Motifu ya Ukame katika Tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015)

  • Mary K. Njeru Chuo Kikuu cha Chuka
  • John M. Kobia, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
  • Dorcas M. Musyimi, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
Keywords: Motifu, Ukame, Uhakiki wa Kiekolojia, Usawiri, Mazingira Asilia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Suala la ukame limeanza kupata umakini mwingi kwa sababu ya kuongezeka kwa hivi karibuni kwa marudio na makali yake. Mathalani, ni mwanzo wa maafa yanayoaminika kuwa chanzo cha kimsingi cha baa la njaa kwa ajili ya uharibifu wa mazao. Kadhalika, ni kutokana na makali ya ukame katika mataifa mbalimbali Barani Afrika na ulimwenguni kwa jumla, ambapo kumeibuka mijadala mizito miongoni mwa washikadau mbalimbali wa masuala ya kimazingira kote ulimwenguni. Tangu kuvumbuliwa kwa uwanja wa fasihi mazingira miaka ya tisini, waandishi wa kifasihi wamejihusisha katika masuala ya kimazingira ili kuchangia katika utatuzi wa matatizo yanayotokana na uharibifu wa mazingira. Kwa msingi huu, makala hii inajadili namna watunzi wa tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015) wamesawiri motifu ya ukame kama suala mojawapo la kimazingira kwa lengo la kuweka wazi chanzo na athari zake katika jamii. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Nadharia hii hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Utafiti ulifanyiwa maktabani ambapo uteuzi wa sampuli wa kimakusudi ulitumiwa kuteua matini teule. Data ya utafiti ilikusanywa kupitia usomaji wa kina wa matini teule. Kutokana na matokeo ya makala hii, ilibainika kwamba, waandishi wa tamthilia teule wamesawiri suala la ukame kwa namna mbalimbali kwa kuangazia chanzo na athari zake. Hivyo, makala hii imethibitisha kwamba, fasihi ya Kiswahili ni nyenzo muhimu ambayo inaweza kutumika katika kuangazia masuala yanayoathiri jamii. Vilevile, utafiti huu ni muhimu kwa washikadau wote wa masuala ya kimazingira Barani Afrika na ulimwengu kwa jumla.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Alia, A. (2017). Ecocritical Post-Colonial Studies on Humans, Land and Animals. Unpublished MA Thesis: University of Nothern Iowa.

Arege, T.M. (2015). Majira ya Utasa. Nairobi: Spotlight Publishers (E.A) Limited.

Assumpta, K. (2011). Fani ya Fasihi Simulizi kwa Shule za Upili. Nairobi: Oxford University Press.

BBC News Swahili (17/07/2021). Mafuriko Ulaya: Wanasayansi Waelezea ni kwa Nini Hawawezi Kutabiri Mafuriko kama yale Yanayozikumba Ujerumani na Ubelgiji. Available at https://www.bbc.com/swahili/habari-7872899. Accessed on 19/12/2021.

Bookchin, M. (1980). Toward an Ecological Society. Montreal: Blackrose Books.

Buell, L. (1995). The Environmental Imagination: Thoreau, Nature Writing and the Formation of American Culture. Cambridge Mass: Harvard University Press.

Buell, L. (2005). The Future of Environmental Criticism: Environmental Crisis and Literary Study. Malden: Malden blackwell Publishers.

Easterlin, N. (2012). A Biocultural Approach to Literary Theory and Interpretation. Baltimore: The John Hopkins University Press.

Curry, P. (2011). Ecological Ethics: An Introduction 2nd Edition. Cambridge, UK&Malden, MA: Polity Press.

Garrard, G. (2007). Ecocriticism and Education for Sustainability. In Pedalogy: Critica Approaches to Teaching Literature, Language, Composition & Culture. Volume 7(3): 359-386. Duke University Press.

Gichure, R.W. (2017). Effects of Drought on Crop Production and Coping Mechanisms Undertaken by Small Scale Farmers: A Case Study of Makueni County, Kenya. Unpublished Masters Thesis (MA). University of Nairobi.

