Maelezo Kinzani ya Vipengele vya Sarufi ya Kiswahili Katika Vitabu Teule vya Shule za Upili Nchini Kenya

  • Wanyonyi Fred Wanjala Chuo Kikuu cha Kibabii
  • Misiko David Wasike, PhD Chuo Kikuu cha Kibabii
  • Fred Wanjala Simiyu, PhD Chuo Kikuu cha Kibabii
Keywords: Sarufi, Sarufi Amilifu, Vipengele Tata, Ujifunzaji Kitajiriba, Nomino Za Kawaida, Nomino Za Mguso, Kizuiwa Kwamiza, Kirai
Sambaza Makala:

Ikisiri

Dhamira ya makala hii ilikuwa ni kuonesha tofauti za kimaelezo baina ya waandishi wa sarufi kama inavyojitokeza katika ufundishaji na ujifunzaji wa Sarufi ya Kiswahili katika shule za upili hapa nchini Kenya. Uchunguzi huu uliongozwa na Nadharia ya Sarufi Amilifu na nadharia ya Ujifunzaji Kitajiriba. Sarufi Amilifu ni ya Simon C. Dik (1978). Nadharia hii inashikilia kwamba, uzingatifu wa sarufi ya lugha unadhihirika katika utendaji wa lugha hiyo ambao unakuzwa katika matini inayoandaliwa na wataalamu wake. Nayo nadharia ya Ujifunzaji Kitajiriba iliyoasisiwa na David Allen Kolb mnamo mwaka wa 1984 inaangazia matumizi ya tajiriba katika ufundishaji na ujifunzaji. Kundi lengwa lilikuwa ni waandishi wa Sarufi ya Kiswahili, walimu wa Sarufi ya Kiswahili na wanafunzi wa kidato cha tatu. Tulitumia mbinu za usampulishaji wa kinasibu na usampulishaji wa kimakusudi kuteua sampuli iliyokusudiwa tukizingatia asilimia 30 ya jumla ya idadi lengwa. Walimu 12 na wanafunzi 120 waliteuliwa kushiriki katika uchunguzi huu. Data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo, hojaji na mahojiano. Data katika makala hii iliwasilishwa kupitia maelezo, majedwali na asilimia. Matokeo ya makala hii yalionesha kwamba, waandishi wa Sarufi ya Kiswahili wanakinzana katika ufafanuzi wa baadhi ya vipengele vya Sarufi ya Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya.

Uchunguzi huu utakuwa wenye umuhimu kwa walimu wa Sarufi ya Kiswahili, wanafunzi, wataalamu wa Sarufi ya Kiswahili na wale wanaoandaa na kuchapisha vitabu vya Sarufi ya Kiswahili kwa kutambua vipengele tata katika Sarufi ya Kiswahili. Makala ilipendekeza Taasisi ya Ukuzaji wa Mitalaa ya Kenya kuvichunguza upya vitabu vya kiada na ziada vya Sarufi ya Kiswahili ambavyo vimeidhinishwa na wao huku vikiwa na tofauti za kimaelezo.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abai, R. A., & Nyandiba, C. (2019). Athari za Uandishi na Uchapishaji wa Vitabu vya Kiada katika Ufundishaji wa Kiswahili nchini Kenya. Katika Kobia, J. M., Kandagor, M., Mwita, L. C., Mataira, J. N. na Simwa, S. P. (Wahariri) (2019). Uwezeshwaji wa kiswahili kama wenzo wa maarifa. Eldoret: Moi University Press.

Bruno, E. (2020). A grammar of paraquayan guarani: Phonology and orthography: the sound system and its written representation. UCL Press. Downloaded from https://www.jstor.org//stable/j.ctv13xpscn.8.

Dik, C. S. (1978). The Theory of Functional Grammar: Part 1: The Structure of the Clause. Dordrecht: Foris.

Habibu, N. (2017). Muundo wa kirai kitenzi katika lugha ya Kisambaa. Juzuu ya 21. Kutoka nasra.habibu@out.ac.tz.

Halliday, M. A. K. (1994). Functional Grammar. Birmingham: University of Birmingham Press.

Ipara, I. & Waititu, F. (2011). Ijaribu na Uikarabati: Marudio ya KCSE Kiswahili. Nairobi: Oxford University Press, East Africa Ltd.

Kiai, A.W. & Maroko, G. M. (2013). Textbook Selection Experiences among Secondary School Teachers of English in Kenya. International Journal of Education and Research: Vol. 1 No. 12.

Kolb, D. A. (1984). Experiential Learning Theory. A Dynamic, Holistic Approach to Management Learning, Education and Development. Downloaded at: https://www.researchgate.net/publication/267974468

Kolb, D. A. & Kolb, A, Y. (2011). Experiential Learning Theory: A Dynamic, Holistic Approach to Management Learning, Education and Development. Inapatikana: https://www.researchgate.net/publication/267974468.

