‘Siyasa ni Tʰanga si Nanga’ Mwangwi wa Funzo la Kisiyasa na Azimiyo la Abd̪ilat̪if Abd̪alla Kifungoni: Ut̪afit̪i Kiyelelezo wa Kutendana Katika Sauti ya Dhiki

  • Mohamed Karama, PhD University of Kabianga
  • Issa Mwamzandi, PhD University of Kabianga
  • Khalid Kitito National Museums of Kenya Heritage Training Institute
Sambaza Makala:

Ikisiri

Shairi la Kutendana katika Sauti ya Dhiki limechanganuliwa, mpaka sasa, kwa maono ya juujuu kwamba ni shairi la kingono. Kut̪okana na hit̪imisho hili, Mulokozi amelipuuza kuwa ni shairi lililokosa ubingwa wa kuenreleza maudhui muhimu yanayotatiza jamii. Makala haya yamebayanisha shairi hili kuwa ni fumbo la kisiyasa. Kwa kutumiya madhumuni ya ulingamanishaji wa fasiri ya matukiyo halisi ya kisiyasa katika Kenya wakat̪i huwo na shairi lenyewe; azimiyo la Abd̪ilat̪if katika shairi lenyewe na namna lilivofikiwa; na namna azimiyo hilo lilivoathiri msimamo wake wa kisiyasa baad̪a ya kut̪oka kifungoni, tumeweza kuibuwa maswala muhimu kuhusu maisha ya Abd̪ilat̪if kabla, wakat̪i wa, na baad̪a ya kut̪oka kifungoni. Nadhariya ya Usemezano yenye kud̪ulisha maana kut̪okana na usuli, athari, na mwingiliyano wa kauli nyingi katika mat̪ini na Uhistoriya Mpya yenye kut̪owa fasiri ya matukiyo ya kihistoriya nrizo nadhariya zilizotumika katika uchanganuzi wetu. Kauli mbalimbali zilizojit̪okeza katika mashairi kadhaa ya Sauti ya Dhiki na jazanra zilizotumika zimeweza kufumbuwa ist̪iyara ya shairi hili la Kutendana. Tumeona wahusika wake (wanawake wawili) wanawakilisha vyama va kisiyasa va wakat̪i huwo: KANU (KADU), KPU, na Mwanamume anawakilisha wananchi wa Kenya. Tukiengezeya, Abd̪ilat̪if anajisaili huko gerezani na kupelekeya afanye azimiyo la kujit̪owa katika siyasa za kijumuiya sizisothabit̪i na kuwanasihi wasomaji wengine wasiingiye katika mtego aliyouwingiya yeye. Maisha yake ya kisiyasa baad̪a ya kifungo yanaonekana kufuwata funzo na azimiyo hili.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdalla, A. (2012). Sauti ya dhiki. Nairobi: Oxford University Press.

Abdalla, A. (1985, September). The right and might of a pen. Africa Events, Once upon a time, uk. 25-26.

Abdalla, A. (2015, Disemba 7) Kenya Twendapi? Na Abdilatif Abdalla [video file]. Imesomwa: https://www.youtube.com/watch?v=0soJOZjjCc4

Bakhtin, M. M. (1981). Dialogic Imagination: Four essays. M. Holquist (mh.), C. Emerson & M. Holquist (wat̪afsiri). Austin: University of Texas Press.

Beck, R. M. & Kresse, K. (wah). (2016). Abilaif Aballa: Poet in politics. Dar es Salaam: Mkuki na Nyota.

Biermann, S., Richards, N. & Milbourne, M. (2011, Mei). We Harvest the Present from the Future We Planted Yesterday. Mahojiyano na Abdilatif Abdalla and Ngugi wa Thiong’o, Leipzig, Ujarumani.

Chacha, C. N. (1992). Ushairi wa Abdilatif Abdalla: Sauti ya utetezi. Dar Es Salaam: Dar Es Salaam University Press.

Gibbe, A. G. (1978). Fasihi na jamii baadhi ya washairi wa Kiswahili 1960-1977. Katika Kiswahili 48 (1), 1-25.

Habib, M. A. R. (2005). A history of literary criticism. Malden: blackwell Publishing.

Hamad, M. A. (2017). Suala la ufungwa katika ushairi wa Kiswahili: Mifano kutoka diwani za Sauti ya dhiki na Chembe cha moyo. T̪asnifu ya Uzamili (Haijachapishwa), Chuwo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.

Karanja, M. W. (2014). Matumizi ya istiari, tashbiha na taashira katika diwani ya sauti ya dhiki. T̪asnifu ya Uzamili (Haijachpishwa), Chuwo Kikuu cha Nairobi, Nairobi.

