Utathmini wa Maudhui katika Nyimbo Teule za Newton Kariuki

  • John Muriuki Ireri Chuo Kikuu cha Mount Kenya
  • Onesmus Ntiba, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
Keywords: Nyimbo, Maudhui, Mtindo, Newton Kariuki, Umtindo na Udenguzi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inahusu utathmini wa maudhui katika nyimbo teule za msanii Newton Kariuki. Nyimbo ni moja wapo ya njia zinazotumiwa na wasanii kuwaslisha ujumbe unaowahusu jamii. Utafiti huu ulitumia nadharia ya mseto, yaani nadharia ya umtindo ile ya udenguzi. Nadharia ya umtindo inasisitiza kuwa lugha ina sehemu mbili zinazodhihirika katika usemaji; lugha ni dhahiri na dhahania. Aidha, nadharia ya udenguzi huashiria mgogoro usiosuluhika uliopa baina ya usemi balagha na mawazo kwamba kuna pengo kati ya inachokusudia kusema kazi ya fasihi na inacholazimika au kuelekezwa kusema. Hivyo kuna mvuto katika ya usemi na mantiki. Utafiti ulichukua muundo wa kimaelezo. Mtafiti aliteua kimakusudi jumla ya nyimbo kumi zilizoimbwa na mwanamuziki Newton Kariuki, yaani tano za Kiswahili na tano za Kimbeere. Kutokana na jumla ya nyimbo hamsini alizokuwa ameimba kufikia muda wa kufanya utafiti. Data ilikusanywa kwa kuzingatia kigezo cha yaliyomo. Waaidha, data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Matokeo ya utafiti ni kuwa sampuli iliyoteuliwa ilisheheni maudhui ya mapenzi, ndoa na familia, migogoro katika ndoa, kuporomoka kwa maadili, uongozi na siasa, umaskini, uhalifu, mawaidha, UKIMWI na dini na imani. Maudhui haya yaliakisi maisha katika ulimwengu wa kiuhalisia. Umuhimu wa makala hii ni kuwa matokeo haya yanadhihirisha kuwa mwimbaji yeyote halengi tu kuburudisha bali kuelimisha. Hivyo makala hii inapendekeza utafiti wa baadae ufanywe kwa kuzingatia mahusiano ya uwezo wa kiuana katika sampuli teule

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Crystal, D. & Davy, D. (1969). Investigating English Styles. London. Longman.

Davy, D. (1969). Investigating English Style; Indiana University Press, Bloomington, Indiana.

Derrida, J. (1973). Speech and Phenomena, and other Essays on Husserls Theory of Signs, Evanson: North-Western University Press.

Mbogo, N. (2008). Mabadiliko ya Maudhui Kiwakati katika Nyimbo za Harusi za Jamii ya Waembu (Unpublished Thesis), Kenyatta.

Mugenda, O. M., & Mugenda, G. A. (1999. Research Methods: Quantitativeand Qualitative Approaches. Nairobi; Acts Press.

Mutwiri, G. (2005). Mitazamo ya Utendakazi wa nyiso katika Jamii ya Watigania. Tasnifu ya Uzamili: Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Mweteri, I. (2021). Urejeleano katika Utunzi wa Kamusi za Kiswahili: Uchanganuzi Linganishi wa Kamusi za Lugha Moja. Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta (Haijachapishwa).

Njogu, K. & Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa fasihi, nadharia na mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Saussure, F., (1966). Course in general linguistics. In Bally, C. & Sechehaye, A. New York: McGraw-Hill.

Saussure, F. (1983). Course in General Linguistics (Trans Roy Harris) London. Duckworth.

Simiyu, F. (2007). Maendeleo na Mabadiliko katika Nyiso za Wabukusu: Lugha wa Maudhui (Unpublished Thesis), Kenyatta University.

TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu 4th Edition, Oxford.

Wafula, R. & Njogu, K. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Wamitilia, K. (2004). Kichocheo cha Fasihi Simulizi. Nairobi: Focus Publications Ltd.

Tarehe ya Uchapishaji
9 September, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Ireri, J., & Ntiba, O. (2023). Utathmini wa Maudhui katika Nyimbo Teule za Newton Kariuki. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 319-338. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1419