Landrum, R. E., Gurung, R.A.R & Spann, N. (2012). Assessments of Textbook Usage and the Relationship to Student Course Performance. Boise: Taylor and Francis Group, LLC.

Leigh, L. (2007). The power of prepositions. Cairo: Criminal Brief Press.

Massamba, D. T., Kihore, M.Y. & Hokororo, J. I. (1999). Sarufi miundo ya Kiswahili sanifu (SAMIKISA). Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mogambi, H. (2015). Golden Tips: Kiswahili Kwa Shule za Upili. Nairobi: Moran (E.A.) Publishers Limited.

Mumbo, C. K. & Ngamia, F. O. (2003). Johari ya Kiswahili: Kidato cha Pili. Nairobi: East African Educational Publishers Ltd.

Navaz, A. M. N. & Sama, F. R. F. (2018). Teaching grammar in the English language classroom: Perception and Practices of students and teachers in the Ampara District. Sirlanka: South Eastern University of Sirlanka Press.

O’Neill, R. (1982). Why use textbooks? ELT Journal, Vol 36, Pages 104-111.

O’Grady, W., Dobrovolsky, M., & Katamba, F. (1996). Contemporary Linguistics: An introduction. Harlow Essex, Longmna Publishers.

Omwaka, H. & Gichuhi, N. (2006). Longoman: Marudio ya KCSE. Longman Kenya Ltd.

Olodo, R. & Njogu, K. (2005). Tanzu za Lugha: Kitabu cha Mwanafunzi Kidato cha Nne. Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation.

Richards, J.C. (2001). The Role of Textbooks in a Language Programme. Cambridge: Seameo Relc Publication.

Timammy, R. & Oduor, A. J. O. (2016). Treatment of Kiswahili in Kenya’s Education System. Nairobi: University of Nairobi Journal of Language and Linguistics.

Tomlinson, B. (1998). Materials Development in Language Teaching. United Kingdom: Cambridge University Press.

Wamitila, K. W. (2004). Chemchemi za Kiswahili: Kidato cha Tatu. Nairobi: Longhorn Publishers (Kenya) Ltd.

Wamitila, K. W. (2015). Chemchemi za Kiswahili: Kidato cha Nne. Nairobi: Longhorn Publishers (Kenya) Ltd.

Wamitila, K. W. & Waihiga, G. (2010). Chemchemi za Kiswahili: Kidato cha Pili. Nairobi: Longhorn Publishers (Kenya) Ltd.

Walibora, K. & Wang’endo, F. (2004). Uhondo wa Kiswahili: Kwa Shule za Upili Kitabu cha Mwanafunzi Kidato 1. Nairobi. Moran (E. A.) Publishers Limited.

Waititu, F., Ipara, I. & Okaalo, B. (2015). Kiswahili Fasaha, Kidato cha Tatu. Nairobi: Oxford University Press.

Waititu, F., Ipara, I., Okaalo, B. & Vuzo, A. (2004). Kiswahili Fasaha, Kidato cha Pili. Nairobi: Oxford University Press.

Waititu, F., Ipara, I., Okaalo, B. & Vuzo, A. (2004). Kiswahili Fasaha, Kidato cha Tatu. Nairobi: Oxford University Press.

Waititu, F., Ipara, I. & Okaalo, B. (2003). Kiswahili Fasaha, Kidato cha Kwanza. Nairobi: Oxford University Press, East Africa Ltd.

Wong, V. & Bar-Yam, Y. (2017). How do people differ? A Social Media Approach. Cambridge: 210 Broadway Publication.

Vonyoli, A. J., Watuha, A. I., Mutekwa, F. O., Makombo, H. S., Maina, K. D. & Waweru, M. (2014). Kiswahili Kitukuzwe: Kwa Kidato cha Kwanza, Kitabu cha Mwanafunzi (Toleo la Tano). Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Vonyoli, A. J., Watuha, A. I., Mutekwa, F. O., Makombo, H. S., Maina, K. D. & Waweru, M. (2014). Kiswahili Kitukuzwe: Kwa Kidato cha Pili, Kitabu cha Mwanafunzi (Toleo la Tano). Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Vonyoli, A. J., Watuha, A. I., Mutekwa, F. O., Makombo, H. S., Maina, K. D. & Waweru, M. (2014). Kiswahili Kitukuzwe: Kwa Kidato cha Tatu, Kitabu cha Mwanafunzi (Toleo la Tano). Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Vonyoli, A. J., Watuha, A. I., Mutekwa, F. O., Makombo, H. S., Maina, K. D. & Waweru, M. (2014). Kiswahili Kitukuzwe: Kwa Kidato cha Nne, Kitabu cha Mwanafunzi (Toleo la Tano). Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Tarehe ya Uchapishaji
1 Juni, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Wanjala, W., Wasike, M., & Simiyu, F. (2021). Maelezo Kinzani ya Vipengele vya Sarufi ya Kiswahili Katika Vitabu Teule vya Shule za Upili Nchini Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 3(1), 30-50. https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.335