Mchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi Katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya Kufa Kuzikana

  • Simiyu Benson Sululu chuo kikuu cha kenyatta
  • Richard Makhanu Wafula, PhD chuo kikuu cha kenyatta
  • Joseph Nyehita Maitaria, PhD chuo kikuu cha kenyatta
Keywords: Waswahili, Fasihi Simulizi, Tanzu za Kimaigizo, Riwaya ya Kiswahili, Umahuluti
Sambaza Makala:

Ikisiri

Usomaji wa fasihi katika kipindi cha sasa unabainisha idadi kubwa ya waandishi kutoka jamii zisizo Waswahili ambao wameandika kazi katika tanzu mahsusi za fasihi simulizi ya Kiswahili. Waandishi hawa wameendelea kutumia maudhui, ploti na vipengele vingine vya utamaduni wa fasihi simulizi za jamii zao katika kubuni kazi zao za fasihi andishi ya Kiswahili. Vipengele vya fasihi simulizi za jamii za waandishi hawa, wasiokuwa Waswahili, vimeingizwa katika riwaya ya Kiswahili na kuwa sehemu ya riwaya hii. Makala hii imechunguza jinsi uingizaji wa vipengele hivi vya fasihi simulizi za watunzi wa riwaya ya Kiswahili, wasiokuwa Waswahili, unaifanya riwaya hii kuwa ya kimahuluti. Mahsusi, makala hii imedadavua mchango wa tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi katika umahuluti wa riwaya ya Kiswahili kupitia mfano wa riwaya ya Kufa Kuzikana (2003) iliyoandikwa na Ken Walibora. Tathmini hii imetumia Nadharia ya Umahuluti wa Utamaduni inayoshikilia kwamba panapotokea hali ya mtagusano baina ya tamaduni tofauti, matokeo yake si wingi-tamaduni bali ni mchanganyiko wa vipengele kutoka tamaduni hizi mbalimbali ambao ni bora na imara zaidi kuliko tamaduni asilia. Nadharia hii imetumiwa kufafanua jinsi umahuluti wa riwaya ya Kiswahili umechangiwa na uingizaji wa vipengele vya tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi kutoka jamii za watunzi wake teule wasiokuwa Waswahili. Katika kufanya hivyo, makala hii imebainisha jinsi kuingizwa kwa vipengele hivi vya fasihi simulizi za jamii za waandishi teule katika riwaya ya Kiswahili kumeirutubisha riwaya hii kwa kuifanya kuwa changamano na nyumbufu kwa ambavyo inameza tanzu kutoka tamaduni tofauti na kujiimarisha kupitia kwazo bila kupoteza sura yake asilia.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Ashcroft, B., Giffiths, G. & Tiffin, H. (2004). The Empire Writes Back: Theory and Practice in Post- Colonial Literatures. (2nd Edition). New York: Routledge.

Bhabha, H. K. (1994). The Location of Culture. New York: Routledge.

Dundes, A. (1965). The Study of Folklore. Englewood Cliffs, N. J: Prentice-Hall, Inc.

Jwan, J. O. & Ong’ondo, C. O. (2011). Qualitative Research: An Introduction to Principles and Techniques. Eldoret: Moi University Press.

Khamalwa, J. P. W. (2004). Identity, Power, and Culture: Imbalu Initiation Ritual Among the Bamasaba of Uganda. Bayreuth: Bayreuth African Studies Series.

Kothari, C. R. (2004). Research Methodology: Methods and Techniques (2nd Revised Edition). New Delhi: New Age International (P) Limited, Publishers.

Kraidy, M. (2005). Hybridity or the Cultural Logic of Globalization. Philadelphia: Temple.

Maritim, E. (2012). ‘The Concept and Nature of Drama and Theatre in Traditional African Societies.’ in: African Drama & Theatre A Criticism. Nairobi: Focus Publishers Ltd.

Mason, J. (2002). Qualitative Research (2ndEdition). London: SAGE Publications.

Mohamed, S. A. (2001). Babu Alipofufuka. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Nandwa, J. & Bukenya, A. (1983). African Oral Literature for Schools. Nairobi: Longman Kenya.

Okpewho, I. (1992). African Oral Literature: Backgrounds, Character, and Continuity. Bloomington, IN: Indiana University Press.

Okwena, S. (2019). “Umahuluti wa Miundo katika Tamthilia za Ibrahim Hussein”. Tasnifu ya Uzamifu, Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Raab, J. & Buttler, M. (2008). Hybrid Americas: Contracts, Contrasts and Conferences in New World Literatures and Cultures. Verlag. Tempe: Bilingual Press.

Robert, S. (1952). Adili na Nduguze. London & Basingtoke: Macmillan Publishers.

Rosaldo, R. (1995). “Foreword” in: Hybrid Cultures: Strategies for Entering and Leaving Modernity (Nestor Garcia Canclini). Tafsiri: Chiappari, C.L & Lopez, S.L. Minneapolis: University of Minnesota Press.

Wafula, R. M. (2008). ‘Performing Identity in Kiswahili Literature’ in: Culture, Performance & Identity (ed. Kimani Njogu). Nairobi: Twaweza Communications.

Walibora, K. (2003). Kufa Kuzikana. Nairobi: Longhorn Publishers (Kenya) Ltd.

Wamitila, K. W. (2002). Bin-Adamu. Nairobi: Phoenix Publishers.

Wanjala, F. S. (2020). Safina ya Utafiti wa Fasihi Simulizi. Kakamega: Elgon Epitome Publishers Limited.

Were, W. (2014). “A Traditional Ritual Ceremony as Edurama: A Case Study of Imbalu Ritual Among the Babukusu of Western Kenya”. PhD Thesis, Kenyatta University. (Unpublished).

Tarehe ya Uchapishaji
2 Agosti, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Sululu, S., Wafula, R., & Maitaria, J. (2021). Mchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi Katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya Kufa Kuzikana. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 3(1), 91-99. https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.373