Vipengele vya Mwingilianomatini katika Ujenzi wa Maudhui ya Umaskini: Mfano Katika Musaleo! na Bina-Adamu!

  • Esther J Korir University of Kabianga
  • Issa Mwamzandi, PhD University of Kabianga
  • Simiyu` Kisurulia, PhD University of Kabianga
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala  haya yanatathmini matumizi ya vipengele vya mwingilianomatini (MM) katika ujenzi na uwasilishaji wa maudhui ya kazi za Kiswahili. Uchanganuzi huu ni wa kimaktaba kufuatia mihimili ya nadharia ya Mwingilianomatini. Riwaya za Musaleo! na Bina-Adamu zilichaguliwa kimakusudi kwa sababu mwingilianomatini umetumiwa kujenga dhamira ya umaskini. Maudhui ya ulitima katika riwaya za Musaleo! na Bina-Adamu yamechaguliwa ili kudhihirisha jinsi suala sumbufu ulimwenguni  linaweza kuwasilishwa kwa njia mbalimbali. Waandishi wa kisasa wa fasihi wamechangamkia mno matumizi ya mbinu ya mwingilianomatini katika ujenzi wa dhamira za kazi zao. Riwaya za Musaleo! na Bina-Adamu za Wamitila zilirejelewa kama mifano ya kazi zilizojengwa  Ki-MM. Riwaya za kisasa ni muhimu katika jamii kwani maandishi yanahusu masuala yanayomkumba binadamu katika ulimwengu wake sasa, anapojaribu kujitambua na kujieleza.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
24 October, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Korir, E., Mwamzandi, I., & Kisurulia, S. (2019). Vipengele vya Mwingilianomatini katika Ujenzi wa Maudhui ya Umaskini: Mfano Katika Musaleo! na Bina-Adamu!. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(3), 110-117. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/53

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.