Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi

  • Karuhanga Deusdedit Chuo Kikuu cha Maseno
  • Florence Ngesa Indede, PhD Chuo Kikuu cha Maseno
Keywords: Ukahaba, Ngono, Kuwadi, Madanguro
Sambaza Makala:

Ikisiri

Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi sana katika maisha ya mwanadamu kama vile kupoteza ujira, uharibikaji wa ndoa, maradhi ya zinaa, vifo, kukata tamaa na utengano miongoni mwa wanajamii. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni: kubainisha usawiri wa ukahaba na wahusika makahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; kuchunguza sababu zinazowalazimu wahusika kufanya ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; na kudhihirisha athari za ukahaba kwa wahusika waliomo katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi.  Mtafiti alitumia nadharia ya utekelezi ambayo ni miongoni mwa nadharia nyingi zenye mtazamo wa kisosholojia. Nadharia ya utekelezi imeendelezwa na wanasosholojia kama vile Talcort Parsons na Emile Durkheim kama wanavyonukuliwa na Worsely Introducing Sociology (1970), huku akisema kwamba ukahaba husababishwa na mambo mawili yaani haja ya kutekeleza mahitaji ya kiuchumi na kwa kukidhi matashi ya nafsi zao kiashki.  Mtafiti pia alitumia nadharia ya umaksi iliyoanzishwa na Karl Marx (1818-1863) na Fredrich Engles(1820-1895).  Nadharia hii hufaa utafiti huu kwa kudhihirisha wahusika wanaoshiriki katika vitendo vya ukahaba kwa ajili ya kupata fedha au zawadi. Mabepari au walionacho huwa na lengo la kuridhisha miili yao tu na wanyonge huwa na lengo la kupata pesa ili kutimiza mahitaji yao, pengine, mnyonge hutolea mwili wake kwa ajili ya kupewa kazi au kupandishwa cheo kazini au kama njia ya kuilinda kazi yake ili asipigwe kalamu. Utafiti huu ni wa maktabani kwa hivyo, maktaba yaliyotumika ni yale ya Chuo Kikuu cha uislamu kilichopo nchini Uganda, Chuo kikuu cha Bishop Stuart Mbarara, na maktabani ya shule ya upili Heritage. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na uchunguzaji wa riwaya teule yaani: ile ya Nyota ya Rehema na ya Ndoto ya Almasi kwa kuzisoma na kuzichambua kwa kina na kuiwasilishwa data kwa mbinu ya kiuthamano. Utafiti huu umebainisha kuwa wahusika hufanya ukahaba ili kupata pesa au kuridhisha matashi ya nafsi zao kiashiki. Utafiti huu utakuwa wa muhimu sana kwa kufunza jamii kwamba kahaba si mwanamke peke yake kama inavyochukuliwa katika baadhi ya jamii bali kahaba ni mtu yeyote awe mwanamume au mwanamke anayeshiririki vitendo vya uzinzi.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bakwesegha, C. (1982). Profiles of Urban Prostitution:A case study from Uganda.Kenya Literature Bureau, Nairobi.

Bakwesigha(1982, uk.11). Relationship between sexuality and Poverty in Kampala Uganda

(Cruickshank: 1958, uk.27),

Carrie A. Miles, ( 2012) Tasnifu ya Ph.D . Mafundisho ya Biblia, Kuhusu Ndoa, Familia na Jinsia Swahili(Kenya)

Finnegan, F. (1979). Poverty and Prostitution

Ken. Walobora. (2006).Ndoto ya Almasi.(Moran East Africa publishers Limited

Kishtainy, K. (1982).The Prostitute in Progressive Aliterature. Alalinson and Busby Ltd:

Kothari, C. R. (2004).Research Methodology: Methods and Techniques. New Age International (P). New Delhi India.

Little, K. (1973). Taswira ya mwanamke mjini. Fasihi ya kiafrika. Cambridge University Press.

Lowry, R.P. (1974).Social Problems: A Critical Analysis of Theories and Public Policy.

Mbilinyi, M. (1983).Mwanamke wa Tanzania:Analytical Bibliography.Motala Crafisika, Sweden.

Mghanga, Uppsala, (1997) Demokrasi na Harakati za Kitabaka

Mohamed, M.S. (1972), KIU. (East African Publishing House). (1976). Nyota ya Rehema. (Oxford University Press).

Muga, E. (1980).Studies in Prostitution: East, West and South Africa, Zaire and Naveda. Kenya Literature Bureau: Nairobi.

Nguma, N. (2001), Taswira ya Mwanamke Jinsi Ilivyochorwa Katika Riwaya ya Kezilahabi. Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Omar, S. (2009), Tanzania Hip Hop Poetry as Popular Literature. (Tasnifu ya uzamili, haijachapishwa) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Peck, J.,& Coyle, M. (1984).How to study Literature, Literary terms and criticisms.Macmillan Limited.

Rose Nancy lowrence(20215). Uchungu wa kujifungua nchini Tanzania

TUKI (2004).Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi: Oxford University Press

Karl Marx (1818-1863) na Fredrich Engles (1820-1895).Theory,beliefs and communism Manifesto

Mdee na wenzake, (2011) Kuendelea kuwa wabunge hadi mahakama itakaposikiliza na kuamua

Mwandawiro Mghanga, Uppsala, (1997 Demokrasi na Harakati za Kitabaka

Rose Nancy lowrence(20215). Uchungu wa kujifungua nchini Tanzania

Wafula na Njogu (2007), Nadharia za uhakiki wa Fasihi Jomo Kenyatta Foundation.

Worsely (1970). The Three Worlds: Culture and World Development. Pinguine Books, Ltd.

Tarehe ya Uchapishaji
1 May, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Deusdedit, K., & Indede, F. (2023). Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 119-131. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1194