Dhana ya Kifo katika Mashairi Pepe ya Kumwomboleza Ken Walibora kwenye Kumbi za Kulikoni za Wataalam wa Kiswahili, Africa Mashariki

  • Fred Wanjala Simiyu, PhD Chuo Kikuu cha Kibabii
Keywords: Mashairi Pepe, Dhana ya Kifo, Nadharia ya Jazanda
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inachunguza usawiri wa dhana ya kifo katika mashairi pepe yaliyotumiwa na malenga mbalimbali katika kuomboleza kifo cha hayati Ken Walibora. Kifo kinapotokea, wanajamii huomboleza kwa namna tofautitofauti kutegemea mila na desturi za jamii husika Barani Afrika. Kifo cha Ken Walibora kilivuta hisia za malenga wengi ambao walimwomboleza mtunzi mwenzao kwa kutunga mashairi mbalimbali. Katika huko kuomboleza, malenga hawa walieleza asili, maana na madhara ya kifo cha Ken Walibora kwa jamii nzima ya Waswahili. Katika makala hii, mashairi pepe sita (6) yalikusanywa kutoka kwenye kumbi za kulikoni za wataalam wa Kiswahili, Afrika Mashariki. Mashairi haya teule yamechambuliwa ili kujibu maswali kama vile; Je kifo cha Ken kilisababishwa na nani? Je, kifo chake kilikuwa kizuri au kibaya? Je, Ken ataendelea kuishi miongoni mwa Waswahili hata baada ya kifo chake? Kifo chake kimesababisha madhara gani katika jamii ya Waswahili? Masuala haya na mengine yamedadavuliwa kwa kuchanganua mashairi teule yaliyotungwa kwa ajili ya kuomboleza kifo cha marehemu Ken Walibora. Uchambuzi huu ulifanywa kwa kuongozwa na Nadharia ya Jazanda. Kwa ujumla, Nadharia ya Jazanda ilitumika katika kupasua istiari zilizotumiwa na malenga katika kueleza asili, maana na madhara ya kifo cha Ken Walibora katika mashairi teule

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Alembi, E. (2002). The Construction of the Abanyole Perceptions on DeathThrough Oral Funeral Poetry. Tasnifu ya Uzamifu, Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Alex D. (2008). Death and Dying in the History of Africa Since 1800. The Journal of African History, Volume 49, Issue 3. Pp. 341-359.

Baloyi, L., na Makobe-Rabothata, M. (2014). The African conception of death: A cultural implication. In L. T. B. Jackson, D. Meiring, F. J. R. Van de Vijver, E. S. Idemoudia, & W. K. Gabrenya Jr. (Eds.), Toward sustainable development through nurturing diversity: Proceedings from the 21st International Congress of the International Association for Cross- Cultural Psychology. https://scholarworks.gvsu.edu/iaccp_papers/119/.

Bibilica (2011). Holy Bible: New International Version. Nairobi: Longhorn.

Cameron, L. and Low, G. (Wah). (1999). Researching and applying metaphor. London: Cambridge University Press.

Gibbs, R.W. na Steen, G. (EDS) (1999). Metaphor in Cognitive Linguistic. Amsterdam: Benjamins.

Goatly, A. (2008). Washing the Brain. Metaphor and hidden Ideology. Amsterdam: John Benjamins.

Hackett, R.I.J. (2011). A Rationalization of an African Concept of Life, Death and the Hereafter, katika American Journal of Social and Management Sciences, 2(1): 171-175.

Holdstock. T.L. (MH). The Concept of Death in Sub-Saharan Africa - lh {teu,te} slt44,d. li.oe,. e.r^ dsej i^ de. a.--t - ucatecailleude. au l+lrfe" ^ . le-u*iscacrt.

Kövecses, Z. (2010). Metaphor: A Practical Introduction. 2nd ed. Oxford University Press.

Lakoff, G., & Johnson, M. (1980). Johnson Metaphors We Live by. Chicago: University of Chicago Press.

Mbiti, J.S. (1980). African Religions and Philosophy. London: Heinemann.

Musolff, A. (2012) . The study of metaphor as part of critical discourse analysis. Published

online: 25 May 2012 https://doi.org/10.1080/17405904.2012.688300

Njogu, K. (2020). Kumbukizi ya Kenneddy Waliaula Walibora, katika Swahili Forum 27(2020): 17-26.

Rabi I. E., na Bolatito, L. (2016). African Cultural Concept of Death and the Idea of Advance Care Directives, katika Indian Journal of Palliative Care Vol 22 / Issue 4. DOI: 10.4103/0973- 1075.191741.

Simiyu, F. W. (2020). Safina ya Utafiti wa Fasihi Simulizi. Kakamega: Elgon Epitome Publishers Ltd.

Tarehe ya Uchapishaji
7 April, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Simiyu, F. (2024). Dhana ya Kifo katika Mashairi Pepe ya Kumwomboleza Ken Walibora kwenye Kumbi za Kulikoni za Wataalam wa Kiswahili, Africa Mashariki. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 193-211. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1855