Polisemi Ambazo Zimeundwa Kutokana Na Sitiari Na Metonimu Katika Kiswahili

  • Mark Elphas Masika Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Leonard Chacha Mwita, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Sitiari, Metonimu, Semantiki Tambuzi, Polisemi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya imechunguza polisemi ambazo zimeundwa kutokana na sitiari na metonimu katika Kiswahili.  Kimsingi, polisemi ni leksimu moja yenye maana nyingi ambazo zinahusiana kwa njia moja au nyingine. Pia polisemi huundwa kwa njia zingine kwa mfano, ukopaji, mabadiliko katika matumizi ya neno, na ufasiri mpya wa homonimu. Nadharia ya semantiki tambuzi ilitumiwa katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Nadharia hii ni sehemu ya nadharia ya Isimu Tambuzi ambayo ina misingi yake katika saikolojia tambuzi .  Data ya makala haya ilikusanywa maktabani. Maneno ambayo ni polisemi na yameundwa kwa sitiari na metonimu kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2018) yalikusanywa. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Kutokana na data ya utafiti huu, imebainika kuwa kuna baadhi ya polisemi zilizojitokeza ndani ya homonimu.  Kwa mfano, tata1 na chuo1. Pia, utafiti huu umebaini kuwa polisemi nyingi huundwa kisitiari ikilinganishwa na metonimu. Makala haya inapendekeza kwamba tafiti zingine zaidi zinaweza kufanywa kuhusu namna mbinu zingine za lugha kama vile chuku, methali, nahau na tashibihi zinaweza kuchangia katika Isimu

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bynon, T. (1977). Historical Linguistics. Cambridge: Cambridge University Press.

Chacha, L.M. & Pendo, S.M. (2019). Semantiki. Nairobi: Longhorn Publishers.

Kitundu, G. J. & Malangwa, P.S. (2020). Ujenzi wa Maana katika Sitiari na Tashibiha za Kiswahili. Kioo cha lugha, 17(1). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Lakoff, G. (1987). Women, Fire and Dangerous Things. Chicago: University of Chicago Press.

Lemmens, M. (2017). ‘Cognitive Semantics’ in Routledge Handbook of Semantics. Editor Nick Riemer. London and New York: Routledge.

Mbatiah, M. (2001). Kamusi ya Fasihi. Nairobi. Standard Textbook Graphic Publishing.

Milroy, A.L. (1987). Observing and Analysing Natural Languages. Oxfort: Basil Blackwell.

TUKI, (2018). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi: Oxford University Press.

Ullmann, S. (1967). Semantics: An introduction to the Science of Meaning. Oxford: Basil Blackwell.

Vyvyan, E. & Greens, M. (2006). Cognitive Linguistics. An Introduction. Edinburgh: Edinburgh University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
22 February, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Masika, M., & Mwita, L. (2024). Polisemi Ambazo Zimeundwa Kutokana Na Sitiari Na Metonimu Katika Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 87-97. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1769

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.