Khamis, S. A. (2016). Whither Swahili literature? Translation and the world recognition of Abdilatif’s “sauti ya dhiki”. Katika R. M. Beck & K. Kresse (wah). Abdilatif Abdalla: Poet in politics. Dar es Salaam: Mkuki na Nyota. UK. 35-44.

Kindy, H. (1971). Life and politics in Mombasa. Nairobi: East African Publishing House.

Maitaria, J. N. & Wafula, R. M. (2018). Ushairi wa Abdilatif Abdalla katika kubainisha utamaduni wa Waswahili. Katika Journal of Linguistics and Language in Education 12 (2), 74-92.

Mazrui. A. & Syambo, B. K. (1992). Uchambuzi wa fasihi. Nairobi: East African Educational Publishers.

Mazrui, A. (2017, Novemba). Abdilatif and I: Reflections on comparative experiences. Makala yaliyowasilishwa katika Kongamano la “The imaginative vision of Abdilatif Abdalla: Kenyan poet and activist” Princeton University, Princeton.

Mulokozi, M. M. (1975). Revolution and reaction in Swahili poetry. Katika Kiswahili 45 (2), 46-65.

Mwamzandi, I. Y. (1996). Mbinu za kimaigizo katika ungo za Abdilatif Abdalla. T̪asnifu ya Uzamili (Haijachapishwa), Chuwo Kikuu cha Egerton, Njoro.

Odinga, O. (1968). Not yet uhuru: An autobiography. Nairobi: Heinemann.

Ohly, R. (1974). A review of Abdilatif Abdalla’s Sauti ya dhiki. Katika Kiswahili 44 (2), 82-91.

Oloo, O. (2003, Februari). Mahojiyano na Abdilatif Abdalla. Imesikizwa: https://web.archive.org/web/20030630105524/http://vancouver.indymedia.org/news/2003/02/32103.php 01/10/2019.

Said, Z. & Taib, A. H. (2019). Fasihi ya ufungwa: Nadharia na mikabala ya uhakiki – riwaya kama kifani. Dar es salaam: Heko Publishers.

Salim, A. I. (1975). Swahili speaking peoples of east africa 1895-1975. Nairobi: East African Publishing House.

Senkoro, F. (1988). Ushairi: Nadharia na tahakiki. Dar Es Salaam: Dar Es Salaam University Press.

Shafi, A. (2003). Haini. Nairobi: Longhorn Publishers

Shariff, I. N. (1988). Tungo zetu: Msingi wa mashairi na tungo nyinginezo. New Jersey: The Red Sea Press.

Topan, F. (1994). Chacha Nyaigotti Chacha, Sauti ya utetezi: Ushairi wa Abdilatif Abdalla: A review. AAP 37, 197-198.

Topan, F. (2006). Why does a Swahili writer write? Euphoria, pain, and popular aspirations in Swahili literature. Katika Research in African Literatures 37 (3), 103-119. Imesomwa: https://www.jstor.org/stable/3821182. 18/10/2019.

Tyson, L. (2006). Critical theory today: A user‑friendly guide (Toleo la 2). New York: Routledge.

Walibora, K. (2009). Prison, poetry, and polyphony in Abdilatif Abdalla’s Sauti ya dhiki. Katika Research in African Literatures 40 (3), 129-148.

Walibora, K. (2016). Doing things with words in prison poetry. Katika R. M. Beck & K. Kresse (wah). Abdilatif Abdalla: Poet in politics. Dar es Salaam: Mkuki na Nyota. UK. 55-64.

Wanjiru, K. (2010). Abdilatif Abdalla: My poems gave me company. Imesomwa: https://www.pambazuka.org/arts/Abdilatif-Aballa-my-poems-gave-me-company tarehe 22/10/2019.

Vierke, C. (2017). What is there in my speaking: Re-explorations of language in Abdilatif Abdalla’s anthology of prison poetry, Sauti ya dhiki. Research in African Literatures 48 (1) 135-157 Doi: 10.2979/reseafrilite.48.1.09.

Tarehe ya Uchapishaji
27 April, 2020
Jinsi ya Kunukuu
Karama, M., Mwamzandi, I., & Kitito, K. (2020). ‘Siyasa ni Tʰanga si Nanga’ Mwangwi wa Funzo la Kisiyasa na Azimiyo la Abd̪ilat̪if Abd̪alla Kifungoni: Ut̪afit̪i Kiyelelezo wa Kutendana Katika Sauti ya Dhiki. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 2(1), 28-44. https://doi.org/10.37284/eajss.2.1.144

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.