Dhima ya Usimulizi Katika Uwasilishaji wa Nyimbo za Taarab: Uchunguzi wa Kipengele cha Wakati

  • Dorcas Misoi Chuo Kikuu Cha Kenyatta
  • Richard Makhanu Wafula, PhD Chuo Kikuu Cha Kenyatta
Keywords: Taarab, Mutribu, Naratolojia, Usimuliaji, Simulizi, Analepsia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Taarab ni aina ya nyimbo yenye asili katika Pwani ya Afrika Mashariki. Nyimbo hizi kama zilivyo nyimbo zingine, ni zao la shughuli na hisia za binadamu. Hivyo, ujumbe katika nyimbo hizo hujikita katika miktadha mbalimbali ya jamii. Ntarangwi (2001) anasema, mbali na kuwa nyimbo za taarab huimbwa sana katika harusi za Waswahili, nyingi ya nyimbo hizo hugusia masuala mengine ya maisha kama vile uongozi, dini, urembo wa wanawake, mabadiliko ya kisiasa au hata kuhusu uchungu wa kumpoteza mpenzi. Masuala haya huwasilishwa na watribu kwa kutumia mbinu za lugha kwa ubunifu wa kiwango cha juu. Makala haya yamechunguza dhima ya usimulizi katika uwasilishaji wa nyimbo za taarab kwa kuzingatia kipengele mahsusi cha wakati. Kazi hii imeongozwa na nadharia ya naratolojia inayohusishwa na mwanafalsafa wa Kiyunani aitwaye Plato na kuendelezwa na wataalamu kama vile Genette, Stanzel, Manfred Jan na Mieke Bal. Nadharia hii inahusu usimuliaji wa hadithi. Misingi yake ni kuwa usimulizi lazima uwe na msimulizi, kitendo kinachosimuliwa, usemi kuhusu kinachofanyika, wahusika na dhamira ya usimulizi wowote hubainika kupitia kwa mtazamo wa msimulizi. Kipengele cha usimulizi cha wakati kimetumiwa kuonyesha dhima ya usimulizi katika uwasilishaji wa maudhui na mtindo wa uwasilishi katika nyimbo za taarab. Katika kufanya hivyo, makala haya yamebainisha kuwa kipengele cha usimulizi cha wakati kimedhihirika katika nyimbo teule za taarab na kimechangia kukuza maudhui na mtindo wa uwasilishi kwa kuonyesha kuwa wimbo wa taarab ni utanzu telezi unaosheheni usimulizi

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Arege, T. (2012). Narration in Swahili Narrative Poetry: An Analysis of Utenzi wa Rasi’l Ghuli. Tasnifu ya uzamifu Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Gathogo, E. (2017). Mchango wa Msilimishaji katika Maonyesho ya Filamu: Mfano wa DJ. Afro. Tasnifu ya shahada ya uzamili Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Genette, G. (1972). Narrative Discourse. Ithaca: Cornell University Press.

Kea, P. (2006). Usemezo Katika Nyimbo za Taarab. Tasnifu ya uzamili Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Khamis, S. (2015). Uhakiki wa Usimulizi katika Tamthilia ya Kijiba Cha Moyo na Mstahiki Meya. Tasnifu ya shahada ya uzamili Chuo Kikuu.

King’ei, G. (1992). “Language, Culture and Communication: The Role of Swahili Taarab Songs in Kenya, 1963-1990”. Unpublished Ph. D Dissertation, Howard University.

King’ei, G. (2005). Swahili Taarab: From Tradional Orality to a Globalized Art Form.Lwati. (A Journal of Contemporary Research, Vol. 2, 2005, pp. 1-15): Kenyatta University, Nairobi.

Kisurulia, E.S. (2012). Point of View in the Kiswahili Novel: A Narratology Analysis of selected (Haijachapishwa).

Murimi, J. (2016). Mwingiliano Tanzu Katika Modern Taarabu – Mipasho. Tasnifu ya uzamifu Chuo Kikuu cha Moi. (Haijachapishwa).

Ntarangwi, M. (1998). Taarab Texts, Gender, and Islam in Urban East African Context: Social Transformations among the Waswahili of Mombasa, Kenya. Tasnifu ya uzamifu: University of Illinois at Urbana Champaign. (Haijachapishwa).

Ntarangwi (2001). A Social- historical and Contextual Analysis of Popular Musical Performance Among the Swahili of Mombasa Kenya. Nairobi: Cultural Analysis.

Plato (1930). The Republic, Books 1 to 5 trans. P. Shorey. Cambrigde: Havard University Press.

Ong’ondi, E. (2005). Usimulizi katika riwaya ya Walenisi ya Katama Mkangi. Tasnifu ya uzamili Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Prince, G. (1982). Narratology: The Form and Functioning of Narrative. Berlin: Mouton Publishers.

Rashid, A. (2018). Kuchunguza Dhamira na Fani katika Nyimbo za Taarab Asilia: Mifano ya nyimbo za Shakila Saidi Khamisi. Tasnifu ya uzamili Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. (Haijachapishwa).

Rimmon – Kenan, S. (1983). Narrative Fiction. London: Methuen& Co. Ltd.

Topp, J. (2014). Taarab Music in Zanzibar in the Twentieth Century. London: Ashgate publishing.

Tarehe ya Uchapishaji
10 Juni, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Misoi, D., & Wafula, R. (2022). Dhima ya Usimulizi Katika Uwasilishaji wa Nyimbo za Taarab: Uchunguzi wa Kipengele cha Wakati. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 161-170. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.702