Nafasi ya Fasihi Katika Kuwasilisha Masuala ya Mazingira Kupitia Riwaya Teule Tikitimaji (2013) na Msimu wa Vipepeo (2006) za K. W. Wamitila

  • Esther Lucy Wesonga Chuo Kikuu cha Mlima Kenya
  • Beverlyne Asiko Ambuyo, PhD Chuo Kikuu cha Maseno
  • Rocha Chimerah, PhD Chuo Kikuu cha Pwani
Sambaza Makala:

Ikisiri

Suala la mabadiliko ya hali ya anga ni janga linaloendelea kukumba ulimwengu kwa jumla. Kutokuwepo kwa usawazishaji wa ekolojia ni jambo ambalo linawatia shaka adinasi wengi. Fasihi ni kioo cha jamii na inapaswa kuwasilisha hali halisi ya maisha ya binadamu. Utafiti huu unachambua nafasi ya fasihi katika kuwasilisha masuala ya mazingira kupitia riwaya mbili teule za Wamitila, Tikitimaji (2013) na Msimu Wa Vipepeo (2006). Mwandishi huyu ameonyesha ari katika uwanja wa fasihi mazingira, kwenye makala yake ya “Place and placelessness in Kiswahili literature: The role of setting in Kiswahili creative writing” anasema kuwa mandhari huchukua nafasi katika kuwasilisha masuala ya mazingira. Kazi hii ilichunguza namna mwandishi alivyotumia fasihi kuwasilisha masuala ya mazingira katika riwaya zake za hivi karibuni. Ingawa kwa miaka mingi, masuala ya mazingira yamehusishwa na sayansi haswa katika kutoa takwimu kamilifu kuhusiana na masuala ya mazingira, fasihi inaendelea kuchukua dhima mpya katika jamii inayozidi kukua kiteknolojia. Utafiti huu uliongozwa na madhumuni yafuatayo: kubainisha jinsi mwandishi wa riwaya ya Tikitimaji alivyotumia wahusika ili kuwasilisha maudhui ya mazingira. kueleza mitindo ya lugha iliyotumiwa kuwasilisha masuala ya mazingira na tatu, kutathimini iwapo mwandishi amefaulu kuwasilisha maudhui ya mazingira riwayani. Utafiti huu ulitumia kiunzi cha nadharia kutoka kwa nadharia ya fasihi mazingira na nadharia ya uhalisia. Mihimili zitakazotumiwa kutoka nadharia ya uhalisia ni: kazi ya fasihi imejitosheleza, kazi ya msanii inapaswa kuwasilisha ukweli, mtunzi anaangalia matatizo na kuchunguza chanzo chake na mwisho wahusika ni vielelezo yakini vya binadamu wa kawaida kwa vile wao hutumia lugha ya kawaida wanayoitumia humwezesha mwanadamu kujifafanulia uwezo wake wa kutenda mambo. Mihimili ya fasihi mazingira iliyotumika ni: kuangalia dhana za ekolojia katika kazi za fasihi, mitindo na uwezo wa lugha na jinsi mitindo hiyo huathiri namna binadamu anavyotagusana na mazingira  na mwisho binadamu hawezi ishi bila ekolojia lakini ekolojia huweza kuishi bila binadamu. Data ilipangwa kwenye makundi na kuchanganuliwa kwa kuzingatia madhumuni ya utafiti na mihimili ya kiunzi cha nadharia. Data iliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu umelenga kuhamasisha wasomi na waandishi wa fasihi wajikite zaidi kulenga masuala ya mazingira ambayo ndicho kitovu cha maisha ya binadamu. Utafiti ulibaini kuwa fasihi ni nyenzo mwafaka ya kuwasilisha masuala ya mazingira kupitia vipengele vyake. Kwani huingiliana sana na utamaduni wa jamii.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Adamson, J., & Slovic, S. (2009). Guest editors' introduction the shoulders we stand on: an introduction to ethnicity and ecocriticism. Melus, 34(2), 5-24.

Baek, J., Cho, Y., & Koo, W. W. (2009). The environmental consequences of globalization: A country-specific time-series analysis. Ecological Economics, 68(8-9), 2255-2264.

Barry, P. (1995). Beginning Theory: An introduction to literary and cultural theory. Manchester: Manchester University Press.

Beull, L. (1995). The Environmental Imagination: Thoreau, nature writing, and the formation of American culture. Cambridge University Press.

Cresswell, J. (2009). Research design: Quantitative, qualitative mixed-method approaches. Los Angels: SAGE publication.

