Usemezano Katika Nyimbo za Amani: Athari za Muktadha wa Kijamii Katika Utunzi na Uimbaji wa Nyimbo za Mhubiri Joel Kimetto na Mwinjilisti Philip Rono

  • Ezekiel Kurgat University of Kabianga
  • Issa Mwamzandi, PhD University of Kabianga
  • Simiyu` Kisurulia, PhD University of Kabianga
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya ni uchunguzi kuhusu athari za muktadha halisi wa kijamii katika utunzi na uimbaji wa nyimbo za amani katika jamii. Nyimbo zilizoteuliwa kimakusudi zilitungwa na kuimbwa na wasanii kutoka jamii ya Kipsigis. Waimbaji wenyewe ni Mhubiri Joel Kimetto na Mwinjilisti Philip Rono. Nyimbo zao zinaangazia ghasia zilizozuka kati ya jamii ya Kipsigis na jamii zingine zinazoishi katika kaunti ya Kericho. Ghasia hizo zilianza tu pindi matokeo ya uchaguzi wa kitaifa wa mwaka wa 2007 yalipotangazwa nchini Kenya. Uchanganuzi huu wa kimaelezo uliongozwa na nadharia ya usemezano iliyoasisiwa na Mikhail Bakhtin. Nyimbo ziliteuliwa kimakusudi kwa kuwa zinazungumzia suala la amani na maridhiano katika jamii. Makala haya yalichanganuliwa kimaelezo ili kubainisha nafasi ya nyimbo za amani katika kusemeza haja ya kuijenga jamii mpya inayoheshimu haki na utangamano. Makala haya yatachangia kuiarifu jamii juu ya haja ya kushirikisha fani ya nyimbo katika kutatua sitofahamu zinazoikumba jamii kutokana na tofauti za kisiasa na kiitikadi.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
24 October, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Kurgat, E., Mwamzandi, I., & Kisurulia, S. (2019). Usemezano Katika Nyimbo za Amani: Athari za Muktadha wa Kijamii Katika Utunzi na Uimbaji wa Nyimbo za Mhubiri Joel Kimetto na Mwinjilisti Philip Rono. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(3), 118-128. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/54

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.