Tathmini ya Matatizo ya Kiisimu na Kimtindo katika Matini Tafsiri za Kidini: Mfano Wa Njia Salama, Walioteliwa Na Vita Kuu

  • Vince Arasa Nyabunga Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Miriam Osore, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Leonard Chacha Mwita, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Tafsiri, Matatizo ya Kiisimu na Kimtindo
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yalitathmini matatizo ya kiisimu na kimtindo katika vitabu vya kidini: Njia Salama (1977), Walioteuliwa (2009) na Vita Kuu (1952), (White). Lengo la makala hii lilikuwa kutathmini matatizo ya kiisimu na kimtindo katika matini teule na kuonyesha namna yaliathiri uelewaji na ufasiri wa mafunzo tafsiri miongoni mwa waumini wa SDA. Matatizo ya kiisimu yaliyochunguzwa yalikuwa pamoja na ya kisematiki, kisintaksia, na kimofolojia. Nayo ya kimtindo yalikuwa urudiaji, uradidi, na tofauti za kipolisemia. Utafiti huu ulitumia mbinu za kimaelezo na kitakwimu katika kukusanya na kuchanganua data. Nyanjani, sampuli tarajiwa ilikuwa washiriki 140. Kwa hivyo, viongozi 42 na waumini 98 katika makanisa saba ya SDA waliteuliwa na kutoa sampuli ya utafiti. Maktabani, vitabu teule vilisomwa na vifungu vyenye matatizo ya kiisimu na kimtindo viliainishwa, kuteuliwa na kuunda data ya utafiti. Nadharia ya skopos ilitumiwa katika utafiti huu. Nadharia ya skopos, inaeleza tafsiri kama mchakato wa tafsiri unadhamiriwa kuwa na uamilifu wa zao lenyewe na jukumu hilo hubainishwa na hadhira. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa mikakati iliyotumiwa na watafsiri ilikumbwa na matatizo ya kiisimu na kimtindo yaliayoathiri uelewaji na ufasiri wa ujumbe tafsiri miongoni mwa wasomaji wa vitabu teule. Matatizo hayo yalisabishwa na tafsiri huru, sisisi, mkopo wa moja kwa moja, udondoshaji, unukuzi, uenyeshaji, ugenishaji, na ufidiaji uliofanya matini kuwa aidha finyu au pana. Kwa hivyo, utafiti huu ulichangia na kupanua taaluma ya tafsiri hasa namna ya kuchambua matatizo ya kiisimu na kimtindo katika matini tafsiri za kidini

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Amorim, N. (1990). Histoire de I’Englise. Adventiste. UAAC. Mundende, Rwanda. zake", Tasnifu ya M.A. Chuo Kikuu cha Nairobi.

Ali, S. M. (1965). Matatizo na Matumizi ya Kutafsiri Sheria Swahili Dar-es-salam University Collage.

Boase-Beier, J. (2006). Saying what someone else meant; style, relevance and translation International Journal of applied lingusticts14 (2); 276-86Cleve Don Multilingual matter LTD.

Crystal, D. (1991). A dictionary of linguistics and phonetics. 3rd edition.

Crystal D., 1987, The Cambridge Encyclopedia of Language, Cambridge

Ghazala, H. (2008). Translation as Problems and Solutions, Special Edition. Beirut: Dar Elilm lilmalayin.

Hartman, R.R.K. (1972). Dictionary of language and linguistics. London: Applied Science.

Hervey, S., & Higgins, I. (2002). Thinking Translation. London & New York: Routledge

Holz-Mänttäri, J. (1984). Translatorisches handeln: Theorie und method. Helsinki. Suomalainen Tiedeakatemia.

Leech, G. (1981). Semantics.The Study of Meaning. Second edition revised and updated. Harmondsworth: Penguin Books.

Lyons, J. (1977). Semantics. Cambridge. Cambridge University Press.

Kombo, D. K. & Tromp, D.L. (2006). Proposal and Thesis Writing an Introduction. Nairobi: Paulines Publications Africa.

Maalej, Z. (2015). On the role of Arabic in the misuse of English determination in Arab students written production. Kingdom of South Arabia. King Saul University.

Mathew, P.H (1974). Morphology. Cambridge. Cambridge University Press.

Massamba D.P.B. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. TUKI, Dar es Salaam.

Mathieu. (2003). Translation Studies. The Central Issues of Translation. Division.” Adventist World.

Murundu, A.G. (2021). East Kenya Union Conference. Nairobi. East Central Africa.

Mbwana, G. (2014) “Like a Mustard Seed: Adventism in East and Central Africa Division.” Adventist World.

Munday, J. (2016). Introducing translation studies. Theories and Applications. London. Routledge.

Munday, J. (2001). Introducing Transalation Studies: Theories and Applications. Leiden. Routledge.

Mwansoko, H.J.M. (1992). (mh) “The Style of Swahili Academic Writing,” Katika M.P. Academic Writing: The State of Art. Avon: Multilingual Matters Ltd.

Newmark, P. (1988). A Textbook of Translaton. London: Prentice Hall.

Nida, E.A. (2000). Principles of correspondence. In Laurence Venuti (ed.). The translation studies reader, 126-140. London: Routledge. (Original work published 1964).

Nida, E.A. & Taber, C.R. (1969). The Theory and Practice of Translation. Leiden. E. J. Brill,

Nord, C. (2007). Translating as a Purposeful Activity: Functionalist Approafches Explained. Manchester. St. Jerome Publishing.

Ochorokodi, J. (2021). West Kenya Union Conference.Kisumu. Kenya National Bureu of Statistics.

Reiss, K. (1990). Translation Criticism – the Potentials and Limitations. London and New York. Taylor & Francis Croup

Reiss, K. & Vermeer, J. (1984). Toward a general theory of translation action, skopos theory explained. London &New York. Niemeyer.

Schaffner, C. (1998). Action (Theory of Translational action). In M. Baker, ed. Routledge Encyclopedia of Translation Studies. London. Routledge.

Smith, C. (2022). Souls in Transition: The Religious & Spiritual Lives of Emerging Adults. Amazon. Oxford University Press.

Snell-Hornby, M. (1995). Translation studies – An integrated approach, Revised Edition. Amsterdam. John Benjamins.

TUKI (2012). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar Es salaam. Oxford University Press.

TUKI (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.

TUKI (2006). English-Swahili Dictionary.Dar es Salaam. TUKI.

TUKI (1990). Kamusi sanifu ya isimu na lugha. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. TUKI

Vermeer, H. J. (1984). Towards a general theory of translational action. Skopos theory explained. New york. St. Jerome. Publishing.

Webster (1828). American dictionary of the nglish language. NewYork. Noah Writers Ltd.

White, G.E. (2009). Walioteuliwa. USA.United Bible Society.

White, E. (1977). Njia Salama. Kisii. South Kenya Bookhouse.

White G. E. (1952). Vita Kuu. USA. United Bible Society...

Yang, W. (2010). A tentative analysis of errors in language learning use. Journal of language teaching and research. Vol 1.

Tarehe ya Uchapishaji
19 December, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Nyabunga, V., Osore, M., & Mwita, L. (2023). Tathmini ya Matatizo ya Kiisimu na Kimtindo katika Matini Tafsiri za Kidini: Mfano Wa Njia Salama, Walioteliwa Na Vita Kuu. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(2), 55-72. https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1639

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.