Wahusika na Motifu ya Siri katika Nathari Teule za Fasihi za Kiswahili

  • Beatrice Nyambura Njeru Chuo Kikuu cha Chuka
  • John Kobia, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
  • Allan Mugambi, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
Keywords: Mwingilianomatini, Wahusika, Motifu ya Siri, Nathari, Fasihi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Wahusika ni viumbe muhimu katika ujenzi wa kazi ya fasihi. Mhusika ni mtendaji katika kazi ya kifasihi na huwa ni kielelezo cha viumbe wanaopatikana ulimwenguni ingawa si lazima sifa zote za mhusika zifungamane na za binadamu. Ni picha ambayo huchorwa na fasihi na ni kiini cha vitu vipya, dhamira na mada katika fasihi.  Kwa hivyo, wahusika si watu halisi bali ni watu wa kubuni. Mwandishi huchora viumbe anaowatwika majukumu ya kutenda na kusema kama binadamu na kupitia kwao huwasilisha dhamira yake. Dhamira hii hukuzwa na kuwepo kwa masuala makuu ambayo huwasilishwa kwa hadhira lengwa na kufanikisha lengo kuu la utunzi wa kazi ya fasihi. Makala haya yanalenga kuchunguza namna ambavyo wahusika huingiliana kutoka kwa matini moja hadi nyingine katika nathari teule za fasihi ya Kiswahili. Mwingilianomatini hubainisha kuwa matini moja inaweza kuhusiana na matini nyingine katika viwango mbalimbali kama vile usawiri wa wahusika, usawiri wa mandhari, maudhui na mtindo wa uandishi. Sampuli maksudi ilitumika kuteua vitabu saba kwa msingi kuwa vina dhana ya siri katika uteuzi wa mada. Vitabu hivi ambavyo ni Nataka Iwe Siri, Sitaki Iwe Siri, Siri Ya Baba Yangu Kitabu 1, Siri Ya Baba Yangu 2, Siri Sirini 1, Siri Sirini 2 na Siri Sirini 3 vimedhihirisha kuwa kuna siri ambazo zimejengwa na wahusika katika bunilizi teule na kufanikisha motifu ya siri. Uchanganuzi na uwasilishwaji wa data itakayopatikana kutokana na usomaji wa kazi teule utakuwa wa kimaelezo. Makala haya yatawafaa wahakiki kwa kuwapa mwanga wa namna ya kuhakiki kazi zinazohusiana na siri na kuchunguza namna wahusika wanavyoweza kuingiliana kwa namna tofauti na kufanikisha ujenzi wa motifu ya siri. Aidha walimu na wanafunzi wa viwango vyote watafaidika kwa sababu wataelewa kazi teule zaidi. Waandishi nao watafaidika kutokana na makala haya kwa sababu watayatumia kama kifaa cha kutunga kazi za baadaye za kiwango cha juu zaidi kuhusiana na motifu ya siri. Vilevile makala haya yatatoa mchango mkubwa katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili kwa kuwa yataongeza maarifa mapya kuhusu  namna wahusika wanaweza kuingiliana na kukuza kazi za kibunilizi zilizo na motifu mbalimbali.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abrams, M. H. A. (1981). Glossary of Literary Terms. New York: Holt, Rinehart and Winston.

Allen, G. (2000). Intertextuality. New York: Routledge.

Barry, P. (1995). Beginning Theory: An Introduction to Literary and Cultural Theory. New York.Manchester University Press.

Bosire, T. (2016). Mwingilianomatini Kati ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Mstahiki Meya. Shahada ya Uzamili katika Idara ya Kiswahili. Chuo Kikuu cha Nairobi.

Chimerah, R. (2013). Siri Sirini 1: Mshairi na Mfungwa. Nairobi: Longhorn Publishers.

Chimerah, R. (2013). Siri Sirini 2: Mpiga Mbizi Kilindini. Nairobi Publishers.

Chimerah, R. (2014). Siri Sirini 3: Mtihani wa Mwanamke. Nairobi: Longhorn Publishers.

Coyle, M. na Wengine. (1990). Encyclopedia of Literature and Criticism. London: Macmillan.

