Kimonro cha Mvuli asahau uume wake nrowa ni jamaa kinavowasilishwa katika Utendi wa Ramani ya Maisha ya Ndoa (Mume): Uchanganuzi Kifano

  • Mohameḍ Karama, PhD Chuo Kikuu cha Kabianga
Keywords: Utendi wa Ramani, Masemezano, Ujamaa, Taharuki, Mjadala
Sambaza Makala:

Ikisiri

Katika ṭaaluma ya fasihi ya kiSwahili uṭeṇḍi maarufu uliyoṭafiṭiwa mno kuhusu masiyala ya nrowa, kazi na majukumu ya mke k̇a mumewe, ni ule wa Ṁanakupona. K̇a mara ya k̇anza, makala haya yanaangaziya uṭeṇḍi ṁengine ambao haujaṭafiṭiwa k̇a ṭafsili wenye kuraṭibu kazi na majukumu ya mume k̇a mkewe. Utendi wa Ramani ya Maisha ya Ndoa (Mume) uliyotungwa na Usṭadh Mahmouḍ Mau unampa mvulana wasiya wa kutumiya katika kufaulisha nrowa yake. Makala haya yaṇjaribu kudhihirisha elimu ya kiḍini na hekima ya ṭajiriba ya kimaisha aliyonayo mtunzi k̇a kumnasihi mvuli kuwa hakuna ukʰuu katika nrowa. Makala haya yakiongozwa na nadhariya ya Usemezano yamechanganuwa maudhui ya hekima ya mtunzi na kubainisha kuwa: k̇enye mukṭadha wa nrowa mke na mume wanasemezana si wao peke yao bali na jamii k̇a ujumla; kuna mabaḍiliko ya maana ya maneno kila kukicha basi na maana ya uume piya inabaḍilika kila kukicha; na ṁishowe, maana inayokuja baaḍa ya kukaa nrani ya maisha ya nrowa huwa ṭafauṭi na ile ilozoweleka. Makala haya yanahiṭimisha kuwa mtunzi aliṭaka kumfunza mvulana na msichana kuwa maisha ya nrowa ni ya watʰu wawili lakini majukumu zaiḍi yanaṁangukiya mume katika kufaulisha nrowa yake. Isiṭoshe, uṭeṇḍi huu unamkazaniya mume amsome mkewe kila siku kila saa ili aweze k̇idhibiṭi nrowa. Naṭija ilopatikana k̇a kuushughulikiya uṭeṇḍi huu ni kubaḍilisha nadhari katika ṭaaluma za kiSwahili na kijinsiya k̇a k̇angaziwa sana Ṁanakupona na kuṭoṭafiṭiwa ṭʰeṇḍi nyenginezo haswa zinazotiliya maanani mtoto wa kiyume.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdulkadir, M. A., & Frankl, P. J. L. (2013). ‘Kiswahili’: A poem by Mahmoud AhmadAbdulkadir. Katika Swahili Forum 20, 1—18.

Abdulqadir, M. A. (2004). Utenzi wa ramani ya maisha ya ndoa (mke). Mswada haujachapishwa. Lamu.

Abdulqadir, M. A. (2004). Utenzi wa ramani ya maisha ya ndoa (mume). Mswada haujachapishwa. Lamu.

Ankal, N. N. (2013, April 30). Burudikeni na utenzi wa ramani ya maisha ya ndoa (mke). Facebook. https://tinyurl.com/mtue932h

Baalbaki, R. (1995). Al Mawrid: A modern Arabic-English dictionary. Dar El-Ilm Lilmalayin.

Bakhtin, M. M. (1981). The dialogic imagination. M. Holquist (mh.). The University of Texas Press.

Biersteker, A. (1991). Language poetry and power: A consideration of “Utendi wa Mwanakupona”. Katika K. W. Harrow (mh.) (1991) Faces of Islam in African literature (59—78). Heinamann Educational Books.

Bwanalemba, M. (1662). Das geheimnis der geheimnisse [Uṭeṇḍi wa siri li asrari]. Katika P. E. Dammann (1940). Dichtungen in der Lamu mundart des Suaheli Band 28. Freiderichesen.

Chiraghdin, S. (1987). Malenga wa karne moja. Longman Kenya.

Chiraghdin, S., & Mnyampala, M. (1977). Historia ya Kiswahili. Oxford University Press.

Cory, H. (1947). Jando. Part I: The Constitution and Organization of the Jando. Katika The Journal of the Royal Anthropological Institute of Great Britain and Ireland 77(2), 159—168.

Jamiiforums.com (2008, August 13). https://tinyurl.com/2d8jdv59 Ilisoṁa 23/02/2023

Kezilahabi, E. (1991). Mzingile. Vide~Muwa Publishers Limited.

Mazrui, A. & Njogu, K. (2022). Mikondo ya Kiswahili: Siasa, jamii na utandawazi. Twaweza Communications.

Mazrui, A. & Shariff, I. N. (1993). The Swahili: Idiom and identity of an African people. Africa World Press, Inc.

Mbaabu, I. (1985). Utamaduni wa Waswahili. Kenya Publishing & Book Marketing Co. Ltd.

Middleton, J. (1992). The world of the Swahili: An African mercantile civilization. New Haven/London: Yale University Press.

Mohamed, S. A. (2016). Mashetani wamerudi. Spotlight Publishers (EA) Limited.

Momanyi, C. (2019). Nguu za jadi. Queenex Publishers.

Mwamzandi, I. Y. (2018). Dhana ya zubu katika nyimbo za harusi za Waswahili: Uchambuzi wa kisaikolojia changanuzi. Katika Mulika 37, 45—58.

Nabhany, A. S. (h.t.). Manukato ya Wambeja. Mswada haujachapishwa. Mambasa.

Raia, A., & Vierke, C. (wah.) (2023). In this fragile world: Swahili poetry of commitment by Ustadh Mahmoud Mau. Katika Islam in Africa, 25, 1—396. https://brill.com/edcollbook-oa/title/62192

Shitemi, N. L. (2010). Mashairi ya kabla ya karne ya ishirini. Moi University Press.

Wandera-Simwa, S. P. (2021). Mwanamke wa Kiswahili katika utenzi wa Mwanakupona. Katika East African Journal of Swahili Studies 4 (1), 82—98. https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.422

Werner, A., & Hichens, W. (1934). The advice of Mwanakupona upon the wifely duty. Azania Press.

Tarehe ya Uchapishaji
19 April, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Karama, M. (2023). Kimonro cha Mvuli asahau uume wake nrowa ni jamaa kinavowasilishwa katika Utendi wa Ramani ya Maisha ya Ndoa (Mume): Uchanganuzi Kifano. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 101-118. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1181