedwali na unukuzi wa sheria za kifonolojia. Makala hii ni nafasi bora ya kuchangia katika isimu historia, leksikografia na fonolojia ya Kiswahili.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

BAKITA. (2015). Kamusi Kuu ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.

Bostoen, K. & Bastin, Y. (2016). Bantu Lexical Reconstructions. Oxford Handbook Online: Online publication. https://doi.org/10.1093/oxfordhb/9780199935345.013.36

Botne, R. (1991). Variation and Word Formation in Proto-Bantu: The Case of *YIKAD. Afrika und Ubersf!, Band 74, pp. 247-268.

Campbell, L. & Mixco, M. J. (2007). A Glossary of Historical Linguistics. Edinburgh: Edinburgh University Press.

Campbell, L. (1999). Historical Linguistics: An Introduction: Cambridge. The MIT Press.

Chiraghdin, S na Mnyampala, M. (1977). Historia ya Kiswahili. Nairobi: Oxford University Press.

Chomsky, N & Halle, M. (1968) Sound Pattern of English. New York: Harper & Row.

Crane, B. L., Yeager, E. & Whitman, R. L. (1981). An Introduction to Linguistics. Boston: Little, Brown and Company.

Crowley, T. & Bowern, C. (2010). An Introduction to Historical Linguistics. (4thed). USA: Oxford University Press.

Eshun, F. (2004). Redundancy Rules in Kiswahili. Occasional Papers in Language and Linguistics, Vol. 2 Pg 72-85. University of Nairobi.

Guthrie, M. (1948). Classification of the Bantu Languages. London: International African Institute.

Habwe, J. & Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.

Hyman, L. M. (1975). Phonology, Theory and Analysis. New York: Holt, Rinehart and Wilson.

Massamba D.P.B (2002). Historia ya Kiswahili: 50BK hadi 1500BK. Nairobi: JKF.

Massamba, D. P. B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa. Dar es Salaam: TUKI.

Massamba, D. P. B. (2011). Maendeleo katika Nadharia ya Fonolojia. Dar es Salaam: TATAKI.

Mbaabu, I. (1996). Language Policy in East Africa: A dependency Theory Perspective. Nairobi: EARP.

Mberia, K. (2015). Misrepresentations and Omissions in Kiswahili Phonology. International Journal of Linguistics and Communication, Vol. 3, No. 1, pp. 97-111. Retrieved from: http://dx.doi.org/10.15640/ijlc.v3n1a12

Mgullu, S. R. (1999). Mtaala wa Isimu. Nairobi: Longhorn Publishers.

Mithun, M. (2013). The Dynamicity of Linguistic Systems. How Languages Work. Cambridge, UK: Cambridge University Press.

Mutiso, K. (2005). Utenzi wa Hamziyyah. Dar es Salaam: TUKI

Njogu, N., Mwihaki, A. & Buliba, A. (2006). Sarufi ya Kiswahili: Uchanganuzi na Matumizi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Ontieri, J.O. (2010). Uchanganuzi wa makosa katika insha za wanafunzi wa shule za upili: Mfano wa wilaya ya Nakuru, Kenya. Tasnifu ya uzamifu, Chuo Kikuu cha Egerton.

Polome, E.C. (1967). Swahili Language Handbook. United States of America: Massachusetts Avenue.

Trask, L. (2015). Historical Linguistics. (3rd ed). (R.M. Millar, Eds.). London & New York: Routledge.

Walt, W. (1974). Generative Phonology: Basic model. Paper presented at the Preconvention Workshop on "Linguistics and Reading: Theory into Practice,"International Reading Association” (May, 1974).

Tarehe ya Uchapishaji
15 Novemba, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Kiplimo, C., & Mwita, L. (2021). Thibitisho la Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 4(1), 43-57. https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.474