Mabadiliko Ya Hadithi Fupi Teule Za Kiswahili : Mkabala Wa Usasaleo

  • Paul I. Mwiti Bundi Chuo Kikuu cha Chuka
  • Onesmus Ntiba, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
  • Allan Mugambi, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
Keywords: Hadithi, Usasaleo, Teule
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inachunguza mabadiliko katika hadithi fupi kwa mkabala wa usasaleo. Inaangazia athari za usasaleo katika hadithi fupi za kimapokeo. Kwa kuwa athari ya kiusasaleo inaendelea kujitokeza katika hadithi fupi za kisasa kila kukicha, kulikuwepo na haja ya kutafiti juu ya mabadiliko haya. Katika makala hii mtafiti alichunguza vile baadhi ya hadithi zilivyoegemea uhalisia na umapokeo na jinsi waandishi wengine walivyotumia majaribio ya kimuundo, kimtindo na kimaudhui kuandika hadithi fupi za kisasa. Mtafiti alikusanya data katika diwani tatu za hadithi fupi za: Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine, Mizungu ya Manabii na Hadithi Nyingine na Homa ya Nyumbani na Hadithi Nyingine. Data iliteuliwa, kupangwa na kujadiliwa kulingana na maswali na madhumuni ya utafiti. Makala hii iliongozwa na nadharia ya umuundoleo iliyoasisiwa na Jacques Derrida na Michel Foucalt mwaka wa 1960. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa: Kubainisha mabadiliko ya kimuundo ya kiusasaleo katika hadithi fupi teule za Kiswahili, kudhihirisha mabadiliko ya kimtindo yaliyosababishwa na usasaleo katika hadithi fupi teule za Kiswahili na kufafanua mabadiliko ya kimaudhui yaliyotokana na usasaleo katika hadithi fupi teule za Kiswahili. Katika hadithi sita teule zenye mbinu za kiusasaleo waandishi walitumia mabadiliko majaribio na upya katika muundo mtindo na maudhui. Sampuli maksudi ilitumika kuteua hadithi zilizofaa utafiti huu. Madhumuni na maswali ya utafiti yalitumika kuteua kupanga na kueleza data. Matokeo ya utafiti yalitolewa kimaelezo katika sura ya nne, tano na sita na hitimisha kutolewa katika sura ya saba. Matokeo ya utafiti yanatarajiwa kufaa wanafunzi wa fasihi wa shule za upili,watafiti wa baadaye, wahakiki na wasomi wa fasihi kwa kuwapa uelewa mpana wa mabadiliko yanayotokea katika uandikaji wa hadithi fupi za Kisasa. Zaidi ya haya, utafiti huu ulichangia kuziba pengo lililopo katika utafiti juu ya mabadiliko katika hadithi fupi mkabala wa usasaleo. Maarifa yanayotokana na utafiti huu ni mchango muhimu katika fasihi andishi hasa hadithi fupi za Kiswahili.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Arege na wenzake (2012). Mwongozo wa Damu nyeusi na hadithi nyingine. Target Publications.

Amata K. (2005) . Mwongozo wa kipekee na Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi nyingine. African DF Network.

Ariel S. (1997). Ecofeminism as politics nature, Marx and the postmodernism. Zed Books.

Babu, O. (2015). Kwambizana kweli katika K. Walibora & S.A. Mohamed, (Wah. ), Homa ya nyumbani na hadithi nyingine (uk. 54 - 62). Phoenix.

Baingana, D. (2015). Njaa. ` Katika K. Walibora & S.A. Mohamed, Homa ya nyumbani na hadithi nyingine ( uk. 141- 152). Phoenix.

Douglas, T. (1993). Nineteenth century American short story. Routledge

Farhat, I. & Wenzake (2003). Postmodern approaches to the Short Story. Greenwood Publishing Group.

Giddens ,E. & Antony, K.(1990). The consequencies of modernity. Standford University.

Habwe J. (2010). Mizungu ya manabii na hadithi nyingine. Phoenix.

Iribemwangi (2011). Alidhani Kapata na Hadithi Nyingine . EAEP.

Kwambai, M. (2015). Maudhui ya kihalisia katika riwaya dhahania za Katama Mkangi. Tasnifu ya uzamili.(Isiyochapishwa), Chuo Kikuu cha Nairobi.

Leger, L. (1990). Creating unforgettable characters. Doubley and Company Inc.

Maitaria, J. (2012). Mwongozo wa Damu nyeusi na hadithi nyingine. Longhorn.

March, P.P. ( 2009). The short story an introduction. Edinburgh University Press.

May,C. (1994). The new short story theories . Ohio University Press.

Mbogo, E. (2010). Mizungu ya manabii. Katika J. Habwe (mh.), Mizungu ya manabii na hadithi nyingine ( uk. 32 - 60). Phoenix.

Mohamed , S.A. (2015). Zawadi ya mume wangu. Katika K.Walibora & S.A. Mohamed ( Wah.) . Homa ya nyumbani na hadithi nyingine ( uk. 10-21). Phoenix.

Myszor, F. (2001). The modern short story. Cambridge Universty Press.

Walibora , K. (2007). Atanasi na kismati. Katika K. Walibora & S.A. Mohamed , Kiti cha moyoni na hadithi nyingine (uk. 8-17). Oxford.

Nandwa, R. (2010). Jua litawaka. Katika J. Habwe (mh.), Mizungu ya manabii na hadithi nyingine ( Uk. 190 - 203). Focus Publishers.

Njogu, K. & Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa fasihi: nadharia na mbinu. Jomo Kenyatta Foundation.

Njogu, K. & Wafula, R. (2007). Nadharia za uhakiki wa fasihi. Jomo Kenyatta Foundation.

Sacido, J. ( 2012). Modernism and postmodernism and the short story. Longman Green.

Timammy, R. (2010). Kikojozi. Katika J. Habwe (mh.), Mizungu ya Manabii na hadithi nyingine ( uk. 180 - 188). Phoenix.

Timammy, R. (2004). Uteuzi wa moyoni. Katika Wamitila, K.W. (mh.), Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi nyingine ( uk. 7-19). Focus Publishers.

Wamitila, K. (2003). Kamusi ya fasihi ; istilahi na nadharia. Focus Publications.

Wamitila, K.W. (2004). Kachukua Hatua Nyignine . Katika K.W. Wamitila Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi nyingine ( uk. 38 - 49). Focus Publishers.

Williams, R. (1995). The postmodern novel in Latin America. Politics, culture and crisis of truth. St. Martin’s .

Tarehe ya Uchapishaji
12 October, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Bundi, P. I., Ntiba, O., & Mugambi, A. (2022). Mabadiliko Ya Hadithi Fupi Teule Za Kiswahili : Mkabala Wa Usasaleo. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 1-14. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.882

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.