Nomino Ambatani za Kiswahili Zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano

  • Mofart Onyoni Ayiega Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Leonard Chacha Mwita Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Mofimu, Mwambatano, Ukiukaji, Kanuni ya Kufuta Mabano, Mabadiliko, Utaratibu
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inachanganua nomino ambatani za Kiswahili zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano. Kanuni hii huonesha utaratibu wa kujenga neno kamili kwa kutumia vijenzi. Mabano katika kanuni hii hudhihirisha mipaka na hufutwa kuashiria kuwa sheria za uundaji wa maneno hazina ufikiaji wa muundo wa maneno yaliyotokana na ngazi za awali. Utafiti huu ulifanywa baada ya kubaini kuwa baadhi ya nomino ambatani za Kiswahili hukiuka Kanuni ya Kufuta Mabano hasa pale ambapo mabadiliko hutokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa. Nomino ambatani ifuatayo inadhihirisha mabadiliko yanayotokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa; [mw [enyekiti]] → [we [enyeviti]]. Katika utafiti huu tulikusanya data kutoka kwenye Kamusi Kuu ya Kiswahili (2015) ambapo nomino ambatani thelathini zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano zilitumika kama data ya msingi. Nomino hizi zilichaguliwa kwa kuzingatia sifa bainifu za ukiukaji wa Kanuni ya Kufuta Mabano (KKM). Utafiti huu uliongozwa na mhimili mmoja wa nadharia ya Mofolojia Leksia iliyoasisiwa na Kiparsky (1982) na kuendelezwa na Katamba na Stonham (2019): Kanuni ya Kufuta Mabano. Nadharia ya Mofolojia Leksia iliibuka kufidia mtazamo wa Chomsky wa Sarufi Zalishi ambao haukutambua kiwango cha mofolojia kama kiwango mahususi cha lugha. Kimsingi nadharia hii inaonesha uhusiano wa sheria zinazojenga maumbo ya kimofolojia na sheria zinazodhibiti namna maumbo hayo yanavyotamkwa. Data iliyohusiana na mada ya utafiti ilikusanywa maktabani. Baadhi ya makala ambazo zilitumika katika utafiti huu ni tasnifu za awali, makala ya mtandaoni na majarida. Utafiti huu uliongozwa na usampulishaji kimakusudi ili kufikia maneno husika ya nomino ambatani yaliyo na sifa bainifu. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya michoro, majedwali na maelezo. Utafiti huu unachangia isimu hasa kupitia kuelewa na kueleza mbinu za mwambatano katika lugha ya Kiswahili, kuwahami waundakamusi za Kiswahili na maarifa, na kukuza mofolojia ya Kiswahili.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Allen, M. R. (1978). Morphological Investigations (Unpublished Doctoral, Dissertation). University of Connecticut, Storrs, CT.

BAKITA. (2015). Kamusi Kuu ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Press.

Booij, G. (1997). Non- Derivational Phonology Meets Lexical Phonology. In I. Roca (ed.), Derivations and Constraits in Phonology. Oxford: Clarendon Press, 266-88.

Buberwa, A. (2011). Muundo wa Majina ya Mahali katika Kiswahili: Uchunguzi Kifani wa Majina ya Vituo vya Daladala Jijini Dar es Salaam. Kioo cha Lugha, 9(1)1-14.

Buberwa, A. (2017). Ruwaza za Kimofolojia za Majina ya Mahali ya Kihaya: Mtazamo wa Mofolojia Leksika. Kiswahili, 77(1).

Chomsky, N., & Halle, M. (1968). The Sound Pattern of English. New York: Harper & Row, Publishers.

Cole, J. (1995). Eliminating Cyclicity as a Source of Complexity in Phonology. In Cole, J., Green. G., & James, M. (eds.), Linguistics and Computation. Stanford: CSLI, 255-280.

Gichuru, T. M. (2010). Uchanganuzi wa Nomino Ambatani za Kiswahili: Mtazamo wa Mofolojia Leksia (Tasnifu ya Uzamili, haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Gituru, M. W. (2019). Unyambulishaji wa Vitenzi Katika Kigĩchũgũ (Tasnifu ya Uzamili, haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Chuka.

Gordian, E. (2010). The Handling of Morphological Structures in Bantu Lexicography: The Case of Orunyambo Compound Words (Shahada ya Umahiri, haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Habwe, J. & Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.

Halle, M., Harris, J. W., & Vergnaud, J. R. (1991). A Reexamination of the Stress Erasure Convention and Spanish Stress. Linguistic Inquiry, 22(1), 141-159.

Haspelmath, M., & Sims, A. D. (2013). Understanding morphology. New York: Routledge.

Inkelas, S. (1990). Prosodic Constituency in the Lexicon. New York: Garland.

Katamba, F., & Stonham, J. (2019). Morphology. New York: Palgrave.

Katikiro, E. G. (2018). Tathmini ya Maana katika Maneno Ambatani ya Kiswahili. Mulika Journal, 36(1).

Kiparsky, P. (1982). ‘From Cyclic To Lexical Phonology’ in Verder Hulst and Smith (eds). The Structure of Phological Representation. Dordrecht: Foris Publication.

Kothari, C. R. (2004) Research Methodology: Methods and Techniques (2rd ed). New Delhi: New Age International publishers.

Massamba, D. P. B. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.

Massamba, D. P. B. (2011). Maendeleo katika Nadharia ya Fonolojia. Dar es Salaam: TATAKI.

Matinde, R. S. (2012). Dafina ya Lugha na Isimu na Nadharia. Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers.

McMahon, A. (2000) Lexical Phonology and History of English. Cambridge: Cambridge University Press.

Mgullu, R. S. (1999). Mtaala wa Isimu. Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.

Milroy, A. L. (1987). Observing and Analysing Natural Languages. Oxford: Basil Blackwell Ltd.

Mohamed, S. A. (2010). Nyuso za Mwanamke. Nairobi: Longhorn Publishers Limited.

Mohanan, K. P. (1986). The Theory of Lexical Phonology. Dordrecht: Reidel.

Mustafa, S. K. (2020). Categorization of Compound Nouns in Kurdish and English. LLT Journal: A Journal on Language and Language Teaching, 23(1), 104-115.

Odden, D. (2019). Predicting Tone in Kikuria. Publications in African Languages and Linguistics, 311–326, doi: 10.1515/9783110882681-02.

Orgun, C. O., & Inkelas, S. (2002). Reconsidering Bracket Erasure. In Yearbook of Morphology 2001 (115-146).

Pesetsky, D. (1979). Russian morphology and lexical theory. Manuscript, MIT.

Poser, W. J. (1990). The Phonetics and Phonology of Tone and Intonation in Japanese. Journal of Japanese Linguistics, 12(1), 208-209.

Prince, A., & Smolensky, P. (1993). Optimality Theory: Constraint Interaction in Generative Grammar (Unpublished, Ms). Rutgers University.

Rubanza, Y. I. (1996). Mofolojia ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Siegel, D. (1974). Topics in English Morphology (Unpublished Doctoral, Dissertation). MIT, Cambridge, Massachusetts.

TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: Oxford University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
30 Oktoba, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Ayiega, M., & Mwita, L. (2021). Nomino Ambatani za Kiswahili Zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 4(1), 30-42. https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.452