Hali ya Kipindi cha Kupigania Uhuru na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili Kati ya Miaka 1930 Hadi 1960 Nchini Tanzania

  • Helina Wanjiku Njuguna Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Geoffrey Kitula King’ei, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Richard Makhanu Wafula, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Uhuru, Ukoloni, Ushairi, Mabadiliko, Ubunifu, Maudhui, Utegemezi, Ubidhaaishaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inachunguza jinsi hali ya kipindi cha kupigania uhuru ilivyochochea mabadiliko ya kimaudhui ya ushairi wa Kiswahili kati ya miaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania. Kulingana na makala hii hali ni matukio mahsusi yanayoathiri ubunifu wa maudhui ya ushairi. Ili kukuza mjadala wetu, makala hii imezingatia kipindi cha kupigania uhuru nchini Tanganyika. Uchunguzi unazingatia mashairi teule kutoka diwani za watunzi wafuatao: Mathias Mnyampala, “Diwani ya Mnyampala (1965)”, Amri Abedi, “Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri (1954)”,  Akilimali Snow-White, “Diwani ya Akilimali (1963)”, Shaaban Robert , “ Koja la Lugha (1969), Pambo la Lugha (1966), Kielezo cha Fasili (1968), na Masomo Yenye Adili (1967)”, na Saadani Kandoro, “Mashairi ya Saadani, (1966)”. Mashairi yaliyoteuliwa yanasomwa na kuhakikiwa ili kubainisha maudhui yaliyomo. Uchanganuzi wa data unaongozwa na mihimili ya Nadharia ya Utegemezi na Nadharia ya Ubidhaaishaji wa Lugha. Katika mashairi teule, inabainishwa kuwa washairi walishiriki katika siasa. Vyama vya kisiasa vilitumia Kiswahili kama chombo cha kuunganisha Watanganyika kisiasa. Mashairi yaliandikwa katika magazeti ili kuhamasisha na kuzindua watu wapiganie uhuru. Mashairi yalibeba maudhui ya dhuluma za kikoloni, utetezi wa haki, umoja wa Waafrika, uzalendo, chama cha TANU, uhuru, sifa za viongozi bora, madaraka na utamaduni wa Waafrika

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abedi, K. (1954). Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Nairobi: East African Literature Bureau.

Akilimali, K. (1963). Diwani ya Akilimali. Nairobi: East African Literature Bureau.

Bienen, H. (1970). Tanzania: Party Transformation and Economic Development. Princeton, New Jersey: Princeton University Press.

Bourdieu, P. (1991). Language and Symbolic Power. Harvard University Press: United States

Chachage, C. (2003). Globalisation ana Democracy Governance in Tanzania. In Development Policy Management Forum (www). http://www.dpmf.org/publications/occassional%20papers/occasionalpaper10.pdf

Chiragdin, S., na Mnyampala, M. (1977). Historia ya Kiswahili. Nairobi: Oxford University Press.

Clarke, P. (1960). A Short History of Tanganyika: Mainland of Tanzania. Tanzania: Longman.

Kandoro, S. (1966). Mashairi ya Saadani. Dar es Salaam: Mwananchi Publishing Limited.

Kezilahabi, E. (1983). Uchunguzi katika Ushairi wa Kiswahili. Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili III: Fasihi. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

King’ei, K., na Kemoli, A. (2001). Taaluma ya Ushairi. Nairobi: Acacia Stantex.

Knappert, J. (1979). Four Centuries of Swahili: A Literary History and Anthology. London: Heinemann.

Massamba, D. Kihore, Y. na Hokororo, J. (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA) Sekondari na Vyuo. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

Massamba, D. P. B. (1995). Kiswahili kama Lugha ya Mawasiliano. Kiswahili katika Kanda ya Afrika ya Mashariki. Dar es Salaam: Institute of Kiswahili Research, 1-11.

Mbaabu, I. (1985). New Horizons in Kiswahili: A Synthesis in Developments, Research and Literature. Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Mnyampala, M. (1965). Diwani ya Mnyampala. Nairobi: Kenya Literature Bureau

Mulokozi, M., & Sengo, T. (1995). History of Kiswahili Poetry A.D1000-2000: A Report. University of Dar es Salaam: Institute of Kiswahili Research.

Ngugi, T. (1986). Decolonising the Mind: The Politics of Language in African Literature. Nairobi: East African Educational Publishers.

Robert, S. (1966). Pambo la Lugha. Nairobi: Oxford University Press.

Robert, S. (1967). Masomo Yenye Adili. Nairobi: Nelson.

Robert, S. (1968). Kielezo cha Fasili. Nairobi: Nelson.

Robert, S. (1969). Koja la Lugha. Nairobi: Oxford University Press.

Rubagumya, C. (1990). Language in Education in Africa: A Tanzanian Perspective. Clevedon. Philadelphia: Multilingual Matters Limited.

Senkoro, F. (1988).Ushairi: Tahakiki na Nadharia. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.

Wafula, R., na Njogu, K. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation.

Were, G., & Wilson, D. (1968). East Africa through a Thousand Years: AD 1000 to the Present Day. London: Evans Brothers Limited.

Whiteley, W. (1969). Swahili: The Rise of a National Language. London: Methuen.

Tarehe ya Uchapishaji
6 March, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Njuguna, H., King’ei, G., & Wafula, R. (2024). Hali ya Kipindi cha Kupigania Uhuru na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili Kati ya Miaka 1930 Hadi 1960 Nchini Tanzania. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 124-136. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1804