Makosa ya Kiisimu Yanayofanywa na Wanafunzi Wanaozungumza Lahaja ya Kigichugu Wanapojifunza Kiswahili Kama Lugha ya Pili

  • Nancy Wanja Njagi Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • David Kihara Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Anafora, Harakia, Kanuni, Kisabiki, Sintaksia, Sintaksia Finyizi, Ufungami, Ukategoria, Utarakilishi, Utegemezi Muundo
Sambaza Makala:

Ikisiri

Binadamu wanahitaji lugha ili kuwasiliana na mojawapo ya lugha maarufu ulimwenguni ni Kiswahili. Kiswahili kimetafitiwa na wataalamu wengi ili kutafuta suluhisho la baadhi ya changamoto zinazokumba lugha hii na kuiboresha. Mojawapo ya changamoto na suala ambalo halijatafitiwa na utafiti huu ulikusudia kubaini ni makosa ya kiisimu ya wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili : Uchunguzi kuhusiana na lahaja ya Kigichugu.Utafiti huu ulitumikiza kanuni na mihimili ya nadharia ya Sintaksia Finyizi ili kuweka wazi makosa ya kisintaksia na kisemantiki yanayofanywa na wanagenzi wa Kigichugu wanapojifunza Kiswahili kama L2. Uchunguzi huu uliendelezwa nyanjani na maktabani.Nyanjani ulitekelezwa katika shule za sekondari za kutwa katika kaunti ndogo ya Gichugu kwa sababu ndiko kuna wazungumzaji asilia wa Kigichugu. Katika utafiti huu tulipaswa kuteua shule,na wanafunzi wa kufanyia utafiti. Katika uchaguzi wa shule za kutwa za kufanyia utafiti tulitumia mbinu ya sampuli kimaksudi. Katika uteuzi wa wanafunzi tulitumia usampulishaji wa kinasibu pale ambapo tulipatia wanafunzi nambari kinasibu na kuteua waliopata nambari moja hadi sita. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia hojaji , insha na masimulizi . Data ya utafiti iliwasilishwa kupitia majedwali na maelezo. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha makosa mengi ya kisintaksia na kisemantiki yaliyotokana na lahaja ya Kigichugu. Makosa haya ni kama vile: makosa ya wanafunzi wagichugu katika matumizi ya nomino, vitenzi, vipatanishi, vivumishi, vibainishi, vielezi, vihusishi na vishamirishi. Makosa haya yalipelekea si tu kuibuka kwa muundo wa sentensi usiokubalika(sintaksia) bali hata kuwepo kwa maana, tofauti na iliyokusudiwa na wanafunzi hawa au isiyoeleweka, hivyo basi kuwepo kwa makosa ya kisemantiki (semantiki leksika na semantiki mantiki). Makosa haya yalichanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Sintaksia Finyizi na kudhihirisha ukiukaji wa kanuni za nadharia hii

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Catford, J.C. (1965). Towards a theory of translation. London: Oxford University Press.

Dooley, D. (1984). Social Research Methods. New Jersey: prentice Hall inc.

Fanike, J. (1984). Exceptional Child. London: Oxford University Press.

Kizuka, Y., Oda, K., & Fujii,K. A Hierarchical Model of Braille Reading. In Proceedings of the 23rd Convention of the Japanese Association of Special Education, 1985, 6-7.

Kothari, C. (1985). Research Methodology: Methods and Techniques. Bangalore: New Age International Publishers.

Mwansoko, H. (1996). Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu. Dar es Salaam; TUKI.

Newmark, P. (1981). Approaches to translation. Oxford: Pergamon Press.

Newmark, P. (1988). A Textbook of Translation. Hertfordshire: Prentice Hall Publishers.

Peaco, F. L. (2004). Braille Literacy: Resources for Instruction, Writing Equipment, and Supplies. NLS Reference Circulars. In Library of Congress. Library of Congress. 101 Independence Ave SE, Washington, DC 20540.

Prima (1978). Kiswahili Braille: KIB.

Republic of Kenya. (2010). The constitution of Kenya, 2010. Nairobi: Republic of Kenya.Seleskovitch, D. and Lederer, M. (1984). Translating and interpreting. Paris. Didier.

Travers, R. M. W. (1978). An introduction to educational research. London: Collier-Macmillan.

Tytler, A. (1990). Essay on the Principles of Translation. London. Oxford University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
27 March, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Njagi, N., & Kihara, D. (2024). Makosa ya Kiisimu Yanayofanywa na Wanafunzi Wanaozungumza Lahaja ya Kigichugu Wanapojifunza Kiswahili Kama Lugha ya Pili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 182-192. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1842