Uainishaji wa Mbinu na Viwango vya Usimulizi katika Uendelezaji wa Riwaya ya Kiswahili: Mfano wa Riwaya ya Bina-Adamu! na Babu Alipofufuka

  • Kimatwek Betty Chepkogei Chuo Kikuu cha Kisii
  • Nilson Isaac Opande Chuo Kikuu cha Kisii
  • Ezra Nyakundi Mose Chuo Kikuu cha Kisii
Keywords: Usimulizi, Uhalisia, Ulimwengu mpya na Naratolojia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanaainisha mbinu na viwango vya usimulizi katika riwaya ya Kiswahili. Uchunguzi huu ulichanganua riwaya mbili za Kiswahili zilizoteuliwa kimaksudi kwa uchunguzi wa matumizi ya mbinu ya usimulizi kama mtindo wa uendelezaji wa hadithi na utunzi wa riwaya ya Kiswahili ya kisasa. Riwaya zilizoteuliwa ni Bina-Adamu! na Babu Alipofufuka. Uchunguzi uliongozwa na nadharia ya Naratolojia iliyoongoza uchanganuzi wa mbinu na viwango vya usimulizi vinavyochangia katika uendelezaji wa malengo ya matunzi na utunzi wa riwaya ya Kiswahili. Usimulizi uliowasiliswa kwa vielelezo vya visanduku vya kichina vilivyowakilisha aina mbalimbali za usimulizi ndani ya usimulizi. Data ilikusanywa na kuchanganuliwa kithamano kutokana na riwaya teule kwa kusoma na kudondoa nukuu muhimu za usimulizi wa viwango mbalimbali. Matokeo ya utafiti yaliasilishwa kimaelezo na kwa michoro kuwakilisha viwango mbalimbali vya usimulizi wa hadithi ndogo ndani ya hadithi kuu. Utafiti ulibaini kuwa usimulizi katika mtindo wa viwango mbalimbali vya kidaraja ulitumika kujenga umbo la kipekee la hadithi. Usimulizi katika viwango au daraja mbalimbali ulihusisha hadithi ndogo za aina ya visasili zilizosimuliwa ndani ya hadithi kuu ambao ni mtindo wa utunzi wa riwaya mpya ya Kiswahili na mtindo huo ulichangia katika kuendeleza, kukuza na kuhifadhi mbinu za kijadi ya Fasihi Simulizi katika Fasihi Andishi ya kisasa

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Genette, G. (1980). Narrative Discourse; An Essay in Method.Ithaca: Cornell University Press.

Jahn, M. (2005). Narratology: A Guide to the Theory of Narrative. Cologne: University of Cologne.Retrieved from: www.uni-koeln.de/ame02.pppn.htm.

Kenan, S. (1983). Narrative Fiction Contemporary Poetics. London: Rouledge.

Mohammed, S.A. (2001). Babu Alipofufuka. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Mose, E. N. (2021). Motifu ya sanaa za maonyesho ya jadi katika tamthilia ya kiswahili: mfano wa mashetani, pungwa, ngoma ya ng’wanamalundi na mashetani wamerudi (Doctoral dissertation, Moi University).

Torodov, T. (1969). Structural Analysis of Narrative: The Morton Anthropology of Theory and Critism. (eds). New York:W.W. Norton and Company.

Wamitila, K.W. (2002). Bina-Adamu! Nairobi: Phoenix Publishers,

Tarehe ya Uchapishaji
12 December, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Chepkogei, K., Opande, N., & Mose, E. (2023). Uainishaji wa Mbinu na Viwango vya Usimulizi katika Uendelezaji wa Riwaya ya Kiswahili: Mfano wa Riwaya ya Bina-Adamu! na Babu Alipofufuka. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(2), 44-54. https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1620