Usawiri wa Motifu za Kimazingira Katika Tamthilia ya Kiswahili: Tathmini ya Majira ya Utasa (Arege, 2015)

  • Mary K. Njeru Chuo Kikuu cha Chuka
  • John M. Kobia, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
  • Dorcas M. Musyimi, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
Keywords: Usawiri, Motifu, Uhakiki, Tamthilia, Ekolojia, Mazingira asilia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Suala la kuongezeka kwa viwango vya halijoto na mabadiliko ya tabianchi limeibua mijadala ya kitaifa na kimataifa. Kwa msingi huu, kazi mbalimbali za kifasihi zimebuniwa kwa kuangazia uharibifu wa mazingira asilia na athari zake na mwito wa kuhifadhi mazingira.  Makala hii ilikusudia kuchunguza jinsi motifu za kimazingira zilivyosawiriwa katika tamthilia ya Majira ya Utasa (Arege, 2015). Msisitizo ulikuwa kuangazia jinsi mwandishi wa tamthilia teule amesawiri motifu za kimazingira ili kuonyesha uharibifu wa mazingira pamoja na matatizo yanayotokana na uharibifu huo. Hii ni kwa sababu fasihi huwasilisha hali, maingiliano na mikinzano miongoni mwa binadamu na mazingira. Kwa hivyo, ni mojawapo ya nyenzo inayoweza kuchangia katika kuangazia matatizo yanayokumba jamii yoyote iwayo. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Kimsingi, nadharia ya uhakiki wa kiekolojia hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Tamthilia iliyohakikiwa iliteuliwa kimakusudi kwa kuwa maudhui yake makuu yanahusiana moja kwa moja na mada ya makala hii. Ukusanyaji wa data ulifanywa kupitia usomaji wa kina wa tamthilia teule. Matokeo ya makala hii yalithibitisha kuwa mwandishi wa tamthilia ya Majira ya Utasa amesawiri motifu za kimazingira kwa namna mbalimbali kwa kuonyesha njia za uharibifu wa mazingira na athari zake. Hivyo, kushadidia kuwa fasihi inaakisi kikamilifu matatizo yanayoibuka katika jamii ilimoibuka. Kwa hivyo, ni chombo madhubuti kinachoweza kutumiwa kutatua matatizo hayo.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Arege, T.M. (2015). Majira ya Utasa. Nairobi: Spotlight Publishers (E.A) Limited.

Barry, P. (2013). Beginning Theory: An Introduction to Literary and Cultural Theory. Manchester: Manchester University Press.

Buell, L. (2005). The Future of Environmental Criticism: Environmental Crisis and Literary Study. Maldenblackwell Publishers.

Bulaya, J &Mhango, P (2020). Ujitokezaji wa Maudhui ya Utunzaji wa Mazingira katika Hadithi Teule za Watoto: Mifano kutoka Fasihi ya Kiswahili. Mulika no. (38) pp105-125

Garrard, G. (2004). Ecocriticism. Oxfordshire: Routledge.

Glotfelty, C. & Fromm, H. (1996). The Ecocriticism Reader: Landmark in Literary Ecology. Georgia: University of Georgia Press.

Glotferty, C. (1996). Introduction. The Ecocriticism Reader: Landmarks in Literary Ecology. Katika Cheryll Glotferty and Harold Fromm. Athens: The University of Georgia Press.

Heise, K. U. (2008). Ecocriticism and the Transnatinal turn in American Studies. American Literary History 20(1-2), 381-404.

Idhaa ya Kiswahili (09/09/2021). Rais Kenyatta Atangaza Ukame kuwa Janga la Kitaifa Nchini Kenya. Available at https:/www.google.com/amp/s/amp.dw.com/sw/rais-kenyatta-atangaza-ukame-kuwa-janga-la-kitaifa-kenya/a-59131925: accessed on 05/10/2021.

Maathai, W. (2009). The Challenge for Africa. Britain: William Heineman.

Maganga, A. G. (2019). Umuhimu wa Maji katika Maisha ya Mwanadamu. Available at http://alexmaganga.blogspot.com/2019/02/umuhimu-wa-maji-katika-maisha-ya-.html?m=1: accessed on 03/10/2021.

Matheka, B. (2018). Hatari Nchi kugeuzwa Jangwa Kufuatia Ukataji wa Miti Kiholele. Available at https://taifaleo.nation.co.ke/?p=2630: Accessed on 05/10/2021.

Mulokozi, M. (2017). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili: Kozi za Fasihi Vyuoni na Vyuo Vikuu. Dar es salaam: KAUTTU.

Mutua, P. (2020). “Conserve Environment to Avoid Pandemics”. Daily Nation, page 18: 02/09/2020.

Rigby, K. (2002). Ecocriticism in Julian Wolfreys (ed) Introducing Criticism in the twenty-first century. Edinburgh: Edinburgh University Press.

Rueckert, W. (1978). Literature and Ecology: An Experimentin Ecocriticism. Athens: University of Georgia Press.

Sabula, M na Sangili, N. (2019). Fasihi Mazingira: Mtazamo wa Kinisai katika Riwaya ya Nakuruto. Koja la Taaluma za Insia. 6(2019): 338-354. Wesonga, E et al (2020). Nafasi ya Fasihi katika Kuwasilisha Masuala ya Mazingira Kupitia Riwaya Teule za K. W. Wamitila. East African Journal of Swahili Studies. 2 (2020): 2707-3467.

Ojomo, P. A. (2011). Environmental Ethics: An African understanding in the Journal of Pan African Studies, vol 4(3), march 2011.

Omar, F. (2017). Uchafuzi wa Mazingira ni Hatari kuliko Vita na Baa la Njaa. Available at https:www.dw.com/sw/uchafuzi-wa-mazingira-ni-hatari-kuliko-vita-na-baa-la-njaa-utafiti/a-41051751. Accessed on 03/10/2121.

Sangili, N. (2015). Nafasi ya fasihi ya Kiswahili katika uwanja wa fasihi mazingira. CHAKAMA (2015):73-84.

Sera ya Kitaifa ya Mazingira (2012). Toleo Maarufu ya Sera ya Kitaifa ya Mazingira. Nairobi: The International Development Institute-Africa (IDIA)

VOA (05/10/2021). Maafa ya Ukame na Njaa. Available https://www.voaswahili.com/maafa-ya-ukame-na-njaa. Accessed on 05/10/2021.

Wesonga, E. et al (2020). Nafasi ya Fasihi katika Kuwasilisha Masuala ya Mazingira Kupitia Riwaya Teule za K. W. Wamitila. East African Journal of Swahili Studies. 2 (2020): 2707-3467.

Wikipedia (2018). Ukame. Available at https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Ukame: Accessed on 30/09/2021.

Tarehe ya Uchapishaji
10 June, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Njeru, M., Kobia, J., & Musyimi, D. (2022). Usawiri wa Motifu za Kimazingira Katika Tamthilia ya Kiswahili: Tathmini ya Majira ya Utasa (Arege, 2015). Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 151-160. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.699