Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda

  • Willy Wanyenya, PhD Makerere University Business School
Keywords: Maudhui, Tohara, Matukio, Miti Shamba, Khukhubuluula
Sambaza Makala:

Ikisiri

Katika makala hii, mwandishi anaeleza maudhui mbalimbali yanayopatikana katika nyimbo za tohara za Wamasaaba nchini Uganda. Alifanya hivyo kwa kurejelea angalau mfano mmoja wa nyimbo hizo kwa kila maudhui. Mwandishi amepanga maudhui hayo kulingana na utaratibu wa utendaji wa matukio ya tohara. Kutokana na jambo hili, mwandishi ameangalia matukio mbalimbali katika utekelezaji wa tohara kwa sababu nyimbo hizo huambatana na matukio fulani. Kwa kufanya hivyo, mwandishi ametaja tukio na kutoa mfano wa wimbo unaoimbwa. Baada ya kutoa mfano wa wimbo, anauchanganua na kubainisha maudhui mbalimbali yaliyomo. Mwandishi anafanya hivyo hatua kwa hatua mpaka mwisho. Dhamira ya utafiti ni kueleza jinsi Wamasaaba walivyobobea katika utanzu huu wa sanaa. Hali kadhalika, madhumuni ya utafiti huu ni kueleza namna nyimbo za kiutamaduni zilivyo muhimu katika maisha ya binadamu, kufafanua athari za nyimbo za tohara kisaikolojia na kuonyesha nguvu za mawasiliano za nyimbo za kiutamaduni. Mkabala wa utafiti huu ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani na kukusanya nyimbo. Katika kazi yake, mtafiti alitumia mbinu ya uchunguzi shiriki. Kwa kutumia mbinu hii, mtafiti alifuatilia makundi ya watendaji na kushuhudia jinsi matukio ya tohara yanavyotekelezwa. Kulingana na aina ya utafiti, mtafiti hakuuliza watu maswali. Mtafiti alitumia kinasa sauti kurekodi nyimbo. Baada ya mchakato huo kukamilika, mtafiti alizichanganua nyimbo ambazo alizikusanya halafu akawasilisha matokeo ya utafiti wake. Nyimbo zilizokusanywa zilijumlisha zile za kupokea wageni, zile zinazoonyesha huzuni kwa mhusika, zile zinazodhihirisha furaha kwa mhusika, zile za kuonya mhusika nk. Mtafiti alianza uchanganuzi wa nyimbo kwa kuziandika kwenye karatasi. Baada ya kufanya hivyo, alizipanga kulingana na madhumuni ya utafiti. Alipomaliza kufanya hivyo, mtafiti alieleza maudhui mbalimbali kama yalivyojitokeza katika kila wimbo.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Beier, U. (1967). Introduction to African literature: an anthology of critical writing from Black Orpheus. Evanston IL: Northwestern University Press.

Chesaina, C. (1991). Oral Literature Of the Kalenjin. Nairobi: East Africa Educational Publishers Ltd.

Kichamu, S. & Odaga, A. (1982). Oral Literature, A School Certificate Course. Nairobi: Heinemann Educational Books (E.A) Ltd.

Mlacha, S. A. K. (1995). Lugha, Utamaduni na Fasihi Simulizi. Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dares Salaam.

Nangoli, M. (2001). No more lies about Africa: here's the truth from an African. Brooklyn, NY: A & B Publishers Group.

Njogu, K; Momanyi, C. & Mathooko, M. (2006). Fasihi Simulizi ya Kiswahili. Nairobi: Twaweza Communications.

Nketia, J. K. (1955). Funeral dirges of the Akan people (Vol. 2). Negro Universities Press.

Nkwera, F.F.V. (1989). Tamrini za Fasihi Simulizi. Dar es Salaam: Kitabu Commercial Printing Co. Ltd.

Senkoro, F. E. M. K. (1987). Fasihi na Jamii. Dar es Salaam: Press and Publicity Centre.

Vendler, Z. (1980). Telling the facts. In Speech act theory and pragmatics (pp. 273-290). Springer, Dordrecht.

Tarehe ya Uchapishaji
13 August, 2020
Jinsi ya Kunukuu
Wanyenya, W. (2020). Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 2(2), 84-99. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.194

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.