Mtazamo Linganishi wa Itikadi katika Utenzi wa Mwanakupona na Mashairi ya Muyaka

  • Doreen Nkatha Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Jessee Murithi, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Mtindo, Lugha, Taarab
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii imechunguza itikadi katika Utenzi wa Mwanakupona na mashairi ya Muyaka. Itikadi ni mawazo ambayo hujumuisha malengo, matamanio na matarajio, na matendo ya mtu. Dhana ya itikadi pia imefasiriwa kama matamanio, fikra, malengo na maelezo ya mtunzi kuhusu masuala ya kijamii ya kisiasa, kidini, na kiuchumi kwa ujumla wake.  Hivyo, itikadi kama imani ambazo huelekeza matendo ya binadamu yeyote ulimwenguni zimewaathiri watunzi wa kazi hizi mbili kwa namna wanavyosawiri mitazamo yao kuhusu wanavyowasilisha. Huelekeza matendo yale mtunzi atakayowasilisha na namna atakavyowasilisha kazi yake. Utenzi wa Mwanakupona na mashairi ya Muyaka ni kazi zilizoandikwa katika kipindi kimoja lakini utofauti unajitokeza wa kimtindo. Kwa hivyo, ni muhimu kuchunguza na kuzilinganisha itikadi zilizowaongoza watunzi hawa. Nadharia ya itikadi; mikabala ya Karl Marx (1977), Louis Althusser (1981) na Antonio Gramsci (1985), ilitumika. Mkabala wa Karl Marx ulitumiwa sababu dhana ya "ung’amuzi potoshi," mkabala wa Althusser ulitumiwa kwani unaorodhesha vyombo vya kiitikadi na mkabala wa Gramsci ulitumiwa sababu ya dhana ya ukubalifu na ukawaida.  Data ya makala hii ilikusanywa maktabani. Vitabu teule, majarida na makala kuhusu mada husika mtandaoni yalisomwa kwa kina na kuchambuliwa. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Kutokana na data ya utafiti huu, imebainika kuwa itikadi zinazowaongoza Muyaka na Mwanakupona ni tofauti kwani wanasawiri kazi yao kwa namna tofauti ingawa walikuwa watunzi wa kipindi cha kirasimi. Muyaka ilibainika kuwa aliongozwa na itikadi ya mapinduzi ya nguvu, uhuru wa kiakili na ukandamizaji. Mwanakupona kwa upande mwingine imebainika ameongozwa na itikadi ya utiifu, ukubalifu na ukawaida na hata ubabedume. Makala hii inapendekeza kuwa tafiti zingine zaidi kuhusu itikadi zinaweza kufanywa kuhusu tenzi za mwanzoni na kuzilinganisha, mikabala mingine za itikadi pia inaweza kutumika na pia utafiti zaidi unaweza kufanywa kuhusu utenzi wa Mwanakupona kuhusu wanatapo wa tatu.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdulaziz, M. H. (1979). Muyaka: 19th century Swahili popular poetry. Nairobi, Kenya: Kenya Literature Bureau,

Althusser, L. (1981). Ideology and ideological state apparatuses. Katika Lenin and Other Essays. (B. Brewster, Mtaf.). London: New Left Books.

Finnegan, R. (1970). Oral literature in Africa. Cambridge: Oxford University Press.

Gramsci, A. (1985). Selections from cultural writings. London: Lawrence and Wishart.

Hoare, Q., & Smith, G. N. (Eds.). (1971). Selections from the prison notebooks of Antonio Gramsci. London: Lawrence and Wishart.

Marx, K. (1977). A contribution to the critique of political economy. Moscow: Progress Publishers, Moscow.

Marx, K., & Engels, F. (1977). The German ideology. London: Lawrence and Wishart.

Masinde, E. (2003). Ushairi wa Kiswahili: Maendeleo na mabadiliko ya maudhui. (Tasnifu ya Uzamifu: Haijachapishwa). Kenyatta University, Nairobi, Kenya.

Mohammed, S. A. (1995). Kunga za nathari ya Kiswahili: Tamthilia, riwaya na hadithi fupi. Nairobi, Kenya: East African Educational Publishers.

Mulokozi, M. M. (1999). Tenzi Tatu za Kale. Dar es salaam, Tanzania: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI).

Munyole, S. D. (2017). Usomaji na ufasiri sasa wa Utenzi wa Mwanakupona. Kutoka: http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/18245

Murithi, J. (2017). Itikadi Katika Riwaya za Said A. Mohamed. (Tasnifu ya uzamifu: Haijachapishwa) Kenyatta University, Nairobi, Kenya.

Njozi, H. (1990). Utendi wa Mwanakupona and reception aesthetics. Kiswahili. Juz. 57: 55-67.

Wafula, R. M., & Njogu, K. (2007). Nadharia za uhakiki wa fasihi. Nairobi, Kenya: The Jomo Kenyatta Foundation.

Williams, R. (1985). Keywords: A vocabulary of culture and society (Rev. ed.). New York, NY: Oxford University Press, New York.

Tarehe ya Uchapishaji
21 August, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Nkatha, D., & Murithi, J. (2025). Mtazamo Linganishi wa Itikadi katika Utenzi wa Mwanakupona na Mashairi ya Muyaka. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(2), 214-227. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3531