Ukiukaji wa Kanuni Bia za Greenberg katika Miundo ya Tungo Zenye Vihusishi Katika Lugha ya Kiswahili

  • Jemimah Kwamboka Ongwae Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Peter Githinji, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Kanuni bia, Muundo, Vihusishi, Ukiukaji, Taipolojia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yalidhamiria kubaini ukiukaji wa baadhi ya kanuni bia za Greenberg katika miundo ya tungo zenye vihusishi vya Kiswahili. Katika utafiti wake, Greenberg (1963), alipendekeza kanuni bia 45 na kutafiti lugha 30 ili kuchunguza mpangilio wa vipashio vya kiisimu katika makundi mbalimbali ya lugha. Lugha ya Kiswahili ilikuwepo mojawapo ya sampuli alizoteua. Hata hivyo, katika kuzingatia uwekaji vihusishi, inaonekana kukiuka baadhi ya kanuni hizo. Kwa hivyo, mkabala wa Greenberg (1963) ulitumika. Kanuni bia za Greenberg hasa zile zinazozungumzia vihusishi pekee zilitumika kuchanganua miundo na mazingira ya kiisimu yanayosababisha ukiukaji wa baadhi ya kanuni za Greenberg katika uwekaji wa vihusishi vya Kiswahili. Data iliyotumika ilikuwa ni tungo zenye vihusishi. Mbinu ya usampulishaji wa kimakusudi ilitumika kuteua vihusishi hivi na vilikusanywa kwa kusoma vitabu vya sarufi na makala kutoka kwenye majarida na makala ya mtandaoni. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia mkabala wa kanuni bia za Greenberg kupitia ufafanuzi wa data kwa njia ya maelezo na unukuzi wa kanuni bia za Greenberg. Ilijidhihirisha kuwa baadhi ya kanuni bia za Greenberg zina ukiushi katika lugha ya Kiswahili. Ukiushi hasa ulitokea kwa sababu sifa A haikumiliki sifa B kwa kuzingatia sheria ya uchanganuzi iliyopeanwa. Haya yalibainika hasa kwa kuwa lugha ya Kiswahili inamiliki aina mbili za vihusishi; vihusishi vya kabla ya nomino na vihusishi vya baada ya nomino katika umbo lake la nje. Hata hivyo, baadhi ya kanuni bia zingine zilionyesha utiifu. Aidha baadhi ya kanuni hizi zina utata ambao unaleta changamoto katika juhudi za kutoa kauli jumlishi. Makala haya yatachangia katika kongoo ya utaratibu wa vipashio katika sentensi, taipolojia ya lugha na sintaksia ya Kiswahili

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abraham, W., Givón, T., & Thompson, S. A1 (1995). Discourse, Grammar and Typology: Papers in honor of John WM Verhaar (Vol. 27). Amsterdam. John Benjamins Publishing.

Beliavsky, N. (2004). Review of “Metaphor, Culture and World View: The Case of American English and the Chinese Language” by Dilin Liu. Journal of Asian Pacific Communication, 14(2), 355–361.

Bloomfield, A. L. (1933). Language. New York Holt: Rinehart & Winstorn

Dryer, M. S. (1991). SVO languages and the OV: VO typology1. Journal of linguistics, 27(2), 443-482. (Published online) DOI: 10.1017/S0022226700012743.

Greenberg, J. (1963). Some universals of grammar with particular reference to the order of meaningful elements. In J. Greenberg, (Ed). Universals of Language. 73-113. London: MIT Press.

Greenberg, J. H. (1966). Synchronic and diachronic universals in phonology. Language, 42(2), 508-517.

Hockett, C. F. (1961). Linguistic Elements and their Relations. Language, 37(1), 29-53.

Hopper, P. J., & Traugott, E. C. (2003). Grammaticalization. Cambridge: Cambridge University Press.

Huddleston, R. (2000). Introduction to the Grammar of English. Cambridge: Cambridge University Press.

Huddleston, R., & Pullum, G. K. (2002). The Cambridge grammar of the English language. Cambridge, UK: CUP

Katamba, F., & Stonham, J. (2006). Morphology (2nd Edition). New York: Palgrave Macmillan Publishers.

Keenan, E. (1978). Negative Coreference: Generalizing Quantification for Natural Language. Formal Semantics and Pragmatics for Natural Languages, 77-105.

Koopman, H. (2000). Prepositions, postpositions, circumpositions and particles: The structure of Dutch PPs. In H. Koopman (Ed.), The Syntax of Specifiers And Heads, 198-256. London: Routledge.

Kuno, S. (1974). The position of relative clauses and conjuctions. Lingustic Inquiry, 5(1), 117-136.

Lefebvre, C. & Brousseau, A. (2001). A grammer of Longbe. Berlin: Mouton de Gruyter.

Luraghi, S. (2003). On the Meaning of Prepositions and Cases: The Expression of Semantic Roles in Ancient Greek. Amsterdam/Philadelphia: John Benjamins Publishing Company.

O’Dowd, E. M. (1998). Prepositions and Particles in English: A Discourse-functional Account. New York: Oxford University Press.

Riemsdijk, V. H. (2020). A Case Study in Syntactic Markedness: The Binding Nature of Prepositional Phrases (Vol. 4). London: The Peter de Ridder Press.

Tyler, A., & Evans, V. (2003). The Semantics of English Prepositions: Spatial Scenes, Embodied Meaning, and Cognition. Cambridge: Cambridge University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
25 November, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Ongwae, J., & Githinji, P. (2023). Ukiukaji wa Kanuni Bia za Greenberg katika Miundo ya Tungo Zenye Vihusishi Katika Lugha ya Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(2), 30-43. https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1596