Dhima ya Umahuluti wa Utamaduni katika Uamilishaji wa Nyimbo za Harusi Miongoni mwa Wanandi

  • Jenniffer Chepleting Koech Catholic University of Eastern Africa
  • Fred Wanjala Simiyu, PhD Kibabii University
  • Margan Adero Catholic University of Eastern Africa
Sambaza Makala:

Ikisiri

Wakenya wengi hushutumu suala la umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za wasanii maarufu nchini. Madai yao ni kuwa umahuluti wa utamaduni husababisha kupotea kwa utamaduni asili wa jamii mbalimbali za Wakenya na kuiga ule wa Wakoloni. Utafiti huu ulikusudia kuhakiki dhima ya umahuluti wa utamaduni katika uamilishaji wa nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Wanandi nchini Kenya. Nadharia ambayo iliongoza utafiti huu ni ya ubaada ukoloni. Baadhi ya wahasisi wakuu wa nadharia hii ni Homi Bhabha, Gayatri Chakravorty Spinak, Edward Said, Robert Young na Bill Ashcroft. Mtafiti alipata data yake kupitia usaili na uchanganuzi wa yaliyomo kwenye vipindi vya Tumdo katika runinga ya Kass. Jumla ya wahojiwa nane walisailiwa kutoka kata ya Chepsaita, eneo la kaunti ndogo ya Turbo kwenye kaunti ya Uasin-Gishu. Idadi kubwa ya wakazi wa Uasin-Gishu ni Wanandi ambao walihamia eneo hilo kutoka kaunti ya Nandi; kwa hivyo wameingiliana na jamii zingine wa hapa nchini na kimataifa. Sampuli tajwa ilitumiwa kuteua wasailiwa. Nadharia ya ubaada ukoloni iliwaongoza mtafiti kubainisha vipengele vya umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za harusi. Hatimaye data iliyokusanywa iliwasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mifano. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa: Nyimbo za harusi miongoni mwa Wanandi kwenye runinga ya Kass zina vipengele vingi vya utamaduni wa jadi katika jamii ya Wanandi. Vilevile, nyimbo hizo zina baadhi ya vipengele vigeni hasa vinavyochangiwa na teknolojia na mwingiliano baina ya Wanandi na jamii zingine. Kadhalika umahuluti wa utamaduni umesaidia nyimbo za harusi miongoni mwa Wanandi kutekeleza majukumu yake katika jamii ya sasa. Kwa hivyo, utafiti huu ni muhimu kwa taaluma ya fasihi simulizi na vyombo vya habari hasa kwa wale walimu na wanafunzi watakaotaka kufanya utafiti wa suala la dhima ya umahuluti wa utamaduni katika nyimbo za harusi kwenye jamii za kiafrika.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
15 November, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Koech, J., Simiyu, F., & Adero, M. (2019). Dhima ya Umahuluti wa Utamaduni katika Uamilishaji wa Nyimbo za Harusi Miongoni mwa Wanandi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(4), 142-150. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/62

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.