Si T̪end̪i zot̪ʰe za Kabla ya Karne ya Ishirini ni Utambaji wa Kingano Nyengine ni Ufunzaji: Kiyelelezo cha Ut̪end̪i wa Siri li Asrari

  • Mohamed Karama Chuo Kikuu cha Kabianga
  • Rocha Chimerah Chuo Kikuu cha Kabianga
  • Kineene Mutiso Chuo Kikuu cha Kabianga
Keywords: Siri li Asrari, Utendi, Darasa, Hirizi, Islam
Sambaza Makala:

Ikisiri

Fikra iliyomo katika mawand̪a ya fasihi ya Kiswahili ni kuwa ut̪end̪i ni maelezo marefu ya mapisi ya jamii kiushairi. Makala haya yanat̪aka kuonesha kwamba si t̪end̪i zot̪ʰe zenye madhumuni haya. Kupitiya Ut̪end̪i wa Siri li Asrari tut̪aonesha kwamba mtʰunzi Mwanalemba alikuwa na niya t̪angu mwanzo ya kuweka d̪arasa kuhusu hirizi ya majina ya Mwenyezi Mungu. D̪arasa hii ameigawanya kama namna t̪aasisi za kielimu zinavopendekeza  ienreshwe kiskuli na ameyat̪owa mawazo yake kit̪aalamu. Nadhariya ya Usemezano kupitiya dhana ya Unrimi imetusaidiya kuuwangaziya ut̪end̪i huu na tumefaidika na vigezo va: maudhui, ut̪euzi wa misamiat̪i na mitinro ya uwasilishaji, na mukt̪adha wa matʰumizi ya maneno hayo kama njiya ya kutambuwa aina ya lugha inayotʰumika. Kwa kwangaziya mitinro ya uwasilishaji katika d̪arasa ya hirizi tumepata kujuwa kwamba mtʰunzi alikuwa na dhamira ya kutufunza badala ya kutamba hadithi ya kingano.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bakhtin, M. M. (1981). The dialogic imagination. Micheal H. (mtafsiri na mhariri) Austin: The University of Texas Press.

Bakhtin, M.M. (1986). Speech genres and other late essays. Caryl, E. & Micheal H., (wah.) Austin: The University of Texas Press.

Chimerah, R. M. (1989). The implications of the selected works of Ngugi in theeducational thinking and practices of Kenya. Tasnifu ya Uzamifu (Haijachapishwa). Ohio University, Ohio.

Dammann, P. E. (1940). Dichtungen in der Lamu mundart des Suaheli Band 28.Hamburg: Freiderichesen.

Mazrui. A. & Syambo, B. K. (1992). Uchambuzi wa fasihi. Nairobi: East AfricanEducational Publishers.

Njogu, K. & Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa fasihi: Nadharia na mbinu. Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation.

Shariff, I. N. (1984). Letters to the Editor. Katika Research in African Literatures, 15 (1), 150-156. Imesomwa https://www.jstor.org/stable/3819755 .

Shariff, I. N. (1988). Tungo zetu: Msingi wa mashairi na tungo nyenginezo. New Jersey: The Red Sea Press.

Tarehe ya Uchapishaji
26 June, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Karama, M., Chimerah, R., & Mutiso, K. (2021). Si T̪end̪i zot̪ʰe za Kabla ya Karne ya Ishirini ni Utambaji wa Kingano Nyengine ni Ufunzaji: Kiyelelezo cha Ut̪end̪i wa Siri li Asrari. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 3(1), 51-57. https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.349