Usawiri wa Vijana wa Kisasa katika Riwaya ya Dunia yao ya Kiswahili

  • Naomi Nzilani Musembi, PhD Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Cha Jaramogi
  • Fred Wanjala Simiyu, PhD Chuo Kikuu cha Kibabii
Keywords: Vijana, Usawiri, Riwaya Mpya
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii itachunguza usawiri wa vijana katika dunia ya sasa inayobadilika kila uchao. Itafanya hivi kupitia uchanganuzi wa riwaya mpya ya Dunia Yao (2006) ya S.A Mohamed.  Utafiti unaonyesha kwamba vijana kote duniani sasa wana utamaduni wao ambao watafiti wanaueleza kama ‘ulimwengu huru’ wa vijana ulio na mitindo na njia za maisha ambazo, vijana hufuata ili kujitofautisha na utamaduni wa wazazi wao. Utamaduni wa vijana kwa kiasi kikubwa ni zao la maendeleo katika jamii za ulimwengu. Kadri jamii inavyosonga mbele kimaendeleo, ndivyo ambavyo utamaduni wa vijana unakuzwa, unaimarishwa na kusambazwa miongoni mwa vijana kote duniani. Vijana wamebuni utamaduni wao kama njia moja ya kuasi dhidi ya utamaduni uliotawaliwa na wazee. Wanataka kujihusisha na tabia kama matumizi ya dawa za kulevya, ushoga, uasi wa maadili ya kijamii, Mitindo mipya ya mavazi, muziki miongoni mwa tabia nyingine ambazo wanajua huwatenga wazee. Hii ni tabia ibuka ya vijana kupania kuonyesha nguvu na uwezo wao katika jamii. Ujumbe wanaopitisha ni kuwa hawako tayari kushiriki utamaduni unaowadhibiti na kuwanyima nafasi yao katika jamii. Malengo mahususi yatakayoongoza makala haya ni pamoja na kuangazia sifa za vijana wa kisasa na wakati huo huo kufafanua njia mabazo wanajamii wanaweza kutumia ili kujaribu kuziba mwanya mpana uliopo kati ya kizazi cha jana na cha leo. Makala hii itaongozwa na nadharia ya uhalisia. Mhimili mkuu wa nadharia ya uhalisia ambao utaongoza makala ni kwamba, fasihi ni kioo cha jamii na inapaswa kumulika maisha kama yalivyo. Muundo wa kimaelezo utatumika kuchanganua data. Data itakusanywa kutokana na kusoma riwaya teule na kudondoa sehemu zinazolingana na malengo ya utafiti. Data itadondolewa, itanukuliwa, itapangwa kisha kuchanganuliwa kulingana na mada husika

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Brake, M. ( 1980). The Society of Youth Culture and Youth Subcultures: Sex,Drugs and Rock ‘n’ Roll? London: Routledge and Kegan Paul.

Kaplan, E. A. (1989). Rocking Around the Clock: Music,Television, Postmodernism and Consumer Culture. London: Mathuen.

Kaui, M. (2008). Usawiri wa Vijana katika Tamthilia teule za Kiswahili. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta (Haijachapishwa).

Kavuria, P. (2008). Dhuluma Dhidi ya Watoto katika Riwaya Ya Kiswahili. Tasnifu ya M.A. Chuo Kikuu cha Kenyatta (Haijachapishwa).

Kimilu, D. ( 1962). Mukamba wa Wuo. Nairobi: East Africa Literature Bureau.

Mohamed, S.A. (2006). Dunia Yao. Oxford University Press: Nairobi, Kenya.

Musembi, N. N. (2018). Nafasi ya Fasihi Simulizi katika Jamii Inayobadilika, Karne ya 21. Tathmini ya Nyimbo za Jamii ya Wakamba. Makala yaliyowasilishwa katika Kongamano la CHAUKIDU, SUZA.

Musembi, N. N. (2022). Ukataji Tamaa Miongoni mwa Watoto katika Jamii ya Kisasa. Tathmini kutoka Riwaya ya Kiswahili. Katika Jarida la CHAKAMA. Juzuu 1 uk. 141-147.

Wamitila, K. W. (2008). Kanzi ya Fasihi. Nairobi: Vide-Muwa Publishers Limited.

Tarehe ya Uchapishaji
2 January, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Musembi, N., & Simiyu, F. (2024). Usawiri wa Vijana wa Kisasa katika Riwaya ya Dunia yao ya Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 1-10. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1669