Makosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili

  • Jackson Kimathi Kanake Chuo Kikuu cha Chuka
  • John M. Kobia, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
Keywords: Makosa, Fonolojia, Kiigembe, Ujifunzaji, Kiswahili
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yananuia kuainisha na kuchanganua makosa ya kifonolojia miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Kiigembe katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili. Athari hizo hutokea kwa sababu ya kuingiliana kwa lugha hizi mbili ambazo ni Kiswahili na Kiigembe. Ni kutokana na maingiliano haya ambapo tunapata athari ya Kiigembe katika Kiswahili na athari hizo pia hutegemea miundo ya lugha zinazohusika. Makala haya yameongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Linganuzi. Hii ni nadharia ya ujifunzaji wa lugha ya pili ambayo hulinganisha na kulinganua lugha mbili ili kuonyesha jinsi zinavyofanana na kutofautiana. Data ya makala haya inatokana na sampuli ya wanafunzi mia mbili na arobaini wa shule za upili za kutwa kutoka Kaunti Ndogo ya Igembe Kusini, Kaunti ya Meru nchini Kenya. Utafiti wa nyanjani ulihusisha mahojiano, hojaji, usimuliaji wa hadithi na pia uandishi wa insha. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa kuna tofauti kidogo katika baadhi ya fonimu za lugha ya Kiigembe na ya Kiswahili. Tofauti katika miundo ya lugha hizi mbili imebainika kuwa chanzo cha athari ya Kiigembe inayojitokeza katika lugha ya Kiswahili

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Chimerah, R. (2000). Kiswahili Past Present and Future Horizons. Nairobi University Press, Nairobi.

Ellis, R. (1985). Understanding Second Language Acquisition. Oxford University

James, C. (1980). Contrastive Analysis. Longman, Burnt Mill Harlow.

Lado, R. (1957). Linguistics Across Cultures. The University of Michigan Press, Michigan.

Massamba, D. P. B. na wenzie. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. TUKI, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.

Mbaabu, I. (1985). Kiswahili Lugha ya Taifa. Kenya Literature Bureau, Nairobi.

Mbaabu, I. (1995). Usahihishaji wa Makosa katika Kiswahili. Longhorn Kenya Ltd. Nairobi.

Mudhune, S. (1994). Contrastive Analysis to the Learning of Swahili Morphosyntax by Luo Learners. Unpublished M. A. Thesis, Kenyatta University, Nairobi.

Mukuthuria, M. (2004). Kuathiriana kwa Kiswahili na Kimeru: Mfano kutokana na wanafunzi wa Tigania, Kenya. Unpublished Doctoral Dissertation, Egerton University.

Musau P. M. (1993). Aspects of Interphonology: The study of Kenya Learners of Swahili. Bayreuth African Study.

Norrish, J. (1983). Language Learners and Their Errors. Macmillan Publishers. London.

Onyango, J. O. (1997). Uziada wa Kisarufi katika Kiswahili cha Wanafunzi wa Kinyala: Mtazamo wa Uchanganuzi Linganuzi. Unpublished M. A. Thesis, Kenyatta University, Nairobi.

Van Els, T. (1994). Applied Linguistics and the Learning and Teaching of Foreign Languages. London: Edward Anorld.

Wilkins, D. A. (1972). Linguistics in Language Teaching. Edward Arnold, Bedford Square, London.

Tarehe ya Uchapishaji
10 April, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Kanake, J., & Kobia, J. (2023). Makosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 40-48. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1153