Dhima ya Toponemia kama Utambulisho wa Jamii: mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara Nchini Kenya

  • David Micheni Mutegi, PhD Chuo Kikuu cha Tharaka
  • Allan Mugambi, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
  • Timothy Kinoti M’Ngaruthi, PhD Chuo Kikuu cha Embu
Keywords: Anthroponemia, Dhima, Onomastiki, Toponemia na Uchanganuzi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Utafiti huu ulikuwa wa kionomastiki uliolenga kubainisha dhima ya toponemia za shule za msingi kama utambulisho wa jamii. Utafiti ulifanyika katika eneo la Mwimbi na Muthambi Jimboni dogo la Maara. Nadharia ya Ujinaishaji pamoja na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi na Matini ndizo zilizotumiwa kuongoza utafiti huu. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano na hojaji. Mahojiano yalimwezesha mtafiti kupata data ya kutosha na halisi moja kwa moja kutoka kwa wahojiwa. Hojaji ilimwezesha mtafiti kukusanya data kwa urahisi katika maeneo mengi na kutoka kwa sampuli kubwa. Walengwa katika utafiti huu walikuwa wakaazi wa Mwimbi na Muthambi. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kuhusisha machifu 5 wa kata 5 za Mwimbi na Muthambi na manaibu wa chifu 25 kutoka kata ndogo 25 za eneo hili. Watawala hao walichaguliwa kwa sababu wao ni wenyeji wa eneo hili walio na habari kuhusu maeneo yao ya utawala kwa hivyo wangetoa habari kamilifu kuhusu maswali ya utafiti. Sampuli nyingine ya Wazee 20 wenye umri wa miaka sabini na zaidi walichaguliwa kimakusudi kwa kutumia mbinu ya kimtandao ili kutoa habari kuhusu dhima ya toponemia za shule za msingi katika eneo la Mwimbi na Muthambi. Sampuli ya wazee ilipatikana kwa urahisi kwa sababu ndio wanaopata pesa za wazee na walijulikana katika vijiji vyao. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo kulingana na madhumuni na swali la utafiti. Matokeo ya utafiti huu ni marejeleo muhimu kwa watafiti wengine watakaoshughulikia vipengele vya onomastiki katika lahaja ya Kimwimbi na Kimuthambi. Aidha, utafiti huu ulibainisha kuwa toponemia huwa na dhima mbalimbali katika jamii

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abrams, D. na Hog, M. (1990). An introduction to the social identity Approach, University of Melbourne, Austrilia.

Barnes, H. (2005). ‘Hidasta personal names’: An Interpretation Plains Anthropologistics. Journal of anthropological Research /25 90311-31281.

Best, J, &Khan, J. (1998). Research in Education, New Jersey, Eaglewood Cliffs.

Buberwa, A. (2011). Viambishi ngeli katika nomino za pekee: mifano katika majina ya Kihaya, Kiswahili, Juz. 74. Kur. 41 – 48

Crystal, D. (1987). The Encyclopedia of Language. Cambridge: CUP.

Giles, H. (2001). “Speech accommodation” in R. Methrie (ed) Concise Encyclopedia of Socialinguistics 193-197, Elsevier.

Helander, K. (1999). Place names in multilingual areas in Norway. Journal of anthropological Research /25 90311-312

Habwe, J., &Karanja, P. (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.

Kihore, P., & Wenzake, (2004). Sarufi maumbo ya Kiswahili sanifu: Sekondari na Vyuo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: TUKI.

Kirui, R. (2016). A morphosemantic study of Kipsigis toponyms. (Unpublished) Master thesis.Kenyatta University.

Kothari, C. (2004). Research Methodology: Methods and Techniques, New Delhi: New Age International (P) Ltd.

Kothari, C. (2009). Research Methodology: Methods and Techniques, New Delhi: New Age International (P) Ltd. 189.

Koigi, K. (2008). Lugha kama Kitambulisho. Jarida la Kiswahili la Isimu na Fasihi. Juz na. 4:23, TUKI, Dar es Salaam.

Mbaabu, I. (1996). Language Policy in East Africa, Educational Researchand Publication. Nairobi: Publisher.

Masanja, N. (2019). Uchunguzi wa kisemantiki wa majina ya asili katika koo za Ginantuzu.Tasnifu ya uzamifu, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Msanjila, P., & Wenzake, (2011). Isimujamii, Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam : TUKI.

Majapelo, P. (2009). Namna ngeli zinavyosaidia kuunda majina ya watu (unpublished) M.A Dissertation. University of Dar-es-salaam.

Mugenda, M., &Mugenda, G. (2008). Research Methods: qualitative and quantitative approach.Nairobi Acts press.

Mukuthuria, M. (2018). “Uchanganuzi wa Lugha za Kibantu za Kenya Katika Ngazi ya Mofolojia: Mtazamo wa Sarufi Zalishi Geuza Umbo.” Katika: Islamic University Journal, Vol. 1 No.2, Mbale – Uganda (uk. 103 – 108).

Musymi, D. (2011). Maana za majina ya Watu katika jamii ya Wakamba, Tasnifu ya shahada Ya uzamili, Kenyatta University Bantu Names. Kiswahili (61):28-49. 190 New Age International Publishers. Ltd

Mwenamseke, F. (2011). Uainishaji wa ngeli katika lugha ya Kibena. Tasnifu ya Uzamili (isiyochapishwa) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Raybum, A. (2010). Place names. The Canadian Encyclopedia- Historical- Dominion

Reinsted, A. (1994). Place names of New Zealand Wellington A. H .& A.W Reed.

Rye, J. (2006). A popular Guide to Norfolk Place names. Guist Bottom: Larks Press.

Rugemalira, J. (2009). A Grammar of Runyambo, Dar es Salaam: Language of Tanzania Project, University of Dar es salaam.

Sigh, K. (2007), Qualitative Social Reseach Methods, Indian: SAGE Publication.

Stuart, M. na wenzake, (2001). Different types of dictionaries Grin Verlang.

Thorsten, A. (1994). Place names worthy of caring for. Paper read at the symposium place name culture organized by the National Heritage board. Stockholm.

Wodak, R. (2001). Methods of critical Discourse analysis,London Sage Publisher.

Tarehe ya Uchapishaji
21 November, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Mutegi, D., Mugambi, A., & M’Ngaruthi, T. (2023). Dhima ya Toponemia kama Utambulisho wa Jamii: mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara Nchini Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(2), 1-14. https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1581