Ushairi wa Kezilahabi ni Ushairi wa Nabhany: Ushahidi Kutoka Uchanganuzi wa Umbo la Shairi la Wanajadi

  • Mohamed Karama, PhD University of Kabianga
  • Issa Mwamzandi, PhD University of Kabianga
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanakariri hoja kwamba ushairi wa Wagunduzi ni ushairi wa Wanajadi. Mapitiyo yetu ya maandishi yanayozungumziya ushairi wa Kiswahili yameonesha kwamba kuna makundi mawili: Wanajadi, akiwamo Sheikh Nabhany, na Wagunduzi, akiwamo Kezilahabi. Yaliyoandikwa yanaonesha kuwa mgogoro ulizuka kutokana na wanajadi kudai kuwa ushairi wa wagunduzi si wa Kiswahili kwa sababu haufwati urari wa vina na mizani na hivo umbo lake ni tafauti na la mashairi ya Kiswahili. Fauka ya hayo, wachanganuzi wa mashairi ya Kiswahili wana maoni kwamba mashairi ya Kezilahabi ni aina mpya ya mashairi ya Kiswahili. Lengo la makala haya ni kugeuza mwendelezo wa fikira hii. Lengo hili limefikiwa kwa kutumiya uainishaji wa mashairi ya Kiswahili uliyotolewa na Mwanajadi Nabhany kwamba umbo la shairi linatokana na mpangiliyo maalumu wa sauti. Kwa kuchanganuwa umbo la shairi moja la Kezilahabi kupitiya kigezo cha bahari ya utumbuizo, ambayo Nabhany ameiorodhesha kuwa bahari mojawapo ya mashairi ya kijadi ya Kiswahili, tumeona kwamba ushairi wa Kezilahabi una sifa zote, ama karibu zote, za bahari hiyo. Kwa sababu hiyo, tunahitimisha kuwa ushairi wa Kezilahabi ni ushairi wa Wanajadi.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
10 April, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Karama, M., & Mwamzandi, I. (2019). Ushairi wa Kezilahabi ni Ushairi wa Nabhany: Ushahidi Kutoka Uchanganuzi wa Umbo la Shairi la Wanajadi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(1), 7-12. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/7

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.