Vipengele vya Fasihi Simulizi Vinavyooana na Hali Katika Taaluma ya Sheria

  • Winnie Musailo Wekesa Chuo Kikuu Cha Masinde Muliro
  • Fred Wanjala Simiyu, PhD Chuo Kikuu Cha Kibabii
  • Nilson Isaac Opande, PhD Chuo Kikuu cha Kisii
Keywords: Vipengele, Fasihi Simulizi, Taaluma, Sheria
Sambaza Makala:

Ikisiri

Utafiti ulilenga kubainisha vipengele maalum vya Fasihi Simulizi vinavyooana na hali katika taaluma ya Sheria. Utafiti uliegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano ya utafiti. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha michakato miwili ya uteuzi wa sampuli; ikiwa ni uteuzi sampuli kimaksudi na kinasibu. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tulioyahudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaji kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Dorsch, T. S. (1965). Classical Literary Criticism Aristotle: On the Art of Poetry; Horace: On the Art of Poetry; Longinus: On the Sublime.

Bassey, M. (1999). Case study research in educational settings. McGraw-Hill Education (UK).

Creswell, J. W., & Creswell, J. D. (2017). Research design: Qualitative, quantitative, and mixed methods approach. Sage publications.

Enon, J. C. (1998). Educational research, statistics and measurement. Kampala: Makerere University.

Doke, C. M. (1948). The basis of Bantu literature. Africa: Journal of the International African Institute, 18(4), 284-301.

Dworkin, R. (2015). How law is like literature. In Law and Literature (pp. 45-62). Routledge.

Fish, S. (1990). Almost Pragmatism: Richard Posner's Jurisprudence.

Fortune, J. (1962). Melon of Ecstasy. London: Hutchinson. ISBN 978-1853754708

Gay, R. (2000). Educational Research Conference for Analysis and Application. (Toleo la 4). New Jersey.

Rutherford, R. B., & Rutherford, R. B. (Eds.). (1992). Homer: Odyssey Books xix and xx. Cambridge University Press.

Jilala, H. (2014). Athari za kiutamaduni katika tafsiri mifano kutoka matini za Kitalii katika makumbusho za Tanzania (Doctoral dissertation, University of Dar es Salaam).

Kombo, D. K., & Tromp, D. L. (2006). Proposal and thesis writing: An introduction. Nairobi: Paulines Publications Africa, 5, 814-30.

Kothari, C.R. (2004). Research Methodology: Methods and Techniques (Toleo la 2): New Delhi: New Age International (P) Ltd.

Kothari, C. R. (2013). Research Methodology: Methods and Techniques (Toleo la 3): New Delhi: New Age International (P) Ltd.

Kress, G. (2008). Meaning and learning in a world of instability and multiplicity. Studies in Philosophy and Education, 27(4), 253-266.

Leedy, P. D. (1997). Practical Research: Planning and Design. (Toleo 6). New Jersey: Prentice- Hall, Inc.

Msokile, M. (1992). Misingi ya Hadithi Fupi. Dar es Salaam: Dar es Salaam Printing Press.

Oso, Y. W. & Onen, D. (2005). A general Guide to Writing Research Proposal and Report. Toleo la 2. Kampala: Makerere University Printery.

Robson, C. (2002). Real-World Research: A Resource for Social Scientists and Practitioner – Researchers (2nd ed.). Oxford: Blackwell Publishers Ltd.

Schenck, H. (2000). The influence of negative advertising frames on political cynicism and politician accountability. Human Communication Research. Thousand Oaks: GA Publication

Spata, G. (2006). The Statesman Yearbook: Politics, Cultures and Economics of the World. Palgrave: Macmillan Ltd

Tracey, M. (1948). The Decline and Fall of Public Service Broadcasting and Production of Political Television. Colorado: University of Colorado Boulder Press.

Wanjala, S. F. (2015). Mwingilianotamzu katika Fasihi Simulizi ya Kiafrika: Mfano wa Embalu na Mwaka Kogwa. Tasnifu ya Uzamifu, Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Tarehe ya Uchapishaji
13 August, 2020
Jinsi ya Kunukuu
Wekesa, W., Simiyu, F., & Opande, N. (2020). Vipengele vya Fasihi Simulizi Vinavyooana na Hali Katika Taaluma ya Sheria. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 2(2), 65-83. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.193