Mapokeo ya Utenzi wa Mwana Kupona katika Upya wa Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi wa Adili’

  • Gladys Kinara Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Pamela Muhadia Yalwala Ngugi, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Richard Makhanu Wafula, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Utenzi, Mwana Kupona, Upya, Shaaban Robert, Utenzi wa Hati, Utenzi wa Adili
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inalenga kuchunguza mapokeo ya Utenzi wa Mwana Kupona katika upya wa tenzi za Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi wa Adili’ Robert (1967). Mapokeo yanaweza kuelezwa kama mila, desturi, fikra na hisia za kihistoria zinazohusu mtazamo sio tu wa yaliyopita zamani lakini pia uwepo wa mambo ya kihistoria na ya sasa kwa lengo la kuyapitisha kwa jamii (Sangi na wengine, 2012). Uchambuzi wa kazi hii umeegemezwa katika mihimili ya nadharia ya Bakhtin (1981) inayoshikilia kwamba lugha huwa na nguvu za Kani Kitovu na Kani Pewa. Kiwango cha Kani Kitovu huhusu nguvu za kisheria zinazotambulisha lugha. Hizi ni sheria za kisarufi na hazibadiliki. Katika muktadha wa fasihi, nguvu hizi zinawakilisha utamaduni wa jamii ambao daima unabaki kurithishwa na kufuatwa kama kanuni. Kiwango cha Kani Pewa nacho kinatokana na matumizi ya lugha katika jamii yanayobadilika kiwakati na yanatofautisha taaluma, tabaka na matumizi mengine ya lugha katika jamii. Nguvu za Kani Pewa zinajaribu kusukuma vipengele vya lugha kutoka katikati na kupelekea kuwa na wingi. Katika kiwango cha fasihi, nguvu za Kani Kitovu zinawakilisha utamaduni wa jamii ambao daima unabaki kurithishwa na kufuatwa kama kanuni. Kwa upande mwingine, kiwango cha Kani Pewa kinatokana na matumizi ya lugha katika jamii yanayobadilika kiwakati na yanayotofautisha taaluma, tabaka na matumizi mengine ya lugha katika jamii. Nguvu za Kani Pewa zinajaribu kusukuma vipengele vya lugha kutoka katikati na kupelekea kuwa na wingi. Katika kiwango cha fasihi, nguvu za Kani Pewa zinawakilisha upya na katika muktadha huu Utenzi wa Mwana Kupona katika tenzi za Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi wa Adili’. Utafiti ulikuwa wa kimaelezo na ulifanywa maktabani na nyanjani. Sampuli ya maktabani na nyanjani iliteuliwa kimakusudi. Maktabani, mtafiti alisoma kwa kina matini iliyochapishwa kwa lengo la kupata data ya msingi. Nyanjani, mtafiti alifanya mahojiano na majadiliano na wanajamii walioteuliwa katika kukusanya data. Data kutoka katika tenzi zilizoteuliwa, maandishi yaliyohusu utafiti, data ya nyanjani zilichambuliwa kulingana na lengo la makala haya na mihimili ya nadharia kwa lengo la kuonyesha namna mapokeo ya Utenzi wa Mwana Kupona yalivyobainika katika upya wa maandishi ya tenzi za Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na’ Utenzi wa Adili’. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kwamba Shaaban Robert (1967) katika kuandika ‘Utenzi wa Hati’ na’ Utenzi wa Adili’ aliazima pakubwa kutoka katika Utenzi wa Mwana Kupona mbali na kuongeza upya  kwa mujibu wa hali ya kijamii ya wakati wake

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Achebe, C. (1994). Things Fall Apart. New York: Anchor Books.

Allen, J. W. T. (1971). Tendi. Nairobi: Heinemann.

Bakhtin, M. (1981). Discourse in the Novel. Modern Literary Theory. 4th Edition. London: Routledge.

Beja, S. K. na Mwinyifaki, A. (2013). ‘Iktibasi’ katika Tenzi za Mwanakupona na Al-Inkishafi. Kioo cha Lugha, 11(1), 30-46. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Biersteker, A. (1991). “Language, Poetry and Power: A Reconstruction of ‘Utendi wa Mwana Kupona.’ In Harrow, K. W. (Ed.), ‘Faces of Islam in African Literature’. pp 37-58. London: James Currey.

El-Maawy, A. A. A. (2011). Jawabu la Mwana Kupona. Dar es Saalam: Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. Dar es Salaam.

Gakuo, J. K. (1996). Fani Katika Utenzi wa Vita vya Uhuru. Tasnifu ya Uzamili. Eldoret: Chuo Kikuu cha Moi. (Haijachapishwa).

