Baadhi Ya Sifa Za Sauti Zoloto Zinazotumiwa Na Baadhi Ya Wahubiri Wa Kipentekosti Kuwasilisha Injili Na Umuhimu Wake

  • Teresiah Nyambura Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Peter Githinji, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Kanisa za Kipentekosti, Kanisa zisizo za Kipentekosti, Sauti Zoloto, Uzolotaji, Wapentekosti, Wasikilizaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yalilenga kubainisha baadhi ya vigezo vinavyobainisha sauti zoloto zinazotumiwa na baadhi ya wahubiri wa Kipentekosti kama mtindo wa kuwasilisha injili. Tulilenga waumini wa madhehebu tofauti ya Kipentekosti katika eneo la Gilgil katika kaunti ya Nakuru. Tulitumia mihimili miwili ya nadharia ya “Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji” (Bell, 1984, 2014). Mhimili wa kwanza unadai kuwa Mtazamo wa wasikilizaji hutumika katika viwango vyote vya lugha iwe ni lugha moja au wingi lugha kwani haiangazii tu kubadilisha mtindo wa utamkaji wa sauti, bali pia uchaguzi wa jinsi ya kutamka sauti na upole wa mazungumzo. Mhimili wa pili hudai kuwa mtindo wa matumizi ya lugha katika uzungumzaji huwa chanzo cha mabadiliko katika mahusiano ya mazungumzo. Usampulishaji wa kimaksudi ulitumika kwa sababu ya urahisi wa kupata walengwa wa makala haya. Kiasa kikubwa cha data kilitokana na kanda za sauti za mahubiri mbalimbali kutoka kwa wahubiri tofauti. Hatimaye, kanda tatu ambazo wahubiri walizolota na tatu ambazo wahubiri hawakuzolota zilitumika. Kanda za mahubiri zilichujwa kwa kutumia programu ya PRAAT ili kupata sifa za kiakustika zinazobainisha sauti zoloto. Mbinu za hojaji, mahojiano na wahubiri binafsi, uchunzaji na mahojiano na makundi legwa zilitumika katika uchanganuzi na ufasili wa data. Matokeo ya utafiti yalibainisha vigezo vikuu vitano ambavyo ni kipimo cha hezi, urefu wa mawimbi ya sauti, kiwango cha desibeli, mpumuo wa sauti, kiwango cha tambo na tofauti kati ya fomanti ya kwanza na ya pili kama baadhi ya sifa zinazobainisha sauti zoloto za wahubiri wa Kipentekosti

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Adam, M. (2017). Persuasion in Religious Discourse: Enhancing Credibility in Sermon Titles and Opening. Discourse and Interaction, 10, 2: 5-25.

Anderson, R. C., Klofstand, C. A., Mayew, W. J., & Venkatachalam, M. (2014). Vocal Fry May Undermine The Success of Young Women in The Labor Market. PLOS ONE, 9(5): e97506. doi:10.1371/journal.pone.0097506.

Bell, A. (1984). Language Style as Audience. Design Language in Society, 13, (2), 145-20

Bell, A. (1997). Style as Audience Design. In Nikolas Coupland and Adam Jaworski (Eds),

Sociolinguistics: A Reader and Coursebook. London (pp. 240–50). Macmillan.

Bell, A. (2014). Language when Contents Collapse: Audience Design in Social Networkings

Discourse, Content & Media 462-73.

Bellavance, S. R. (2021). Glottalization Variation in Young Speakers. Vermont University of Pennsylvania Working Papers in Linguistics, 27(1-3). https://repository.upenn.edu/pwpl/vol27/iss1/3

Belotel-Grenié, A., & Grenié, M. (2004). The Creaky Voice Phonation And The Organisation Of Chinese Discourse. International Symposium on Tonal Aspects of Languages: With Emphasis on Tone Languages, Beijing, China, March 28-31, 2004

Belotel-Grenié, A & Grenié, M. (1994). Phonation Type Analysis in Standard Chinese. 3rd International Conference on Spoken Language Processing (ICSLP 94), Yokohama, Japana, Sept 18-22, 1994)

Brown, P. & Levinson. S.C. (1987). Politness: Some Universals in Language Usage. Cambridge:

Cambridge University Press.

Crystal, D. & Davy, D. (1969). Investigating English Style. New York: Longman.

Esposito, L. G. (2015). I Am a Perpetual Underdog': Lady Gaga's Use of Creaky Voice in the Construction of a Sincere Pop Star Persona. Unpublished Masters Thesis. Swarthmore University

Gichuki, D. M. (2015). Conflict in Pentecostal Churches: The Case of Christian Church

International, Kiria-ini Town, Murang`a County, Kenya. Unpulished Masters Thesis.

Kenyatta University.

González, G., De Los Dngeles, M. & Sánchez, R.T. (2016). English Pronunciation for Speakers of Spanish: From Theory to Practice. Berlin, Boston: De Gruyter Mouton.

Hedelin, P. & Huber, D. (1990). Pitch Period Determination of Aperidic Speech Signals. In International Conference of Acourstics, Speech and Signal Processing (pp. 361-364).Held in Albuquerque, NM (April 3-5)

Hildebrand-Edgar, N. (2014). Creaky voice: An interactional resource for indexing authority.

