Masimulizi Katika Mchakato wa Ufundishaji wa Kipengele Maalum cha Msuko Katika Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na Ile Ya Chozi la Heri.

  • Stephen Muyundo Ndinyo Kibabii University
  • Fred Wanjala Simiyu, PhD Kibabii University
  • Deborah Nanyama Amukowa, PhD Kibabii University
Sambaza Makala:

Ikisiri

Masimulizi katika mchakato wa ufundishaji wa vipengele maaalum vya msuko katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na ile ya Chozi la Heri. Lengo la Makala haya lilikuwa ni kubainisha namna ambavyo masimulizi yalivyojitokeza katika mchakato wa ufundishaji wa kipengele maalum cha msuko katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na ile ya Chozi la Heri. Utafiti huu ulitumia muundo wa kithamano mkabala wa kimfano. Mbinu za ukusanyaji data zilizotumiwa ni uchunzaji usaili na majadiliano ya vikundi viini. Data iliwasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi ,majedwali, nukuu za dondoo kutoka kwa mahojiano. Sampuli lengwa ilihusisha shule 10 kati ya 27, wasailiwa 18 kati ya 54 katika Kaunti ndogo ya Navakholo. Matokeo ni kwamba matukio yalitiririshwa katika mchakato wa ufundishaji wa vipengele maalum vya fani na maudhui katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na ile ya Chozi la Heri.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
22 Agosti, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Ndinyo, S., Simiyu, F., & Amukowa, D. (2019). Masimulizi Katika Mchakato wa Ufundishaji wa Kipengele Maalum cha Msuko Katika Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na Ile Ya Chozi la Heri. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(2), 48-54. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/25

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.