Eagleton, T. (1983). Literary Theory: An Introduction. Oxford: Basil Blackwell.

Eliot, T. S. (2015). Tradition and Individual Talent. The Sacred Wood. Retrieved August 10, 2015 from http://www.bartleby.com/200/sw4.html

Friedman, N. (1955). Forms of Plot. Journal of General Education. Vol. 8. Pgs 241-253.

Fyre, N. (1957). Anatomy of Criticism. Princeton University Press.

Garci, B. B. (2016). Around The Function of Characters in Literary Fiction. Shahada ya Uzamili, (Haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Granada.

Have, J. Na Omboga, J. (2019). Kamusi ya Isimu na Fasihi. Jomo Kenyatta Foundation.

Karama, M., Mutiso, K. na Chimerah, R. (2018). Ushairi wa Kisufi Katika Tendi za Kale za Kiswahili: Mfano Wa Utendi wa Siri La Asrari. Katika Mara Research Journal of Kiswahili Vol. 3, No. 1.The African Premier Research Publishing Hub.

Kehinde, A. (2003). Intertextuality and the Contemporary African Novel. Nordic Journal of African Studies 12(3) Pg. 372-386.

Kirumbi, P. (1971). Nataka Iwe Siri. Tanzania: Printpak Publishers.

Kristeva, J. (1969). Intertextuality. Literary Theory and Criticism. Edinburgh University Press.

Leitch, V. B. (1983). Deconstructive Criticism: An Advanced Introduction. New York: Columbia University Press.

Madumulla, J. S. (2009). Riwaya ya Kiswahili: Nadharia, Historia na Misingi Ya Uchambuzi. Nairobi: Phoenix Publishers.

Matundura, B. (2008). Sitaki Iwe Siri. Nairobi: Longhorn Publishers.

Matundura, B. (2018). Motifu ya ‘Siri’ Katika Fasihi ya Kiswahili na Jinsi Inavyoendeleza Dhamira ya Mwandishi. Taifa Leo. Novemba 21.

Matundura, B. na Maina, R. (2014). Secret of Swahili Literature is out. The Standard. December 21.

Made, J. S. na Wengine. (2018). Kamusi ya Karne ya 21. Nairobi: Longhorn Publishers.

Mohammed, S. A. (1995). Kunga za Nathari ya Kiswahili, Riwaya, Tamthilia na Hadithi Fupi. Nairobi: East Africa Educational Publishers.

Mulokozi, M. M. (1996). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Dar es Salaam.

Mutembei, A. (2016). Epistolary role in East African literary works on HIV/AIDS. Journal of University of Namibia Language Centre Volume 1, (1). University of Dar es Salaam, Tanzania.Kur 104-109.

Mutuku, Y. (2017). Siri ya Baba Yangu: Kitabu cha Kwanza. Nairobi: Queenex Publishers Ltd.

Mutuku, Y. (2017). Siri ya Baba Yangu: Kitabu cha Pili. Nairobi: Queenex Publishers Ltd.

Ombito, E. K. (2014). Uhakiki wa Kitabu cha; Siri Sirini 1: Mshairi na Mfungwa. Katika Miaka Hamsini ya Kiswahili Nchini Kenya. Nairobi: Twaweza Communications. Kur.261-262.

Plett, H. F. (1991). Intertextualities, Intertextuality. Walter de Gruyter and Co. Berlin and New York.

Ponera, A. S. (2014). Utangulizi wa Nadharia ya Fasihi Linganishi. Karljamer Print Technologies.

Saraswati, K. P. (2019). Analysis of Characters and Characterization in the Compilation of Malay Poetry “Mirror. Shahada ya Uzamili (Haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Negeri Semarang.

Scheppele, L. K. (1988). Legal Secrets; Equality and Efficiency in the Common Law. University of Chicago. Chicago and London.

Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Phoenix Publishers.

Tarehe ya Uchapishaji
29 September, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Njeru, B., Kobia, J., & Mugambi, A. (2022). Wahusika na Motifu ya Siri katika Nathari Teule za Fasihi za Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 234-249. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.782