Unpublished Masters Thesis. University of Crocker.

Holt, G. S. (1972). Stylin’ Outta the Black Pulpit. In Thomas Kochman (ed.), Rappin’ and

Stylin’ out: Communication in Urban Black America, (pp. 189–204). Urbana: University

of Illinois Press.

Hornibrook, J., Ormond, T., & Maclagan, M. (2018) Creaky Voice or Extreme Vocal Fry in Young Women. The New Zealand Medical Journal 131 (1486), 36-40.

Keating, P, Garellek, M. na Kreiman, J. (2015). Acoustic Properties of Different Kinds of Creaky Voice.18th International Congress of Phonetic Science. Glasgow: Scotland.

Ladefoged, P. na Gordon, M. (2001). Phonation types: A cross-linguistic Overview. Journal of Phonetics 29, 383-406.

Ladefoged, P. na Johnson. K. (2011). A Course in Phonetics. Boston: Michael Rosenberg.

Lin, W. (2019). Three Modes of Rhetorical Persuation. Sino-US Englsih Teaching 16, 3: 106-112

Mahoney, R. (1993).The Shepherds Staff. Burbank: World Map Publishers.

McAlpine, A. (2016). An Examination of Vocal Fry as a Feminine Identity Marker. Academic Excellence Showcase Proceeding 47. https://digitalcommons.wou.edu/eas. Imepakuliwa Juni, 1, 2020.

Møller, H & Pedersen, C.S (2004). Hearing at Low and Infrasonic Frequencies. Noise and Health, 6, 23, 35-57.

Mshvenieradze, T. (2013). Logos, Ethos and Pathos in Political Discourse. Theory and Practice in Language Studies, 3, 11: 1939-1945.

Naeem, M.H., Adleeb, N., Nadvi, N. A., Umar, M., Shabir, S.A. & Shabir, G (2014). Language of Religion. International Journal of Innovation and scientific Research 5, 1: 40-43.

Ndung’u, V. (2001). Uchanganuzi wa Usemi Katika Sajili ya Dini: Sifa Bainifu za Lugha ya

Mahubiri. Tasnifu ya Uzamili, Haijachapishwa. Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Omowumi, A., Soku, D. (2015). Language Craft by Nigerian and Ghanaian Christian Preachers-

What Impact? Double Blind Peer Reviewed International Research Journal (vol. 15)

Podesva, Robert J. na Patrick C. (2015). Voice Quality and Identity. Annual Review of Applied Linguistics 35: 173-194.

Samely, U. (1991). Kedang (Eastern Indonesia), some aspects of its grammar. Hamburg: Helmut Buske Verlag.

Shaw, F. na Crocker, V. (2015). Creaky Voice as a stylistic feature of young American female Speech: An intraspeaker variation study of Scarlet Johanson. Lyfespans & Styles: Undergraduate Working Papers on Intraspeaker Variation, 1: 19-27.

Similly, L. (2012). Make it Happen Preacha: African American Rhetorical Licence, African American Vernacular Englsih (AAVE), and a Modern Rendering of Epideictic Rhetoric. Unpublished PhD Dissertation. University of Texas.

Sorokowski, P., Puts, D., Johnson, J., Zoleklewicz, A., Oleszklewicz, A., Sorokowska, A., Kowal, M., Borokowska, A & Plsanski, K. (2019). Voice of Authority: Professional Lower their Vocal Frequencies when Giving Expert Advice. Journal of Non-Verbal Behavior 43: 257-269.

Smithermann, G. African American Englsih: From the hood to the Amen Corner. Keynot Speech Presented for the Center for Interdisciplinary Studies of Writing 1995 Conference Linguistics Diversity and academic Writing. University of Minnesota.

Taylor, G. C. (1977). How shall They Preach. Elgin.IL: Progressive Baptist Publishing House.

The Bible societies (2008). Holy Bible. Revised Standard: China. Bible Society Resources Limited.

Tumbull, R. (1967). Baker’s Dictionary of Practical Theology. Grand Rapids: Baker Book House.

Waweru, T. W. (2014). Matumizi ya Lugha Katika Kanisa Katoliki: Uchanganuzi wa

Ubadilishaji Msimbo Katika Mahubiri. Tasnifu ya Uzamili Haijachapishwa. Chuo Kikuu

cha Nairobi.

Wolk, L., Abdelli-Beruh, N na Slavin, D. (2012). Habitual use of Vocal Fry in Young Adult Female Speakers. Journal of Voice, 26(3), 111-116.

Yuasa, I. P. 2010. Creaky Voice: A New Feminine Voice Quality for Young Urban-oriented Upwardly Mobile American Women? American Speech 85:315-337.

Tarehe ya Uchapishaji
10 April, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Nyambura, T., & Githinji, P. (2023). Baadhi Ya Sifa Za Sauti Zoloto Zinazotumiwa Na Baadhi Ya Wahubiri Wa Kipentekosti Kuwasilisha Injili Na Umuhimu Wake. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 68-83. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1166