Athari Ya Viarudhi Vya Ekegusii Kwa Kiimbo Cha Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Upili.

  • Christine Nyougo Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Peter Githinji, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Lugha ya kwanza, Lugha ya pili, Trokee, Wizani silabi, Uhawilisho, Viarudhi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inadhamiria kuonyesha athari ya viarudhi vya Ekegusii kwa matumizi ya kiimbo cha Kiswahili sanifu. Wasailiwa wetu ni wanafunzi wa shule tatu za upili zinazopatikana katika eneo la Kisii. Tulijikita katika nadharia ya Mennen (2015) ya ujifunzaji wa kiimbo katika lugha ya pili. Nadharia hii huchunguza matatizo ambayo wajifunzaji wa lugha ya kwanza hupata wakati wa kujifunza kiimbo cha lugha ya pili. Tumejikita kwa mantiki kuwa mtagusano baina ya lugha moja na nyingine huweza kuibua kufanana au kutofautiana kimatumizi katika uenezaji wa viimbo tofauti. Tumetumia mihimili minne katika uchanganuzi wa data tuliyopata nyanjani. Mhimili wa kimfumo unashughulikia vipengele vya kiarudhi katika lugha husika na usambazaji wake, mhimili wa utekelezaji unashughulikia utaratibu wa namna ambavyo vipengele mbalimbali vya kifonolojia vinavyotekeleza majukumu yavyo katika lugha husika. Mhimili wa ujirudiaji unaangazia kiwango cha matumizi ya vipengele hivi vya fonolojia ambapo lugha hutofautiana katika kiwango cha matumizi ya vipengele vyake na mhimili wa kisemantiki unaoshughuklika maana inayopatikana kutokana na matumizi ya viarudhi husiaka. Usampulishaji wa kimaksudi ulitumiwa katika kuteua wanafunzi wa vidato tofauti katika shule tatu teule na walimu wanaofunza Kiswahili katika shule hizo. Data yetu ilitokana na hojaji, mahojiano usomaji wa sentensi pamoja na kifungu ambacho kilikuwa na aina nne za viimbo ambapo wasailiwa walizisoma kwa sauti. Data ya ziada ilitokana na usomaji wa sentensi nane za Ekegusii zenye kiimbo cha taarifa, swali, amri na mshangao ambazo zilisomwa na walimu wanaozungumza Ekegusii kama lugha ya kwanza katika shule hizo tatu. Uchanganuzi wa data ulifanywa kupitia ufasili wa data ya hojaji, mahojiano na uchunzaji wa kushiriki. Matokeo tuliyopata yalibainisha kuwa uhawilisho wa viarudhi hivi kwa kiwango kikubwa huathiri matumizi sahihi ya kiimbo cha Kiswahili ambapo wasailiwa wa lugha ya kwanza hurudufu baadhi ya vipengele vya lugha hiyo katika kiimbo cha lugha ya pili. Matokeo haya pia yalidhihirisha kuwa maumbo ya silabi katika Ekegusii, shadda, toni na wakaa huathiri matumizi ya kiimbo cha Kiswahili sanifu

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Barlow, A. R. (1960). Studies in Gikuyu Grammar and idioms. Endinburgh: Harvester Wheatshef.

Batibo, H. (2017). Evolution of Tone in Bantu Languages. Linguistic and Literary Broad Research and Innovation, 6(2), 34-40.

Beale-Rivaya, Y. (2022). Ekegusii-Minority or minoritized language and cultures. NEH Distinguished Professor. Texas State University.

Corder, S. (1967). Error Analysis and Interlanguage. Oxford University Press.

Durand, V. (1990). Severe Behavior problems: A functional Training Approach. New York: Guilford press.

Goldsmith, J. (1990). Autosegmental and Metrical Phonology. Oxford: Basil Blackwell.

Hayes, B. (1985) Iambic and Trochaic Rhythm in Stress Rules. Proceedings of the Eleventh Annual Meeting of the Berkeley Linguistics Society, 429-446.

Hubbard, K. (1995). ‘Prenasalised consonants’ and syllable timing: evidence from Runyambo and Luganda. Phonology, 12(2), 235-256.

Hyman, L. M. (1975). Phonology: theory and analysis. (No Title).

