Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu

  • Jotham Muyumba Chuo Kikuu Cha Kenyatta
  • David Kihara, PhD Chuo Kikuu Cha Kenyatta
Keywords: Leksimu, KS, S.E.D, Sheng’, Mabanda Jijini Nairobi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchunguzi huu kwa sababu ndio kamusi ya kwanza ya Sheng’ kuwahi kuchapishwa. Licha ya kamusi hii kuchapishwa katika lugha ya Kiingereza ina leksimu za Sheng’ ambazo yafaa kuchunguzwa namna zinavyoathiri Kiswahili sanifu. Lengo la utafiti huu lilikuwa kubainisha maneno yaliyomo kwa Sheng’- English Dictionary na katika Kiswahili sanifu. Nadharia ya utafiti ilikuwa Nadharia ya Fonolojia Boreshi ambayo inapatikana katika mtazamo mpana wa Nadharia Boreshi iliyoasisiwa na Alan Prince na Paul Smolensky (1991). Hii ni nadharia inayochunguza hatua za ukuaji wa msamiati kutoka hali ghafi hadi ukubalifu wake kupitia kwa vizuizi tofauti. Mahali pa utafiti palikuwa maktabani na mtandaoni. Mbinu ya uchunguzi ikawa kupitia kusikiliza na kusoma makala mbalimbali kuhusu mada hii. Data ilikusanywa kupitia kwa kuchunguza maneno na vidahizo vya maneno kutoka kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003). Iliaminika kuwa kamusi hii ingetupa sampuli ya maneno mahsusi ya Sheng’ ambayo muundo wake huathiri matumizi katika Kiswahili sanifu kwenye jamii ya kisasa. Uchanganuzi wa maelezo ulitegemea mtazamo wa Fonolojia Boreshi katika nadharia ya fonolojia inayoangazia sarufi zalishi. Katika mtazamo huu, uambishaji wa maneno uliangaziwa na jinsi uundaji huo hutawaliwa na vizuizi mbalimbali na sheria za fonolojia. Uwasilishaji wa data ulikuwa kupitia kwa maelezo ya kina, michoro na jedwali. Uchunguzi huu ulidhamiria kuchangia usomi wa Kiswahili kwa kuweka wazi athari za Sheng’ katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili kimsamiati. Kadhalika, utafiti huu utawasaidia wanafunzi kuweka mipaka bayana kati ya msimbo wa Sheng’ na lugha ya Kiswahili sanifu.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bosire, M. (2006). Hybrid languages: The Case of Sheng’ State University of New York, Albany.

East African Educational Publishers. (2013). Kamusi Teule ya Kiswahili. Nairobi. EAEP.

Ferrari, A. (2014). Evolution of Sheng’ during the Last Decade. Les Cahiers d’Afrique de l’Est / The East African Review, 49 | 2014, 29-54.

Githiora, C. (2018). Sheng’: Rise of a Kenyan swahili vernacular. London: James Currey.

Jomo Kenyatta Foundation. (2016). Kamusi Elezi ya Kiswahili. Nairobi. JKF.

Kihara, D. (2006). Uchambuzi wa matini: matumizi ya lugha katika sajili ya matatu. Tasnifu ya uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta. Haijachapishwa.

Mugenda, O. na Mugenda, A. (1999). Research Methods. Acts Press.

Mwangi, I. na Mukhwana, A. (2011). Isimu Jamii. Nairobi. Focus.

Ogechi, O. (2005). On Lexicalization in Sheng. Nordic Journal of African Studies 14(3): 334–355

Prince, A. na Smolensky, P. (1991). Optimality theory in phonology. Oxford: Oxford University Press

Taifa Leo. (2021, Juni 22). Dondoo za Hapa na Pale. Gazeti la Taifa Leo. Uk. 12.

Tarehe ya Uchapishaji
29 Septemba, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Muyumba, J., & Kihara, D. (2022). Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 314-329. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.827