Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda

  • Willy Wanyenya, PhD Makerere University Business School
Sambaza Makala:

Ikisiri

Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Kwa kurejelea jamii hii, mtafiti alieleza namna wazazi wanavyotumia lugha kulea watoto wao.  Alifanya hivyo kwa kunukuu baadhi ya semi ambazo zinasemekana zinatumiwa na wazazi katika shughuli ya kulea watoto. Ni kweli kwamba lugha yoyote ile hufanya kazi nyingi sana kama vile kutumbuiza watu, kuficha siri, kuseng’enya watu, kuibia watu, kutongozana, kushawishi, kugombana, kujitetea, kufundisha, nakadhalika. Hii ni kwa sababu bila kutumia lugha, mtu hawezi akaimba, akagombana, akaiba kwa kudang’anya, akafundisha, akaseng’enya, akatongoza, n.k. Hata hivyo, katika makala haya, mtafiti alijikita kwenye malezi ya watoto. Katika kazi hii, mtafiti alizingatia semi mbalimbali ambazo Wamasaaba huzitumia kwa ajili ya kuwaelekeza watoto wao ili wasije wakatenda maovu ukubwani. Katika jamii mbalimbali, watu hutumia lugha kutekeleza jambo hili. Jamii hasa zile za jadi zilitumia lugha kuwaelekeza watoto wao. Kuna namna ambavyo walisuka lugha kisanaa kwa lengo la kufunza watoto wao. Hii ni kwa sababu hawakuwa na madarasa maalumu mwa kufunzia watoto wao kama ilivyo sasa. Katika jamii hizo, shule zenyewe hazikuwepo. Kwa hiyo, lugha ndiyo ilikuwa chombo maalumu cha kufunzia watoto. Matumizi ya lugha yalidhamiria kukuza watoto wenye tabia nzuri. Hii ni kwa sababu watoto wenye tabia mbaya waliletea wazazi wao aibu. Hivyo basi, katika kazi hii, mtafiti alijikita katika matumizi ya lugha na kueleza jinsi Wamasaaba wanavyotumia semi mbalimbali kuelekeza watoto wao kitabia.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Dale, P. S., Tosto, M. G., Hayiou-Thomas, M. E., & Plomin, R. (2015). Why does parental language input style predict child language development? A twin study of gene–environment correlation. Journal of communication disorders, 57, 106-117.

Hoff, E. (2006). How social contexts support and shape language development. Developmental review, 26(1), 55-88.

Johnston, J. (2010). Factors that influence language development. Language Development and Literacy, 11-15.

Maccoby, E. E. (2000). Parenting and its effects on children: On reading and misreading behavior genetics. Annual review of psychology, 51(1), 1-27.

Maschinot, B. (2008). The Changing Face of the United States The Influence of Culture on Early Child Development. Washington, DC; Zero to Three.

Nuttall, E. (2018, Dec 8). How Culture Affect the Language Development of a Child? Retrieved from https://www.hellomotherhood.com/how-does-culture-affect-the-language-development-of-a-child-9653552.html.

Oyogho O. V. (2017). How Does Culture Influence Human Behaviour? Retrieved at https://www.quora.com/How-does-culture-influence-human-behavior

Racoma, B. (2018, June 28). Language Shapes the Way People Think and Behave. Retrieved from https://www.daytranslations.com/blog/language-shapes-thinking/.

Safwat, R. F., & Sheikhany, A. R. (2014). Effect of parent interaction on language development in children. The Egyptian Journal of Otolaryngology, 30(3), 255.

Tamis-LeMonda, C. S. & Rodriguez, E. T. (2009). Parents’ Role in Fostering Young Children’s Learning and Language Development. New York, NY: New York University Press.

Vallotton, C., & Ayoub, C. (2011). Use your words: The role of language in the development of toddlers’ self-regulation. Early Childhood Research Quarterly, 26(2), 169-181.

Verial, D. (2018, Nov 28). The Effects of Environment on a Child's Behaviour. Retrieved from https://www.hellomotherhood.com/the-effects-of-environment-on-a-childs-behavior-4892177.html.

Way, J. (2011). Five Components of Effective Oral Language Instruction. Professional Development services for Teachers, 48.

Tarehe ya Uchapishaji
11 May, 2020
Jinsi ya Kunukuu
Wanyenya, W. (2020). Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 2(1), 45-55. https://doi.org/10.37284/eajss.2.1.151

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.