Mnyambuliko wa Vitenzi Katika Lugha za Kiafrika: Mfano katika Lugha ya Kimasaaba Nchini Uganda

  • Willy Wanyenya, PhD Makerere University Business School
Sambaza Makala:

Ikisiri

Katika makala hii, mtafiti anaeleza jinsi vitenzi vya lugha za Kiafrika vinavyonyambuliwa na kuleta maana tofauti tofauti. Anafanya hivyo kwa kurejelea Kimasaaba ambayo ni lugha inayozungumzwa na Wamasaaba nchini Uganda. Unyambuaji wa vitenzi ni jambo la kawaida na huwa linatekelezwa katika lugha mbalimbali. Hivyo basi, katika makala hii, mtafiti anaeleza mnyambuliko ya vitenzi katika lugha ya Kimasaaba. Anawasilisha mkusanyiko wa vitenzi na kueleza jinsi vinavyonyambuliwa na wazungumzaji. Aidha, mtafiti anaeleza namna vitenzi hivyo vinatumiwa katika sentensi. Mtafiti anafanya hivi kwa sababu lugha nyingi za Kiafrika hazijatafitiwa na kuna mambo mengi sana mazuri ambayo hayajulikani kwa ulimwengu. Katika kazi hii, mtafiti anaandika vitenzi mbalimbali katika lugha asili halafu anavitafsiri katika Kiswahili. Kwenye kazi hii, madhumuni ya utafiti ni kudhihirisha utaratibu wa kunyambua vitenzi katika Kimasaaba. Pili, kueleza maana tofauti zinazotokana na mnyambuliko ya vitenzi. Tatu, kuonyesha kuwa Kimasaaba ni lugha inayoendelea kukua kama lugha zingine za Kiafrika. Mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani ambako aliendeleza mahojiano na wahojiwa wake. Majibu ya wahojiwa yalijumlisha data ambazo zilihitajika na mtafiti. Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa Kimasaaba kama lugha nyingine za Kiafrika ina vitenzi vingi sana vinavyonyambuliwa na kwendeleza mazungumzo ya wazungumzaji.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Baraka, Y. (2018). Unyambulishaji wa Vitenzi vya Lugha ya Kinyakyusakatika Mkoa wa Mbeya-Kyela. Morogoro, TZ: Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino.

Katamba, F. (2003). Bantu nominal morphology. The Bantu languages, 103, 120.

Khamis, A. M. (2008). Maendeleo ya Uhusika, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Kihore, Y. M., Massamba, D. P. B., & Msanjila, Y. P. (2003). Sarufi maumbo ya Kiswahili sanifu (SAMAKISA): Sekondari na vyuo. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Matei, A. K. (2008). Darubini ya sarufi : ufafanuzi kamili wa sarufi ya Kiswahili : maswali na mazoezi. Nairobi: Phoenix Publishers.

Mbwillow, S. N. (2017). Uambikaji kama Dhana Kuu: Tofauti ya Uambikaji na Unyambulishaji. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mhadhara wa 8 katika kitabu kilichotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mwaka wa (2008). Uambishaji na Mnyambuliko wa Maneno, Taasisi ya Elimu, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dar es Salaam.

Niyirora, E. & Ndayambaje, L. (2012). Kiswahili Sanifu kwa Shule za Sekondari. Kitabu cha Mwalimu, Kidato cha Tano. Tanprints.

TUKI. (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi, KE: OxfordUniversityPress.

Wahiga, G. (1999). Sarufi Fafanuzi ya Kiswahili. Nairobi, KE: Longhorn Publishers.

Tarehe ya Uchapishaji
15 Julai, 2020
Jinsi ya Kunukuu
Wanyenya, W. (2020). Mnyambuliko wa Vitenzi Katika Lugha za Kiafrika: Mfano katika Lugha ya Kimasaaba Nchini Uganda. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 2(2), 44-53. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.184

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.