Kutathmini Mafunzo Tafsiri katika Matini za Kidini: Mfano wa Njia Salama

  • Vince Arasa Nyabunga Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Miriam Osore, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Leonard Chacha Mwita, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Hali ya Maisha, Uinjilisti, Skopos
Sambaza Makala:

Ikisiri

Tafsiri imekuwa njia ya kuhamisha maarifa na ujumbe kutoka lugha moja hadi nyingine kwa muda mrefu lakini imetambuliwa kama taaluma ya kiusomi siyo miaka mingi iliyopita (Munday, 2001). Tafsiri zilizopo zimefanywa kwa kuzingatia mtazamo wa ulinganifu wa visawe vya lugha chanzi na lugha pokezi bila kuhusisha dhana ya uelewaji na ufasiri wa hadhira lengwa. Utafiti huu ulivuka mtazamo huo na kuchunguza uelewaji na ufasiri wa mafunzo tafsiri katika Njia Salama. Matini za kidini hutumiwa katika maeneo ya maabadi ili kuadilisha, kukuza mahusiano na kutangamanisha jamii. Vilevile, huwasilisha mafunzo muhimu ya kihistoria ya kidini ambayo yanafaa kueleweka na kufasirika kwa njia ya wazi. Hata hivyo, uchanganuzi wa awali wa matini tafsiri, unaonyesha kuwepo kwa matatizo ya uelewaji na ufasiri wa ujumbe wa hali ya maisha na uinjilisti. Kwa hivyo, lengo la utafiti huu ni kuthamini mafunzo hayo na kubainisha namna matatizo hayo yanavyojitokeza. Hali kadhalika, utafiti huu unakusudia kuthibitisha iwapo matatizo ya uelewaji na ufasiri wa ujumbe katika matini teule yanasababishwa na tofauti za kiisimu, kimtindo, kimuundo na kitamaduni baina ya lugha asilia na lugha pokezi. Katika kutekeleza jukumu hili, washiriki 140 walishirikishwa kutoa data ya utafiti. Data iliyopatikana ilichanganuliwa kwa njia ya kimaelezo na kitakwimu. Kwa hivyo, viongozi 42 na waumini 98 kutoka kanisa saba teule walishiriki. Washiriki waliojua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili walisailiwa na kuhojiwa. Nadharia ya skopos inayoweka mkazo kwenye matini tafsiri iliongoza utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalilenga kuchangia uelewaji na ufasiri wa ujumbe katika matini tafsiri za kidini.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Anna, Matamala. (2009). Terminological Challenges in the Translation of Science Documentaries: A Case Study, Across Languages and Cultures,11(2):255-272.

Chaula, N. (2012). Insufficiency Translation In Religious Texts Its Causes, Effects and Solutions. LAP Lambert Academic Publishing

Eugene, A. Nida. & Charles, Taber. (1969). The Theory and Practice of Translation. Laiden. Brill Publishers.

Ghazala, Hasan. (1995). Translation as problems and solutions. (10th ed.). Jeddah: Konooz Elmarefa.

George, R. Knight. (2009). A search for identity: The development of Seventh-day Adventist beliefs. Hagerstown, MD: Review and Herald.

Jeremy, Munday. (2008). Introducing Translation Studies: Theories and Applications. Leiden. Routledge.

Jeremy. Munday. (2001). Introducing Transalation Studies: Theories and Applications. Leiden. Routledge.

Joel, Donald, Heck. (2011). Evangelism. Blackwell.Blackwell Publishing Ltd.

John, Hedley, Brooke. (2011). Science and Religion Around the World, (eds). New York: Oxford University Press.

John, Touliatos & Compton, H., Norma. (1988). Research methods in human ecology/home economics. Ames, Iowa: Iowa State University Press.

Kombo K.D., & Tromp, L.,A.,D., (2006). Proposal and Thesis writing: An introduction. Nairobi. Paulines Publishers.

Kothari, C. R. (2004). Research Methodology: Methods and Techniques. 2nd Revised. New Delhi: New Age International.

Knight, R., George. (2009). A search for identity: The development of Seventh-day Adventist beliefs. Hagerstown, MD: Review and Herald.

Malangwa, S., Pendo. (2017). The Significance of Cross-Fertilization Practices in Kiswahili technical and Specilized Translation, The Journal for Studies in Humanities and Social Sciences, 6(1):154-169.

Mike, Mazzalongo. (2019). The Idea of A Christian. University Essays in Theology And Higher Education.

Lawrence, B., Venuti. (2008). The translator’s invisibility: A history of translation. USA. Routledge.

Reiss, Katharina (1990). Towards of General theory of translation action. Skopos Theory Explained. London &New York. Routledge.

Reiss, Ktharina &Vermeer, J., Hans (1984). Groundwork for a General Theory of Translation. Neimeyer. Tubergen.

Schaffner, C. (1998). Action (Theory of Translational action). In M. Baker, ed. Routledge Encyclopedia of Translation Studies. London: Routledge, pp 3-5.

Vermeer, Hans. (1989). Skopos and translation Commission. Heidelberg: Universitat.

Vermeer,J., Hans. (1978) Ein Rahmen Fur eine allgemeine translationsthe Sprachen, London &New York. 23. 95-98.

Wamitila, Kyalo, Wadi. (2004). Kamusi ya tashbihi, Vitendawili, Milio na Mishangao. Lulu za Lugha 3. Nairobi. Longhorn publishers.

Wang, Mian. (2012). International Conference on Education Technology and Management. Engineering Lecture Notes in Information Technology, Vols.16-17

Tarehe ya Uchapishaji
4 January, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Nyabunga, V., Osore, M., & Mwita, L. (2023). Kutathmini Mafunzo Tafsiri katika Matini za Kidini: Mfano wa Njia Salama. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 1-15. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1036

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.