Ubadili Maana katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Kifonolojia na Kimofolojia

  • Kimathi Mwembu Chuo Kikuu cha Tharaka
  • Allan Mugambi, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
  • Timothy Kinoti M’Ngaruthi, PhD Chuo Kikuu cha Embu
Keywords: Kîîtharaka, Leksia, Ubadili Maana, Leksika-Pragmantiki
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanalenga kubainisha jinsi ubadili katika vitamkwa na mofu unavyoathiri maana ya leksia katika Kîîtharaka. Maana katika leksia hutegemea kipengele cha kiisimu na vile vile kile cha kijamii ili ieleweke vilivyo. Katika hali hii, mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia, pamoja na kileksia yanayoathiri maana yameangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Makala haya yanabainisha ubadili wa kifonolojia pamoja na kimofolojia ambao huchangia katika kuibuka kwa maana fulani katika leksia za Kîîtharaka. Makala haya yanabainisha kwamba maana katika leksia za Kîîtharaka hutegemea kwa njia moja au nyingine mabadiliko yanayohusisha usilimisho, kuimarika na kudhoofika kwa fonimu, uchopekaji, uyeyushaji, hapololojia, kanuni ya Dahl na Ganda. Aidha, ubadili unaoathiri maumbo ya mofu huchangia pakubwa kutokea kwa maana katika leksia. Mofu za ngeli, ukanusho na uambishaji ni miongoni mwa zile ambazo zimebainika kuathiriwa na ubadili, ambao huzua maana fulani. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na misingi yake katika kiwango cha fonimu na mofimu zinazotumika kuunda neno. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha wa leksia.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bauer, L. (1983). English Word Formation. Cambridge: Cambridge University Press.

Bennett, R.P. (1977). Dahl’s Law andtheThagicu. InAfrican LanguageStudies, Vol. VII, pp. 127-159.

Bennett, R.P. (1985). DhaagicwLifeStages: A StudyinParadigmaticReconstruction. In HistoryinAfrica, Vol 12 pp. 11-28.

Blutner, R. (1990). Lexical Pragmatics in Journal of Semantics; Vol. 15 (2) Pp. 115-162 katika tovuti https:/www.blutner.de/iex.pragpdf, accessedon 23/9/2020.

Crowley, T.,&Bowern, C. (2010). An Introduction to Historical Linguistics. London: Oxford.

Gichuru, T. M. (2020). Mabadiliko ya Maana za Leksia za Kiswahili: Mtazamo Linganishi wa Kale na Kisasa. Tasnifu ya Uzamifu (Haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Guthrie, M. (1970). The Classification of Bantu Languages, London: International African Institute.

Katamba, F. (1993). An Introduction to Phonology. London: Longman.

Massamba, D.P. (2011). Maendeleo katika Nadharia ya Fonolojia. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mberia, K. (1993). Kîîtharaka Segmental Morphophonology with special reference to the Noun and Verb. (Unpublished) PhD. Thesis.University of Nairobi.

McMahon, A.M.S. (1994). Understanding Language Change. Cambridge: Cambridge University Press.

Mgullu, R. (1999). Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.

Mukuthuria, M. (2004). Kuathiriana kwa Kiswahili na Lahaja ya Kitigania: Uchanganuzi wa Taathira katika Muktadha wa Shule za Msingi na Upili katika Tigania-Kenya. Tasnifu ya Uzamili (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Egerton.

Mwembu, K.N. (2012). Uasilishaji wa Maneno ya Kigeni katika Lahaja ya Kîîtharaka, Kenya. Tasnifu ya uzamili (Haijachapishwa), Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuka.

Peng, L. (2007). Geminationand Anti-Gemination: Meinhof’s Law inLuGandaand Kikuyu.

Richards, J.C. na Wenzake (1985). Dictionary of Applied Linguistics. Harlow: Longman.

TUKI, (1990).Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam: Educational Publishers and Distributers Ltd.

Uffmann, C. (2013). Set the Controls for the Heart of the Alteration: Dahl’s Law in Kîîtharaka. Nordlyd Vol 40.1 pp 323-337.

Tarehe ya Uchapishaji
28 September, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Mwembu, K., Mugambi, A., & M’Ngaruthi, T. (2022). Ubadili Maana katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Kifonolojia na Kimofolojia. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 353-362. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.860