Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari

  • Winnie Musailo Wekesa Chuo Kikuu Cha Masinde Muliro
Keywords: Mkabala, Uchanganuzi, Changamano, Kiada
Sambaza Makala:

Ikisiri

Rasimu ya mtalaa mpya wa elimu nchini Kenya imebaini vipengele anavyopaswa kuzingatishwa mwanafunzi ili kuimarisha uwezo na maarifa yake katika ujifunzaji wa Kiswahili. Hali hii imetokana na mpango wa kufanyia mtaala wa elimu mabadiliko ili kumudu mahitaji ya jamii katika karne ya ishirini na moja. Silabasi ya sasa ya Kiswahili kwa shule za upili inaeleza kwa wazi vipengele vya kufundishwa katika sarufi na matumizi ya lugha. Sentensi ni mojawapo ya vipengele vya sarufi vinavyofundishwa katika shule za upili kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Kuna aina tatu kuu za sentensi kimuundo; miongoni mwazo ikiwa ni sentensi changamano Makala haya itaangazia aina hii ya sentensi kwa msingi wa uchanganuzi wake kutumia mikabala mbalimbali. Pengo lililopo ni kwamba vitabu vya kiada vilivyopendekezwa na Taasisi ya Ukuzaji wa Mtaala kisha kuidhinishwa na wizara ya elimu nchini; vimerejelea mada hii kwa mtazamo tofauti tofauti. Hali ambayo inazua mkanganyo na kuathiri mchakato wa ufunzaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi. Mada ya uchanganuzi wa sentensi inapasa kutiliwa msingi katika kidato cha kwanza na pili kisha kusisitizwa katika kidato cha tatu na  nne. Kinyume na inavyojitokeza katika vitabu hivi vya kiada ambapo ufundishaji wa mada hii unaanzia kidato ha tatu na kukamilishwa katika kidato cha nne. Masebo (2002), anasema uchanganuzi wa sentensi ni kipengele cha sarufi miundo ambacho ni utanzu unaoshughulikia maneno katika tungo na uhusiano wa vipashio vyake. Ni muhimu mwanafunzi kupata mwelekeo faafu wa mada hii kwa kuelekezwa kwa njia na namna moja sio kwa kuhitilafiana. Lugha kando na kuwa ni chombo muhimu cha kujieleza, pia ina jukumu la kupitisha elimu faafu

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Chimera, R. M. (1996). Kiswahili: Past, Present and Future Horizons. Nairobi: University of Nairobi Press.

Cohen, L., Manion, L. na Keith M. (2000). Research Methods in Education. (6th ed.) London: Routledge.

Illes, J. (2009). Encyclopedia of 5000 Spells. HarperCollins: NewYork.

Ipara, I. O. (2007). “Utekelezaji wa silabasi mpya ya somo la Kiswahili katika shule za upili: Mtazamo wa walimu.” Katika Kimani Njogu (mh). Kiswahili na Elimu nchini Kenya. Limuru: Kolbe Press.

K.I.E. (2002). Secondary education syllabus vol. 1. Nairobi: Kenya Institute of Education.

Masebo, J. A. (2002). Kiswahili: kidato cha 3 na 4. Dar es Salaam: The General Booksellers Ltd.

Mbunda, M. (1985). Historia na matumizi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Educational Publishers and Distributors Ltd.

Mulokozi, M.M. (1999). Publishing in Kiswahili: a writer’s perspective. Publishing in African Languages. Challenges and Prospects. Chicago:

Nsubuga, E. H. K. (2000). Fundamentals of Educational Research. Kampala: MK Publishers (U) Ltd.

Sedlack, R. G na Stanley, J. (1992). Social Research: Theory and Methods. Indiana University: Allyn and Bacon.

Tarone, E. 1998. A sociolinguistic perspective on an SLA theory of mind. Studia Anglica: Posnaniensa. 23.431-444

TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili sanifu (toleo la pili). Nairobi: Oxford University Press.

Ur, P. (1991). A Course in Language Teaching, Practice and Theory. Cambridge: Cambridge University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
14 Oktoba, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Wekesa, W. (2022). Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 15-28. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.886