Glotfelty, C. & Harold, F. (1996). The ecocriticism reader: Landmarks in Literary Ecology. Athens: University of Georgia Press.

Greg, G. (2004). Ecocriticism. London and New York: Routledge.

Greenblatt, S. (1992). Marvellous Possessions: The wonder of the New World: Chicago University Press.

IPCC. (2013). Climate change 2013:The Physical Science Basis. Contribution of working group 1 to the Fifth Assessment Report of the New York, NY, USA: Cambridge University Press.Available: http://www.climatechange2013.org/images/uploads/WGS_AR5_SPM_Bronchure.pdf.

IPCC (2014).Climate Change 2014: Mitigation of climate of Climate Change Working Group III Contribution to the Fifth Assessment Report of the Intergovernmental Panel on Climate change. Cambridge University Press; New York: 2014 chap AnnexII.2 [Google Scholar]

Kavila, F. S. (2013). The Theme of Environmental Conservation in Different Colours and Terrorists of the Aberdare by Ng’ang’a Mbugua. Doctoral dissertation. University of Nairobi.

Mohamed, S. A. (2001). Babu Alipofufuka. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Moore, N. (2008). Eco/feminism, non-violence and the Future of Feminism. International Journal of Politics, 10(3), 282-298.

Nixon, N. S., & Ronald, O. N. (2014). Literary environmentalism: An ecocritique of Kiswahili literature. International Journal of Ecology and Ecosolution, 1(2), 29-41.

Njogu, K & Chimera, R. (1999). Ufundishaji wa fasihi: Nadharia na mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Ntarangwi, M. (2004). Uhakiki wa kazi za fasihi. Rock Island: Augustana college:.

Nwagbara, U. (2010). Poetics of Resistance: Ecocritical reading of Ojaide’s poems “Delta Blues and Home Songs and Daydream of Ants and other poems.” African study monographs, 31 (1), 17-30.

Reuveny, R. (2007). Climate Change-induced migration and violent conflict. Political geography 26, 656-67.

Rigby, K. (2007). Ecocriticism: introducing ecocriticism in the twenty-first century. Edinburgh: UP.

Rueckert, W. (1978). Literature and Ecology: An Experiment in Ecocriticism. Athens: University of Georgia Press

Sabula, M. A. (2014). Nafasi ya wanawake katika uhifadhi wa mazingira katika riwaya ya Nakuruto: mtazamo wa fasihi ya ufeministi wa kiekolojia. Chuo Kikuu cha Nairobi

Vasquez, A. (1983). Art and Society in Essays in Marxist Aesthetics. New York: Monthly Review Press.

UNFCC. 2009. Decisionx.CP.15 Methodological guidance for activities relating to reducing emissions from deforestation and forest degradation and the role of conservation, sustainable management forests and enhancements of forests carbon stocks in developing countries. FCC/CP/2009/11Add.1,decision4/CP.15. Retrieved from http://unfccc.int/files/na/application/pdf/cop15 ddc auv.pdf. Accessed 07/08/2017.

Wa Mberia, K. (2001). Bara Jingine. Nairobi: Mariba publications.

Wafula, R. M., & Njogu, K. (2007). Nadharia za uhakiki wa fasihi. Nairobi, KE: Jomo Kenyatta Foundation.

Wamitila, K. W. (2004). Kichocheo cha fasihi simulizi na Andishi. Focus publishers.

Wamitila, K. W. (2006). Msimu wa vipepeo. Nairobi : Vide-Muwa Publishers

Wamitila, K. W. (2013). Tikitimaji. Nairobi: Vide Muwa publishers.

Wanyonyi, A. (2009). Sintaksia, italiki, lugha ya kitamathali, Tasfida, Ishara za uwashiriaji na masuala balagha katika riwaya ya Nyuso Za Mwanamke. Tasnifu ya Uzamili (haijachapishwa). Chuo kikuu cha Nairobi.

Wu, C. C. (2016). Towards an Africa-Focused Ecocriticism: The Case of Nigeria. Doctoral dissertation. Chuo Kikuu cha Nevada, Reno.

Tarehe ya Uchapishaji
11 August, 2020
Jinsi ya Kunukuu
Wesonga, E., Ambuyo, B., & Chimerah, R. (2020). Nafasi ya Fasihi Katika Kuwasilisha Masuala ya Mazingira Kupitia Riwaya Teule Tikitimaji (2013) na Msimu wa Vipepeo (2006) za K. W. Wamitila. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 2(2), 54-64. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.192