Gibbe, A. G. (1995). Inkishafi: Uhakiki wa Kidayakronia. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Moi. Eldoret. (Haijachapishwa).

Gwakee, J., Timammy, R. na Mogambi, H. (2017). ‘A comparative Analysis of Virtue- Based Content for Youth in Two Epics in Swahili: Siraji and Adili’. International Journal of Languages and Linguistics. 4, 4.

Hardy, T. (2015). The Mayor of Casterbridge. Tustin: Xist Publishing.

Hirschkop, K. & Shepherd, D. (Eds.). (2001). Bakhtin and cultural theory. Oxford: Oxford University Press.

Holquist, M. (2002). Dialogism: Bakhtin and His World. London: Routledge.

Kehinde, A. (2003). ‘Intertextuality and Contemporary African Novel’. In Nordic Journal of African Studies. 12(3): 372-386. Uppsala: The Nordic Africa Institute.

Khatib, M. S. (1985). ‘Utenzi wa Mwana Kupona’ katika Mulika. Na. 17: 46-52. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Maina, V. (2005). Nafasi ya Mwanamke Katika Tenzi Mbili za Shaaban Robert. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Mbaabu, I. (1985). Utamaduni wa Waswahili. Nairobi: Kenya Publishing and Book Marketing Co. LTD.

Mdee, J. S., Njogu, K. & Shafi, A. (2011). Kamusi ya Karne ya Ishirini na Moja. Nairobi: Longhorn.

Mohamed, F. A. (2016). Kuchunguza Mila na Desturi za Mwanamke wa Visiwani Pamoja na Fani katika Tenzi za Howani na Mwana Kukuwa. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. (Haijachapishwa).

Momanyi, C. (1998). Usawiri wa Mwanamke Muislamu Katika Jamii ya Waswahili kama Inavyobainika Katika Ushairi wa Kiswahili. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Momanyi, C. (2007). ‘Patriachal Symbolic Order: The Syllables of Power as Accentuated in Waswahili Poetry.’ In The Journal of Pan African Studies, 1, 8.

Mulokozi, M. M. (1999). Tenzi Tatu za Kale. Dar-es-salaam: TUKI.

Mulokozi, M. M. & Sengo, T. S. (1995). History of Kiswahili Poetry, AD 1000-2000: a Report. Institute of Kiswahili Research. University of Dar es Salaam

Munyole, S. D. (2017). Usomaji na Ufasiri Sasa wa Utenzi wa Mwana Kupona. Chuo kikuu cha Kenyatta. Tasnifu ya Uzamili (Haijachapishwa).

Ndulute, C. L. (1987). Shaaban Robert's Poetic Landscape: From Ethnicism to Nationalism' Kiswahili. Vol. 54, No. 1/2, pp. 92-116. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Njozi, H. M. (1990). Utendi wa Mwana Kupona and Reception Aesthetics. Kiswahili, 57, 55-67.

Okwena, S. (2019). Umahuluti wa Miundo Katika Tamthilia za Ebrahim Hussein. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Robert, S. (1967). Maisha yangu na Baada ya Miaka Hamsini. Dar es Salaam: Thomas Nelson and Sons Ltd.

Sangi, M. K. et. al. (2012). ‘T. S. Eliot and the Concept of Literary Tradition and the Importance of Allusions’. International Journal of Science and Research.1, I, 3. India: American Association for the Advancement of science.

Strobel, M. (1979). Muslim Women in Mombasa. 1890-1975. New Haven and London: Yale University Press.

Swaleh A. (1992). Maudhui Katika Utenzi wa Mwana Kupona. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Timammy, R. na Swaleh, A. (2013). ‘A Thematic Analysis of Utendi wa Mwana Kupona: A Swahili Islamic Perspective’ In Journal of Education and Practice. 4, 28.

Wamitila, K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi. Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publication Limited.

Wamitila, K. W. (2003). Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi. Nairobi: Focus Publications.

Wandera, S. P. (1996). “Usawiri wa Mwana Kupona Katika Ushairi wa Kiswahili: 1800-1900; Uhalisi au Ugandamizwaji? Tasnifu ya Uzamili; Chuo Kikuu cha Egerton. (Haijachapishwa).

Watuha, A. I. (2011). Maudhui ya Waadhi katika Utenzi wa Adili. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Tarehe ya Uchapishaji
11 July, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Kinara, G., Ngugi, P., & Wafula, R. (2024). Mapokeo ya Utenzi wa Mwana Kupona katika Upya wa Shaaban Robert: ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi wa Adili’. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 319-331. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2043