Glotferty, C. (1996). Introduction. The Ecocriticism Reader: Landmarks in Literary Ecology. In Cheryll Glotferty and Harold Fromm. Athens: The University of Georgia Press.

Iheka, C.N. (2015). African Literature and the Environment: A Study in Postcolonial Ecocriticism. Unpublished PhD Thesis: Michigan State University.

Maathai, W. (2006). Unbowed. United States: Alfred A. Knopf.

Maathai, W. (2009). The Challenge for Africa. Britain: William Heineman.

Magharibi, L. (2017). Athari za Ukame. Available at https://sw.eferrit.com/athari-za-ukame: Accessed on 08/12/2021.

Mohamed, S.A. (2011). Janga la Werevu. Nairobi: Longhorn Publishers.

Mulokozi, M. (2017). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili: Kozi za Fasihi Vyuoni na Vyuo Vikuu. Dar es salaam: KAUTTU.

Njiru, H.M. (2015). Eco-Techno-Cosmopolitanism: Education, Inner Change and Practice in the Contemporary U.S. Eco-Disaster Novel. Unpublished PhD Thesis: Miami University.

Public Service International (2020). Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. Available at https://pop-umbrela..s3.amazonaws.com/uploads/105d8e43-efaa-4d91-aba4-f287453c0671_2020_SWAHILI_PSI-ClimateCrisisHandbook-master-web-01-56.pdf: Accessed on 15/12/2021.

Quick, P.S (2004). An Ecocritical Approach to the Southern Novels of Cormac Mccarthy. Unpublished PhD Thesis: University of Georgia.

Riccardo, R. (2017). Ukame-Wikipedia, Kamusi Elezo Huru. Available at https://sw.wikipedia.org/wiki/ukame: Accessed on 18/12/2021.

Rigby, K. (2002). Ecocriticism in Julian Wolfreys (ed) Introducing Criticism in the twenty-first century. Edinburgh: Edinburgh University Press.

Sabula, M., & Sangili, N. (2019). Fasihi Mazingira: Mtazamo wa Kinisai katika Riwaya ya Nakuruto. Koja la Taaluma za Insia. Vol 6(2019), PP 338-354.

Sangili, N. (2015). Nafasi ya Fasihi ya Kiswahili katika Uwanja wa Fasihi Mazingira. CHAKAMA (2015): 73-84.

Shemboko, L. (2020). Matambiko katika Jamii ya Wasambaa. Available at https://www.academia.edu/12037128/Matambiko_Katika_Jamii_yA_Wasambaa. Accessed on 15/12/2021.

Simel, A. (2015). The Effect of Drought and Famine on Agricultural Production, Living Standards and Education, Status of the People of Kitui County, Kenya. Unpublished MA Thesis: University of Nairobi.

Tan, C. (2019). An Ecocritical Study of J.G Ballard`s Climate Fiction Novels. Unpublished PhD Thesis. Pamukkale University.

Turton, A., & Henwood, R. (eds) (2002). Hydropolitics in the Developing World; A Southern Africa Perspective, Africa. Walter issues Research Unit: Pretoria.

UN (2021). Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP26-/Vatican News. Available at https://www.vaticannews.va/sw/pope/news/2021-10/mkutano-umoja-mataifa-mabadiliko-tabianchi-cop26-wito-vatican.html:Accessedon 23/12/2021.

UNEP (2020). Misitu Inapoendelea Kupungua Duniani, Hatua za Dharura Zinahitajika ili Kutunza Bayoanuai yake. Available at https://www.unep.org/habari-na-matukio/toleo-la-habari/ripoti-ya-umoja-wa-mataifa-misitu-inapoendelea-kupungua-duniani: Accessed on 18/12/2021.

Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publications Ltd.

Wanjohi, A. (2010). Effects of Draught in Kenya. KENPRO Publications Online Papers Portal. Available at https://www.kenpro.org/paper/effects-of-draught-in-kenya.htm: Accessed on 19/12/2021.

Tarehe ya Uchapishaji
29 September, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Njeru, M., Kobia, J., & Musyimi, D. (2022). Motifu ya Ukame katika Tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015). Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 183-195. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.733