Janda, R & Auger, J. (1992). Quantitative evidence, qualitative hypercorrection, sociolinguistic Variables And French speakers' 'eadhaches with english h/Ø. Language & Communicafion 12, 3/4 (195-236).

Khvtisiashvili, T. (2018). Phonological processes, transfer, and markedness. The TESOL encyclopedia of English language teaching, 1-6.

Kihore, Y. M., Massamba, D. P. B., & Msanjila, Y. P. (2003). Sarufi maumbo ya Kiswahili sanifu (SAMAKISA): Sekondari na vyuo. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Komenda, S., Maroko, G.M., & Ndung’u, R.W. (2013). The morphophomemics of vowel compensatory lengthening in Ekegusii. International Journal of Education and Research, 1(9), 1-16

Labov, W. (1966). Hypercorrection by the lower middle class as a factor in linguistic change. Sociolinguistics. The Hague: Mouton, 84(10).

Massamba, D. P. B. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.

Massamba, D. P. B. (2012). Misingi ya Fonolojia. Dar es salaam: TUKI.

Mennen, I. (2004). Bi-directional Interference in the Intonation of Dutch Speakers of Greek. Journal of Phonetics, 32, 543-563.

Mennen, I. (2007). Phonological and phonetic influences in non-native intonation. Non-native prosody: Phonetic descriptions and teaching practice, 53-76.

Mennen, I. (2015). Beyond segments: Towards a L2 intonation learning theory. In Prosody and language in contact: L2 acquisition, attrition, and languages in multilingual situations (pp. 171-188). Berlin, Heidelberg: Springer Berlin Heidelberg.

Mennen, I., Reubold, U., Endes, K., & Mayr, R (2022). Plasticity of native intonation in the L1 of English migrants to Austria. Language, 7(3), 1-27.

Mgullu, R. (1999). Mtalaa wa Isimu: fonetiki, fonolojia na mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publisher

Mgullu, R. (2010). Mtalaa wa Isimu: fonetiki, fonolojia na mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publisher

Mogaka, R. (2009). Fonolojia ya utohozi wa maneno mkopo ya Ekegusii kutoka Kiswahili. Tasnifu isiyochapishwa ya M.A. Chuo kikuu cha Kenyatta.

Mose, E. G. (2020). A morphophonological analysis of borrowed segments in Ekegusii language: An Optimality Perspective. Unpublished PhD thesis, Kenyatta University, Nairobi, Kenya.

Mwaliwa, H. C. (2014). An analysis of the syllable Structure of Standard Kiswahili loanwords from Modern Standard Arabic (Doctoral dissertation).

Nandelenga, H. S. (2015). The Lubukusu syllable structure in optimality theory in Phonology. The international journal of Humanites and Social studies, 3(3), 86-10.

Nash, C. M. (2011). Tone in Ekegusii: A description of nominal and verbal tonology. University of California, Santa Barbara.

Ntihirageza, J. (2001). Quantity Insensitive in Bantu Languages. Unpublished phD Dissertation. University of Chicago.

Obara, J. M. (2014). Uchanganuzi wa makosa yanayofanywa na wanafunzi wazungumzaji wa lugha ya Ekegusii (Doctoral dissertation, University of Nairobi).

Osinde, K. N. (1988). EkeGusii morphophonology: An analysis of the major consonantal processes (Doctoral dissertation, University of NAIROBI).

Park, J. I. (1997). Minimal word effects with special reference to Swahili. Indiana University.

Perlmutter, D. (1995). Phonological quantity and multiple association. The Handbook of Phonological Theory. Oxford: Blackwell, 307-17.

Roach, P. (1983). English phonetics and phonology: A practical course. Cambridge: Cambridge University Press.

Son, J. (2018). Acquisition of Spanish intonation by Native Korean speakers. University of California, Los Angeles.

Vâlcea, C. S. (2020). First language transfer in second language acquisition as a cause for error-making in translations. Diacronia, (11), 1-10. DOI: http://dx.doi.org/10.17684/i11A161en

Welmers, W.E. (1973). African Language structure. Berkeley: University of Califonia Press.

Yip, M. (2002) Tone. Cambridge. Cambridge university press

Tarehe ya Uchapishaji
10 November, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Nyougo, C., & Githinji, P. (2023). Athari Ya Viarudhi Vya Ekegusii Kwa Kiimbo Cha Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Upili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 468-482. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1564