Ni Mvit̪a ni Mvita?: Uchanganuzi wa Usuli wa Toponimi za Mitʰaa ya Mambasa, Kenya

  • Mohamed Karama Chuo Kikuu cha Kabianga
Keywords: Mambasa, Mvita, Toponimi, Isimu, Swahili, Mombasa
Sambaza Makala:

Ikisiri

Miji yot̪ʰe ulimwenguni imepawa majina ili kuitambulisha. Majina haya ni hazina ya mapisi na ut̪amad̪uni kuwahusu wakaaji wa miji hiyo. Namna inavoitwa, fasiri na fasili za majina hayo husema mengi kuhusu maana na nyusuli zake. Makala haya yamechunguza toponimi ya baadhi ya mitʰaa ya mji wa Mambasa, Kenya. Madhumuni yalikuwa ni kuchanganuwa nyusuli za majina kwa kubainisha t̪afaut̪i za kimat̪amshi ya majina hayo, kuthibit̪isha kuwa t̪afaut̪i hizi zaleta t̪afaut̪i ya maana ya majina, na kwamba toponimi za mitʰaa hiyo imeelemeya kwelezeya maumbile ya mazingira ya mahali hapo jambo linaloshuhud̪iwa katika jamii nyengine za Kibantu, Kenya. Tulitumiya T̪arat̪ibu za Ulinganisho na Toponimi Kina ili kuchanganuliya data yetu. Data yetu tuliipata kwa kuwauliza wazee wa miyaka 50 na zaidi ambao wana maelezo simulizi kuhusu fasili za majina hayo na data ya upili. Kwa kulinganisha na lugha za jamii zinazokaribiyana za Kimvit̪a, Kimijikenra, Kipokomo na lugha za Kibantu kut̪oka bara Kenya tuliweza kung’amuwa kuwa majina haya ya Mambasa yanashabihiyana na yale ya lugha nyengine hivo kutupa ufunuwo mpya kuhusu maana za majina hayo. Tumepata kuwa ut̪amkaji wa majina unaleta t̪afaut̪i ya maana na hivo usuli wao piya ni t̪afaut̪i na ilivozoweleka. Tumepata kuwa majina ya kale yaliitwa kutegemeya maumbile ya mazingira na majina ya mitʰaa ya kisasa yameelemeya zaidi vitu au majengo yaliyoko hapo. Kupitiya makala haya tunaamini tumet̪owa fasili mpya kuhusu mitʰaa hii na hivo kuwapa fikira nyengine wataalamu wa Chimbo, Ut̪alii na Isimu kuhusu majina haya na historiya inayobebwa na majina haya.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdulaziz, M. H. (1979). Muyaka: 19th century Swahili popular poetry. Kenya Literature Bureau.

Antilla, R. (1989). Historical and comparative linguistics. John Benjamins Publishing Company.

Bynon, T. (1977). Historical linguistics. Cambridge University Press.

Campbell, L. (1998). Historical linguistics: An introduction. Edingburgh University Press.

Centre for Advanced Studies of African Society, (2012). A unified orthography for Bantu languages of Kenya. Monograph no. 249.

Helander, K. R. (h.t.). Renaming indigenous toponymy in official use in light of contact onomastic theories. Sami University College, Norway.

Hiistoriya, (2020, Jul 12). Who are the Swahili? [video file]. Imetolewa https://www.youtube.com/watch?v=pghUezn9FE4

Karama, M. R. (2021, June). Kugeuza d̪ira ya toponimi ya ‘Swahili’. The University of Kabianga Newsletter 1(5), 8-9.

Kindy, H. (1972). Life and politics in Mombasa. East African Publishing House.

Krapf, L. (1882). A dictionary of Suahili language. Trubner & Co.

Kresse, K. (2007). Philosophising in Mombasa: Knowledge, Islam and intellectual practice on the Swahili coast. Edinburgh University Press.

Makoti, V. S. (2007). Digo anthroponymes: Meaning and significance. Maarifa: A Journal of Humanities and Social Sciences 2 (1) 18-28.

Mazrui, A. A. (2012). What’s in a name?: European imperialism and the re-naming of Africa. Kandi ya A. Mazrui, State University of New York at Binghamton, New York.

Mindat.org. (2021, June). Ras Iwetine, Mombasa, Kenya. Ilisomwa kutoka https://www.mindat.org/feature-196036.html .

Mohamed, M. A. (2001). Modern Swahili grammar. East African Educational Publishers.

Mohamed, S. A. (2001). Babu alipofufuka. Jomo Kenyatta Foundation.

wa Mutiso, K. (2005). Utenzi wa Hamziyya. TUKI.

Mutua, M. (2021, June 20) It’s time to decolonise Kinyaa. Nation.Africa. Ilisomwa kutoka https://nation.africa/kenya/blogs-opinion/opinion/it-s-time-to-decolonise-kinyaa-3443516

Mwalonya, J., Nicolle, A., Nicolle, S. & Zimbu, J. (2004) Mgombato: Digo-English- Swahili dictionary. Bible Translation Literacy.

Numista, (2021, June 2). IBEA coinage.

Ilisomwa kutoka https://en.numista.com/catalogue/pieces8981.html

Nurse, D. & Spear, T. (1985). The Swahili: Reconstructing the history and language of an African society 800-1500. University of Pennsylvania Press.

Nzasu, J. & Odongo, W. (2014). Our county: Mombasa. Oxford University Press.

Owino, S. (2019, October 27). What’s in a name? Take heed in these legal views, implications. Kenyan Digest. https://kenyandigest.com/whats-in-a-name-take-heed-in-these-legal-views-implications/

Rose-Redwood, R., Alderman, D. & Azaryahu, M. (2010). Geographies of toponymic inscription: New directions in critical place-names studies. Progress in Human Geography 34(4), 453-470.

Sacleux, C. S. (1939). Dictionnaire Swahili-Francais. Institut d' Ethnologie.

Stigand, C. H. (1915). A grammar of dialectic changes in the Kiswahili language. Cambridge University Press.

Taylor, W. E. (1891). African aphorisms. Society for Promoting Christian Knowledge.

Tent, J. & Slatyer, H. (2009). Naming places on the Southland: European place-naming practices from 1606 to 1803. Australian Historical Studies 40(1), 5-31.

Tent, J. (2015). Approaches to research in toponymy. Names 63(2), 65-74. https://doi.org/10.1179/0027773814z.000000000103 .

Walsh, M. T. (2003). Hunter-gatherers in the hinterland of Mombasa: Notes on the Maumba of Chonyi and related traditions. Notes.

Wamitila, K. W. (1999). What’s in a name: Towards literary onomastics in Kiswahili literature. AAP 60, 35-44.

Wanjiru, M. W. & Matsubara, K. (2017). Street naming and the decolonisation of the urban landscape in post-colonial Nairobi. Journal of Cultural Geography 34(1), 1-23. https://doi.org/10.1080/08873631.2016.1203518.

Tarehe ya Uchapishaji
27 Julai, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Karama, M. (2021). Ni Mvit̪a ni Mvita?: Uchanganuzi wa Usuli wa Toponimi za Mitʰaa ya Mambasa, Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 3(1), 78-90. https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.368