Utandawazi na Elimu Tumizi Barani Afrika: Haja ya Mustakabali Mpya kwa Mujibu wa Dunia Yao, Msimu wa Vipepeo na Nakuruto

  • Arthur Kinyanjui Muhia University of Kabianga
  • Issa Mwamzandi, PhD University of Kabianga
  • Simiyu Kisurulia, PhD University of Kabianga
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya ni uchanganuzi wenye madhumuni makuu ya kuchanganua uhusiano uliopo baina ya itikadi ya utandawazi na elimu tumizi barani Afrika kwa mujibu wa riwaya za Dunia Yao (Said A. Mohamed, 2006), Msimu wa Vipepeo (Kyalo Wamitila, 2009) na Nakuruto (Clara Momanyi, 2009). Riwaya hizi zinapendekeza kuwepo kwa mustakabali mpya unaozingatia nafasi ya maarifa asilia ya Kiafrika kwenye elimu tumizi katika kipindi cha utandawazi ili kuikomboa elimu tumizi barani Afrika dhidi ya athari hasi za utandawazi. Ukombozi huo unatarajiwa kufanikisha maendeleo barani Afrika. Uchanganuzi huu wa kimaktaba uliongozwa na nadharia ya Ujumi Mweusi. Kazi za kifasihi ambazo zinarejelewa ziliteuliwa kimaksudi kwa kuwa zinazungumzia suala la utandawazi na elimu tumizi barani Afrika. Kazi hizi zilichanganuliwa ili kuonyesha mtazamo wa kifasihi kuhusu suala tata la elimu tumizi katika jamii. Makala haya yatachangia na kuimarisha uelewaji wa matatizo yanayoikumba sera ya elimu ya Mwafrika ili aweze kutafakari kuhusu elimu tumizi yenye msingi katika maarifa asilia ya Kiafrika jambo ambalo linaweza kufanikisha maendeleo ya Mwafrika na jinsi anavyojiona

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
30 August, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Muhia, A., Mwamzandi, I., & Kisurulia, S. (2019). Utandawazi na Elimu Tumizi Barani Afrika: Haja ya Mustakabali Mpya kwa Mujibu wa Dunia Yao, Msimu wa Vipepeo na Nakuruto. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(2), 68-79. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/20

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.