Chanzo cha Makosa ya Kiisimu Miongoni mwa Wanafunzi Wanaozungumza Lahaja ya Kigichugu Wanapojifunza Kiswahili Kama Lugha ya Pili

  • Nancy Wanja Njagi Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • David Kihara, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Sintaksia Finyizi, Tafsiri Sisisi, Ujumlishaji Mno, Kishamirishi, Kibainishi, Kipatanishi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kiswahili kimekuwa muhimu sana hata kabla ya ujio wa wakoloni nchini Kenya hasa katika kuendeleza mawasiliano. Kabla ya wakoloni, Kiswahili kilitumika katika maeneo ya Pwani kuendeleza mawasiliano ya kibiashara miongoni mwa wakaazi wa Pwani na Waarabu. Biashara ilipoendelea kunoga na watu kutoka maeneo ya bara kuanza kushiriki katika biashara ya pale pwani, Kiswahili kilienea na matumizi yake yakapanuka. Licha ya kupanuka kimatumizi Kiswahili kimekubwa na changamoto nyingi, mojawapo ikiwa ni kuwepo kwa makosa ya kiisimu hasa kwa wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Hivyo basi utafiti huu ulikusudia kubaini chanzo cha makosa ya kiisimu miongoni mwa wanafunzi hasa wanaozungumza lahaja ya Kigichugu wanapojifunza kiswahili kama lugha ya pili. Uchunguzi huu uliendelezwa nyanjani na maktabani.Nyanjani ulitekelezwa katika shule za sekondari za kutwa katika kaunti ndogo ya Gichugu zilizoteuliwa kwa kutumia mbinu ya sampuli kimaksudi. Wanafunzi walioshiriki katika shule hizi walichaguliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji wa kinasibu pale ambapo walipatiwa nambari kinasibu na waliopata nambari moja hadi sita kuteuliwa. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia hojaji, na masimulizi na kuwasilishwa kupitia majedwali na maelezo. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha kuwa wengi wa wanafunzi katika shule za upili za kutwa katika eneo la Gichugu hujifunza Kigichugu kama lugha yao ya kwanza. Isitoshe, wengi huanza kutumia Kiswahili wanapojiunga na shule. Isitoshe, utafiti huu ulidhihirisha makosa mengi ya kiisimu (yaliyovunja kanuni za nadharia ya Sintaksia Finyizi) yaliyotokana na lahaja ya Kigichugu. Vyanzo vya makosa haya ambavyo vinaegemea kwa kiasi kikubwa kwa L1 ni : uhamishaji wa mifumo ya kiisimu, tafsiri sisisi, na ujumlishaji mno

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Adjer, D. (2003). Core Syntax: A Minimalist Approach. London: Oxford University Press. https://doi.org/10.1515/tlir.2003.014

Chomsky, N. (1995). Categories and transformations. The minimalist program, 219, 394.

Chomsky, N. (2014). The minimalist program. (20th Anniversary ed.). MIT press.

Hwang, K. D. (2011). Language Policy in Kenya With a Special Reference to Education. Asian Journal of African Studies, (30), 113-131.

Karingi, B. (2012). Ufunzaji na ujifunzaji wa vibainishi katika shule za upili Wilayani Kirinyaga. Mtazamo wa sintaksia Finyizi, M.A Thesis,Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Mauti, G. M. (2022). Lugha Katika Katiba Ya Kenya: Ujitokezaji Wake Katika Utangazaji Wa Janga La Uviko-19 (Doctoral dissertation, University of Nairobi).

Mulokozi, M. M. (2018). Makala Elekezi: Kiswahili na Umajumui wa Kiafrika. Mulika Journal, 1(1).

Mwihaki, A. (2007). Minimalist Approach to Kiswahili Syntax. Kiswahili a referred journal, (70) 27.

Njoka, A. (2021, Machi 17). Uchambuzi: Kiswahili kinaweza kuwa Lingua Franka ya dunia. https://www.mwananchi.co.tz/mw/kolamu/uchambuzi-kiswahili-kinaweza-kuwa-lingua-franka-ya-dunia-3010788.

Norrish, J. (1983). Language Learners and their Errors. London: Macmillan Press.

Radford, A. (1997). Syntax: A Minimalist Introduction.( 1st edition) Cambridge: Cambridge University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
7 May, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Njagi, N., & Kihara, D. (2024). Chanzo cha Makosa ya Kiisimu Miongoni mwa Wanafunzi Wanaozungumza Lahaja ya Kigichugu Wanapojifunza Kiswahili Kama Lugha ya Pili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 212-223. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1912