Maongezi Katika Riwaya Za Kiswahili

  • Daniel Kiprugut Ng’etich Chuo Kikuu Cha Kenyatta
  • Richard Makhanu Wafula Chuo Kikuu Cha Kenyatta
  • Joseph Nyehita Maitaria Chuo Kikuu Cha Kenyatta
Keywords: Maongezi, Riwaya ya Kiswahili, Uainishaji, Dhima, Ukuaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inaangazia dhima ya maongezi katika riwaya ya Kiswahili. Riwaya ni mojawapo wa tanzu muhimu za fasihi ya Kiswahili ambayo inaendelea kukua kwa upande wa wahusika, dhamira, maudhui, mtindo na upeo. Utanzu wa riwaya ya Kiswahili ulianza mwanzo wa karne ya ishirini wakati James Juma Mbotela alipoandika riwaya ya Uhuru wa Watumwa (1934). Ukuaji wake umeshika kasi zaidi katika mwongo wa mwisho wa karne ya ishirini na mwanzo wa karne ya ishirini na moja. Ni muhimu pia kutambua kuwa, utungaji wa riwaya umeendelea kukua sambamba na uhakiki wake. Katika karne ya ishirini na moja, riwaya ya Kiswahili imefikia utungaji wa kimajaribio (Mwamzandi, 2013:48-66 na Mohamed 2003:78-79). Katika riwaya za kimajaribio, watunzi hujumuisha nadharia, visasili pamoja na kuzungumzia masuala ya utandawazi na soko huru. Ni riwaya ambazo hukiuka miundo ya riwaya iliyozoeleka. Kwa upande wa maongezi, usemaji wa wahusika katika riwaya umekua kutoka sahili hadi changamano kutokana na masuala yanayojadiliwa katika riwaya mahususi. Ni maoni ya waandishi wa makala hii kuwa, usemaji wa wahusika unaweza kuathirika na vipindi vya kihistoria hivyo basi kuwa na mchango muhimu katika maendeleo ya riwaya. Madhumuni ya makala hii ilikuwa ni kuainisha maongezi katika riwaya za Kiswahili. Riwaya ambazo zilichanganuliwa kwa mujibu wa makala hii ni Kusadikika (1951), Mafuta (1984) na Kufa Kuzikana (2003). Riwaya hizo ziliteuliwa kuwakilisha vipindi mahususi vya ukuaji na maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi wa Usemi Hakiki. Kutokana na uchanganuzi huo, makala hii imebainisha mchango wa maongezi kwa ukuaji, maendeleo na uumbufu wa utanzu wa riwaya kwa ujumla.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bakhtin, M. (1989). The Dialogic Imagination. Austin: University of Texas Press.

Bolinger, D. (2014). Language - The Loaded Weapon: The Use and Abuse of Language Today. London: Routledge.

Celce-Murcia, M. na Olshtain, E. (2000). Discourse and Context in Language Teaching: A Guide for Language Teachers. Cambridge: Cambridge University Press.

Fairclough, N. (1992). Discourse and Social Change. Cambridge, UK: Polity Press.

Haines B. (1991). Dialogue and Narrative Design in the Works of Adalbert Stifter. London: Modern Humanities Research Association.

Hawthorn, J. (1992). Studying the novel: An Introduction. (2nd ed). London: Hodder/ Arnold.

Kezilahabi, E. (1990). Nagona. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.

Mayr, A. na Machin, D. (2012). How to Do Critical Discourse Analysis: A Multimodal Introduction. London: sage.

Mbotela, J.J. (1934). Uhuru wa Watumwa. London: Sheldon Press.

Mkangi, K. (1984). Mafuta. Nairobi: Heinemann Educational Books.

Mohamed, S.A. (2001). Babu Alipofufuka. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Mohamed, S.A. (2003). “Fragmentation, Orality and Magic Realism in Kezilahabi’s Novel Nagona.” Nordic Journal of African Studies, 12(1). 78 – 91.

Mohamed, S.A. (2006). Dunia Yao. Nairobi: Oxford University Press, East Africa Ltd.

Mohamed, S.A. (2007). “Vionjo vya Riwaya Mpya ya Kiswahili.” Kioo cha Lugha, 5(1), 11–17. Retrieved from http://dx.doi.org/10.4314/kcl.v5i1.61424.

Mwamzandi, I. (2013). “Riwaya Teule za Karne ya Ishirini na Moja na Udurusu wa Nadharia za Fasihi.” Swahili Forum, Vol. 20, 48 – 66.

Paltridge, B. (2006). Discourse Analysis: An Introduction. London: Continuum.

Robert, S. (1951). Kusadikika. Nairobi: East African Literature Bureau.

Robert, S. (1952). Adili na Nduguze. London & Basingstoke: Macmillan Publishers.

Robert, S. (1967) Kufikirika. Nairobi: Oxford Universty Press.

Robert, S. (1968). Utubora Mkulima. Nairobi: Evans Brothers Ltd.

Robert, S. (1968). Siku ya Watenzi Wote. Nairobi: Nelson.

Van Dijk, T. (1998). Ideology: a multidisciplinary approach. London: Sage.

Van Dijk, T. (2006). "Ideology and Discourse Analysis." Journal of Political Ideologies 37(2), 115 -140. doi:10.1080/13569310600687908.

Van Leeuwen, T. (2008). Discourse and Practice: New Tools for Critical Discourse Analysis. Oxford: Oxford University Press.

Walibora, K. (2003). Kufa Kuzikana. Nairobi: Longhorn Publishers.

Wamitila, K.W. (2006). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix Publishers.

Wodak, R. (2001). What CDA is about – a summary of its history, important concepts and its developments. Katika R. Wodak and M. Meyer (Wah.) Methods of Critical Discourse Analysis (uk. 1 – 13). London: Sage.

Wodak, R. (2001). The discourse – historical approach. Katika R. Wodak and M. Meyer (Wah.), Methods of Critical Discourse Analysis (uk. 63 – 94). London: Sage.

Tarehe ya Uchapishaji
29 September, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Ng’etich, D., Wafula, R., & Maitaria, J. (2022). Maongezi Katika Riwaya Za Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 224-233. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.781